Ushauri: Rais Samia mpe kazi Prof. Anna Tibaijuka, ana uzoefu mkubwa sana wa masuala ya utumishi

Ushauri: Rais Samia mpe kazi Prof. Anna Tibaijuka, ana uzoefu mkubwa sana wa masuala ya utumishi

Naona Watu wanazunguka ukweli kwa mbaliiii.....
Balozi Mulamula, Kabudi, Jerry Slaa,....orodha ni ndefu, awamu hii ukiwa "smart upstairs" wewe ni adui by nature!
 
Ushauri wangu kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia ampe tena kazi Prof Anna Tibaijuka kwasababu ana uzoefu mkubwa sana wa masuala ya utumishi akili kubwa kama hii isistaafu mapema

Prof Tibaijuka ana uwezo mkubwa sana wa masuala ya utumishi vilevile anaweza kuwa kama mama mwenye busara

Kwa miaka mingi sana nimekuwa nikimfuatilia katika speech zake niligundua ana akili sana lakini nikasikitika kuona hayupo tena kwenye mfumo wa Serikali

Huyu Profesa Tibaijuka ana uzoefu mkubwa sana wa masuala ya nje na ndani ya nchi na anaweza kutufikisha mahali tunapostahili

Binafsi nashauri apewe angalao hata Wizara moja hakikia tutavuna kitu kutoka kwake
Uzoefu sio ishu, nadhani ampe ili amuweke karibu. Huyu mama akiruhusiwa press conference kama nne tu upepo wa kisiasa utabadilika.
 
A
kili nyingi za kuhongwa milioni kumi na kusema ni pesa ya mboga? Alikuwa wizara ya Ardhi nini ulifanya?
Swala la kusema ni hela ya mboga ni kawaida sana kwasababu sifa ya kiongozi lazima uwe na uwezo wa fedha, huwezi kuongoza watu wakakuelewa kama ni maskini sana lakini kiongozi akiwa na uwezo wa fedha inampa sifa, kashfa ya hela ya mboga sio kosa kusema hivyo alitaka kuonesha uwezo wake wa fedha kwamba ana nguvu kubwa ya kiuchumi na hiyo ni sifa ya kiongozi
Mfano Marekani hawataki kiongozi maskini
 
Tibaijuka hawezi kuwa chini ya mama. Yeye ndo alipaswa aongoze nchi sio yeye aongozwe. Akili nyingi sana yule bibi.
Akili nyingi kafanya nn Cha maana ? Wenye akili ni wale wa pale Dubai ,Singapore na china ...Miaka ya 90's nchi zao zilikuwa kawaida ila ona Sasa.

Wenzenu Wana uwezo wa kuiba maarifa huyo profesa wako kazi kukariri ,anaamini kutegemea wazungu milele ...Elimu au ujinga ?
 
Hakufanya vibaya kukosoa kwasababu hoja zake ni za msingi sana, alitaka kukumbushia swala la rasilimali na hasa ardhi huwa haiongezeki bali watu ndiyo wanaongezeka, kwahiyo tujifunze kutunza rasilimali zetu tusizigawe kwa watu kwani tutabaki mikono mitupu

Mtu akikushauri usiuze mali zako kwasababu utakuwa masikini huko mbeleni amekosea? Hapana hajakosea bali amekufungua akili kwamba ukifanya hivyo umaskini utakuandama
 
Akili nyingi kafanya nn Cha maana ? Wenye akili ni wale wa pale Dubai ,Singapore na china ...Miaka ya 90's nchi zao zilikuwa kawaida ila ona Sasa.

Wenzenu Wana uwezo wa kuiba maarifa huyo profesa wako kazi kukariri ,anaamini kutegemea wazungu milele ...Elimu au ujinga ?
Aliyefanya ni nani sasa! Nchi za Afrika ni nchi zinazoendelea bado hatujafikia hatua ya kusema kafanya nini, bado zinahitaji kujengwa ndiyo maana ukimtafuta aliyefanya hutampata
 
Aliyefanya ni nani sasa! Nchi za Afrika ni nchi zinazoendelea bado hatujafikia hatua ya kusema kafanya nini, bado zinahitaji kujengwa ndiyo maana ukimtafuta aliyefanya hutampata
Bado mdogo sana ,bado una akili za kukariri ...Huyo profesa wako Hana hata Cha kumzidi Lipumba ,ila Lipumba ni chenga tu kama yeye ...kuwa makini sana wenzenu walijitoa kwa uzalendo :Fuatilia speech ya kiongozi wa Singapore!

Tibaijuika nje ya kukariri Hana kipya alitakiwa kuwa na kampuni au taasisi binafsi sio kupokea hongo na kubwatuka...Alipotokq kweny mfumo akaanza kuongea shombo ..

Kiufupi hamna kitu ana elimu ya kizamani.
 
Back
Top Bottom