Ushauri: Rais Samia itisha kura ya maoni kupitia akaunti yako ya X kuhusu suala la Bandari, utapata picha halisi na ikusaidie kufanya maamuzi

Ushauri: Rais Samia itisha kura ya maoni kupitia akaunti yako ya X kuhusu suala la Bandari, utapata picha halisi na ikusaidie kufanya maamuzi

Au afuatilie mikutano ya CHADEMA Nchi nzima,

Wanapiga kura ya WAZI, Kwa wanaopinga na wanaokubali mkataba wa DP World.

Hadi sasa, hajatokea hata mmoja mwenye kuukubali mkataba Ule fake na BATILI.

Wote wanasema HAPANA waziwazi akiwemo Kishimba PM.
Sijui wamepewa nini hawa viongozi na hawa waarabu!!!
 
Mhe, Rais, kama unavyopenda kutumia mtandao wa X kuelezea mambo yanayohusu nchi na watanzania ikiwemo kutoa taarifa mbalimbali za Serikali yako, nakushauri utumie mtandao huo kupata maoni ya wananchi ni namna gani wameupokea mkataba wa Bandari ambao umekuwa gumzo kuu hapa nchini.

Mhe. Rais ,mijadala mingi inaibuka na kupita, ila huu wa Bandari ni wazi umekuwa na utakuwa endelevu, hivyo fanya jambo la tofauti ,na hili si lingine bali kuitisha kura ya maoni isiyo rasimi kupitia mitandao na hapa napendekeza utumie mtandao wa twitter au ukiweza kupitia hapa JamiiForums vile vile.

Au ikiwezekana, jukumu hilo wape wasaidizi wako kama vile Msemaji wa Serikali ambae nae ana akaunti X

Swali la msingi liwe ni je, unaunnga mkono mkataba huu wa uwekezaji kwenye bandari zetu?

Majibu yawe ni ya kuchagua kati ya haya yafuatayo:

1. NDIO
2.HAPANA
3.SIJUI

Hilo swali mnaweza kuliuiza kwa kuliandika mnavyoona inafaa, ila ujumbe uwe ni huo huo.

Mhe. Rais, nukuu hii hapa chini ya Baba wa Taifa ikuongoze.

Julius Nyerere: Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo.
Kipi cha maana kilichompeleka , huko urabuni
 
Ishu sio nani anataka na nani hataki aaah! Ishu ni Moja tu lazima do world wapewe
 
Kwa maana iyo bibi,shangazi, njomba wangu n babu hawana haki ya kupiga kura? Kwakua hawana mtandao X?
 
Pengine sababu zinazofanya ashindwe au aone aibu kusitisha zipo nyuma ya pazia ama huwenda zipo nje uwezo wake au akisitisha yaliyonyuma ya pazia yatawelwa wazi na yatamfedhehesha sana na kulitia aibu taifa
UKISHAAKULA VYA WATU LAZIMA UONE AIBU
 
Ujinga mtupu.....

Yaani kila uamuzi wa serikali...uwekezaji uitishwe kura ya maoni ?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Uuzwaji wa benki ya NBC....hakukuwa na kura ya maoni...

Ushirikiano wa serikali na barricks katika migodi....hakukuwa na kura ya maoni.....

IPTL je ?!!

Escrow je ?!!

Ununuzi wa ndege za serikali je ?!!

Ujenzi wa MNHEEP je ?!!

Ujenzi wa SGR je ?!!!

Hizi siasa za kiliberali wakati mwingine ni za "kichoookooor" sana [emoji1787][emoji1787]

Karibu wanzuki [emoji120]
 
Atakuja kujilamu kama alivyofanya Mkapa kwenye kitabu chake na hawa kina Zitto watakuwa ni wasomaji tu kama watu wengine.

Sisi tunamkosoa na kumpa ushauri.
Haturudi nyuma....

Tuziache TRILIONI 26 kila "fiscal year"?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Baaambaash
 
Umesemaje eti?
Uko dunia gani wewe?!! [emoji1787]
images%20(16).jpg
images%20(15).jpg
 
Back
Top Bottom