Nakubaliana na wewe kwenye baadhi ya mambo ila kuna mengine sikubaliani kabisa na wewe
Mosi, hawa jamaa ni watendaji wakuu kwenye HALMASHAURI mfano miradi mingi mtambuka kama miradi ya Tasaf, ujenzi wa madarasa, usimamizi wa rasilimali watu, kuhamasisha maendeleo, kushiriki mazoezi ya kitaifa kama vile SENSA, uchaguzi, mwenge n.k ni uzoefu adimu sana kupata kwa masenior wanaokaa Ofisini hawajui mambo mengi
Mbili, Maafisa Elimu Kata wananyumbuka sana kutokana na nafasi zao. Ni kweli Mkurugenzi na Katibu utawala wa Wilaya ni nafasi zinazotakiwa unyumbukaji sana maana anadeal na zaidi ya Idara moja. Maafisa hawa kwa uzoefu wanaoupata wanaweza kuicheza ngoma hii kwa ufasaha kwani karibuni mazoezi mengi yanayofanywa na serikali kwenye ngazi ya jamii wanashiriki moja kwa moja.
Ukiachana na mambo mengine, hawa jamaa ni seniors kwenye idara zao. Maana yake walishatumika sana kwenye nafasi ya ualimu, ukuu wa shule na hatimae wamekuwa Maafisa Elimu kata. Kiukweli inahitajika upembuzi wa kina lakini hawa jamaa wanaweza na wenye sifa wapo isipokuwa wa kuwapigia debe ndio hawapo