Ushauri: Rais Samia apumzike Urais 2025

Uko sahihi kabisa, nimewahi kusema huko nyuma kwenye post mbalimbali. Ubovu wote wa mifumo na udhaifu ndani ya nchi hii unaletwa na katiba ya rais Mungu mtu. Ukifuatilia vizuri bunge na mahakama inayosemwa ni mihimili inayojitegemea, yote udhaifu ni kwa sababu ya madaraka ya urais.

Kwa sasa kwenye nchi yetu amri toka juu ndio yenye nguvu kuliko katiba na sheria. Na hii amri toka hutoka kwa rais ambaye huweza kutumia vyombo vya dola kuviagiza kufanya lolote. Ilitakiwa rais apewe nguvu ya kuagiza vyombo vya dola kuingia vitani tu na sio kwenda kukomoa watu. Na iwapo akitaka kuagiza vyombo vya dola vifanye kazi fulani aombe ruhusa ya mahakama, na atoe sababu za kisheria kufanya hivyo. Sio rais kuagiza usalama wa taifa kuteka watu wanaomkosoa, au kuzuia hata mambo yaliyoko kisheria kisa ni hatari kwa madaraka yake na chama chake.
 
Nami nikaona Gari kubwa likiteremka Kutoka mlimani limefunikwa bendera ya Taifa , naliona watu wengi wenye nyuso za furaha wanapunga matawi ya miti na kuimba nyimbo za furaha wakilisindikiza gari Hilo.

Nikastuka ghafula, kumbe ni ndoto tu.
 
Baba alituonyesha kua hii nchi inautajiri mkubwa sana na tunaweza jiendesha wenyewe ila sasa ni majanga tupu. ..matajiri hela waliochukuliwa kipindi cha baba sasa wanairejesha tena kinguvu utake usitake utailipa
 
Tusikubali tena kuongozwa na mtu asiye na ndoa rasmi
 
Tulia dozi ikuingie,kwani Mungu ni WA chadomo na sukuma gang pekee? 😆😆
Nakushauri tu kwa kuwa akili unazo ila mapenzi yanakuzidia na nahisi kwa kuwa unafaidika na uongozi kwa namna moja ama nyingine. Ukikaa chini na kutafakari kwa kina yakupasa kuyatambua haya.
1. Hali na mwelekeo wa upepo wa kisiasa kwa mama siyo mzuri hivyo mshauri ajipange asiaminishwe na chawa au walamba asali. ( sifaidiki na kupoteza kwake kiti hivyo namuombea mema)
2. Wakati mwingine jitahidi kuuona ukweli kwenye thread za watu hata kama zinakuumiza (ukweli ulio mchungu utakusaidia kutafuta tiba kuliko uongo mtamu utakaokudumaza).
3. Mi siyo muumini wa chama fulani ila mnakosa uadilifu kwa kushindwa kuchukua lililo jema hata kama limetolewa na asiyemuumini wa chama chenu. ( mazuri huigwana mabaya huachwa)
4. Rais siyo Perfect na wanaomzunguka siyo malaika hivyo awapime hata kwa kutumia vyombo vyake vya dola kufuatilia fikra zao juu ya wanayoyaanzisha na kuja kulalamikiwa vikali na wananchi.
5. Fadhira ni nzuri ila siyo kwa wanaokuangusha ama lazima watoke kwenye jamii ya watu fulani, awe na kundi maalumu la wanaofuatilia watu wanaostahili uongozi kama wafanyavyo watu wa mchezo wa mpira miguu / kikapu.
6. Kuvaa tai yenye bendera ya taifa kwa kofia ya uzalendo ni mbinu tu we fuatilia matendo yao ni kama wale waliokuwa wakitembea na katiba ya nchi kila mahali.
7. Wengi wa wanaosifu kwa kuimba na kucheza ni wanaofaidika ( rejea mei mosi 2 zilizopita reactions zake) na response baada ya nyongeza kuwekwa, ama rejea hotuba ya Waziri wa fedha na mipango akisoma bajeti watu walivyodemka.
8. Mwisho nakutafakarisha kuhusu wananchi. ( Waandishi wa habari wanahujumu kwa kutochukua picha vizuri kuonesha nyomi la watu ). Ni ziara ya kuzindua mradi lkn unaletewa kikundi cha hamasa kama vile ni sherehe za kitaifa (kuna tatzo hapo).
 
Ndio ilivyo kote huko hata Duniani ndio maana ya kuwa na manifesto za vyama.

