Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Uko sahihi kabisa, nimewahi kusema huko nyuma kwenye post mbalimbali. Ubovu wote wa mifumo na udhaifu ndani ya nchi hii unaletwa na katiba ya rais Mungu mtu. Ukifuatilia vizuri bunge na mahakama inayosemwa ni mihimili inayojitegemea, yote udhaifu ni kwa sababu ya madaraka ya urais.Misingi ya kutegemea kudra na hisani za kiongozi ili kupata suluhu ya matatizo yetu ndo chanzo mpaka Sasa tupo hapa tulipo pasi kuzingatia sheria na kanuni zinataka nini au zina toa muongozo gani kuhusu jambo hilo.kama taifa ni muda Sasa kuunda misingi bora ya kuzingatia sheria na kanuni kwa kuweka mifumo imara yenye uwajibikaji na kila mtu anapaswa kuwajibika kulingana na sheria na kanuni.
Tabia za kuona viongozi Kama miungu watu ndo imeleta shida mbalimbali mfano leo hii shida ya kukatika kwa umeme hovyo hovyo lawama zote kwa rais ,ufisadi katika miradi mbalimbali ya umma lawama zote kwa rais wakati Kuna TAKUKURU na muda huo huo ana wasaidizi kibao chini yake hili ni zao la katiba yetu ambapo rais anapewa nguvu katika kila kitu hivyo jambo lolote ili lifanyiwe kazi lazima pawepo msukumo wa kauli ya rais.
mfumo wa check and balance haupo katika nchi yetu hivyo dhana ya uwajibikaji wa kila mihimiri ya serikali kuwa hovyo.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwa sasa kwenye nchi yetu amri toka juu ndio yenye nguvu kuliko katiba na sheria. Na hii amri toka hutoka kwa rais ambaye huweza kutumia vyombo vya dola kuviagiza kufanya lolote. Ilitakiwa rais apewe nguvu ya kuagiza vyombo vya dola kuingia vitani tu na sio kwenda kukomoa watu. Na iwapo akitaka kuagiza vyombo vya dola vifanye kazi fulani aombe ruhusa ya mahakama, na atoe sababu za kisheria kufanya hivyo. Sio rais kuagiza usalama wa taifa kuteka watu wanaomkosoa, au kuzuia hata mambo yaliyoko kisheria kisa ni hatari kwa madaraka yake na chama chake.