Manifesto ziko kufuata formalities tu, lakini utekelezaji ni utashi wa rais. Mfano halisi, manifesto ya CCM ya 2015-2020 ilisema mabinti watakaojifungua watarejea shule, lakini Magufuli si aligoma tena akiongea kwa kejeli jukwaani kuwa hasomeshi wazazi, na hakuna mwanaccm alimwambia manifesto imeruhusu? Ni mpaka mashinikizo toka nje ndio ikawa inatafutwa lugha ya zimamoto kuwa watatafutiwa elimu maalum nje ya utaratibu wa kawaida,?

Hebu niambie ni kipi rais atashindwa kufanya akitaka kisa manifesto imesema?
 
Magufuli hakuwa anafuata sheria yeyote,pili manifesto haziko kisheria ila zinatakiwa kusisitizwa na vyama husika.
 
Umeandika ujinga mtupu..

Nataka unile deadline umesema mwisho wa Samia kuwepo madarakani ni lini? Nataka niweke Kumbukumbu sawa.
 
Akijerekebisha katika mambo yafuatayo atafaa kuendelea ila kama hawezi akae pembeni

1. Ajirekebishe kwenye teuzi, inaelekea anajiteulia tu bila kujali anaowateua wanakubalika vipi na wananchi. Teuzi za watu kama Kingai ni aibu yake

2. Apunguze kukopa nje, Haya mamikopo wanayokopa utafikiri hakuna kesho yakimature ndo wanahaha kutupoka savings zetu kupitia matozo yasiyo na maana

3. Aache kuendesha operesheni bila kupima athari za maisha ya watu, opeesheni za kondoa wamchinga bila kuwapa alternative nzuri, na operesheni iliyojaa uonevu mkubwa dhidi ya wamasai haikuwa sahihi kuzifanya.

4. Atumie kidogo tulichonacho wisely, abane matumizi, kutumia bilion 629 kufanya sensa wakati watu hawana maji safi na salama ya kunywa, vijana hawana ajira, watoto wanakosa mikopo vyuo vikuu , hatuna umeme wa kutosha, barabara ni mbovu huo ni ujinga!

5. Awe sensitive na maisha yetu, haya matozo, makodi yasiyokuwa na kichwa wala miguu hatuyataki. Kama anataka hela inabidi abane matumizi na apunguze ukubwa wa serikali yake

6. Kuna upigaji mwingi ktk seriksli yake, mafisadi yenye njaa yametoka kifungoni yana njaa kwelikweli. Adhibiti ufisadi

7. Tunataka katiba mpya, kama hawezi kuideliver akae pembeni
 
Hili swala la kusema anashauriwa vibaya linanikera balaa,kwamba yeye haoni,hasikii, hatumii akili zake ama vipi?

Jukumu la kuongoza nchi linahitaji mwanaume wa ukweli huo ndo ukweli pasipokupindisha maneno rais kwa sasa kapwaya,naunga hoja Mwinyi wa zanzibar kama Mungu ataendelea kumuweka hai hadi miaka hiyo arudi huku Tanganyika.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Akina Kabudi na Lukuvi ni maelekezo ambayo yalikuwa hivyo. Mafisadi wenyewe wenyewe kabisa....😁 Hao inakuwa ngumu. Nchi itatikisika.
 
Hii ni namna nyingine ya kumdharau Rais. Maana yake yeye hana uwezo so kuna wanaomwendesha.
 
Reactions: nao

Kocha mzuri ndio huyo anaetakiwa kujua kwamba tatizo la wachezaji wake ni mbio na achukue hatua stahiki kurekebisha Hilo.
 

Hao tu ndio wanastahili kuwa marais wa nchi hii?
 
Hii ni namna nyingine ya kumdharau Rais. Maana yake yeye hana uwezo so kuna wanaomwendesha.

Chembe chembe za siasa za ujamaa hayo ndio madhara yake, jambo likifanyika vizuri wapambe wake wanawahi kumsifia kuwa ni rais kafanya hata kama sio yeye. Ila mambo yakienda vibaya lawama wanatupiwa wengine, mara sijui washauri wake na uhuni mwingine kama huo.

Hizi tabia za kumfanya rais kuwa ni Mungu mtu, tunaziona pia kwenye fedha za maendeleo, zikitoka hata kama ni za mikopo zinaitwa ni fedha za rais, lakini madeni sio ya rais bali ni ya wananchi!
 
Kwanza niseme wazi Mama ni moja ya Marais bora kabisa kuwai kutokea katika taifa letu. Sijawai kusikia kashifa yeyote ya wizi na ufisadi kutoka kwake, ni Rais mwadilifu kweli kweli.

Hapo umenena mkuu.
 

Rais Samia apumzike Urais 2025 vinginevyo ataiweka ccm mahali pagumu sana.​

Ukitarajia kuwa kuna mwanaccm anayetarajia kuhamia upinzani kuchuana naye.​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…