Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Habari wadau! Katika mihangaiko ya hapa na pale kuna binti nilimkuta mahali, kifupi nikamtamani na nikataka nipite tu.

Baada ya mbinu za hapa na pale, alinipa namba na tukajikuta penzini, baada ya mawasiliano ya kama wiki, nilimwambia aje home..nilitaka kula mzigo akabana, na mm kulazimisha huwa siwezi na ukizingatia sikumuelewa kabisa ikabidi nimpotezee mazima.

Yule binti baada ya hapo hakukata tamaa aliendelea kunitafuta mara kwa mara, kila mara alikuwa akianza yeye, pamoja na kumchunia kote hakukata tamaa na kipindi hicho alikuwa hayupo tena mkoa niliokuwepo!

Muda ulienda ikapita kama miaka miwili, mimi juhudi zangu za kupata mwenzi zikawa zinagonga mwamba, kuna wakati uchumi wangu uliyumba sana na kwa vyovyote nilikuwa nahitaji mtu wa kusimamia shughuli zangu ili mimi nipambane kivingine.

Huyu binti nilimpanga nianze kuishi naye akakubali, hapo kiukweli moyo haukuwepo kabisa kwake, kilichonivuta kwake ni ule uvumilivu na kutoomba hela kabisa. Nikajipa moyo pengine nitampenda nikianza kuishi naye.

Baada ya kama miezi mitatu, alipata ujauzito na mm mambo yangu angalau yakaanza kwenda mbele. Hapo kuna mwanamke wangu ambaye alikuwa bado A level nilikuwa nachatt naye bado. Kuna siku alikuta sms, akatishia kuondoka alafunga mpaka mabegi, nikaona isiwe kesi nikaomba msamaha nikaita mpaka mtu akaniombea msamaha maisha yakaendelea.

Wakuu kuishi na mtu usie na hisia naye ni kazi sana, nikawa naona yote nafanya kumfurahisha yeye tu, kweli ananipenda sawa lakini kwangu je? Nitajidanganya mpaka lini, nikawa nawaza sana hivi huyu kweli ndo wa kufa na kuzikana? Kifupi sikuwahi kuwa proud na yeye hata siku moja, mapenzi yakageuka mateso bila chuki, hakuna kitu kigumu kama unalala na kuamka na mtu ambaye humpendi na wala huna hisia naye

Miezi ilienda mimba ikawa kubwa ikabidi arudi kwao kujifungua, hapo kwao hawanifahamu zaidi ya kuwasiliana na dada ake. Miezi ilienda akajifungua mtoto wa kike, copy yangu kabisa..furaha yake ilikuwa kubwa ila mm kwangu ilikuwa tofauti nikawa nawaza sana hatma yetu.

Ilipita miezi kadhaa nikawafuata wakarudi nyumbani, hapo furaha sina najilazimisha tu. Mwanamke naye akaanza visirani vya hapa na pale, tatizo dogo mara atishie kurudi kwao, mara naenda lini kujitambulisha (moyoni nikawa najisemea huyu angejua).

Basi kuna siku katika pita pita huko mtaani kuna binti nikapata namba yake nikaanza kumtongoza kwa kutumia kisimu kidogo, sms inbox nikawa nafuta dah kumbe nilisahau kusett sent item zijifute, basi kwenye pekua pekua yake akakuta zile sms, akalia sana mara mimi nataka kumuua sijui mtoto mdogo n maneno mengine mengi sana.(kifupi toka nimekuwa naye sikuwahi chepuka kabisa). Basi baada ya hapo minuno ikaanza, nikijaribu kujirudi anakaza, nikasema poa isiwe shida.

Siku moja niliamka asubuh, sikumsemesha kitu akaweka maji bafuni sikuoga wala chai aliyoandaa sikunywa nikaondoka zangu, baadaye akatuma sms kwa haya maisha yamemchosha nikamwambia sawa, akataka nauli na mtaji. Nikamwambia mm nina nauli tu, akasema bila mtaji haondoki nikamwambia nauli hiyo hapo, ukiondoka sawa usipoondoka sawa ni wewe.

Kweli akakusanya mazaga yake, asubuh nikawapeleka ubt, wakaondoka. Niseme tu ukweli siku hiyo nilijihisi kutua mzigo mzito sana, nafsi ikawa nyeupe sana, japo nilijua nilimkosea na kumpotezea muda lakini ningefanyeje.

Sasa baada ya kuondoka haikupita hata wiki akaanza kuomba kurudi na kuomba msamaha sana. Kiukweli mimi sikuwa tayari, niligoma na sasa ni mwaka umepita tangu aondoke, kifupi bado sijapata mwanamke wa kueleweka atakayetuliza moyo wangu, kwenye hili wala sina haraka najipa moyo nitampata tu hata kama nitatumia miaka kumpata.

Sasa changamoto inakuja huyu mama wa mtoto wangu, bado hajakata tamaa mpka leo anaamini atarudi kwangu, kumwambia ukweli kwamba simpendi naona itamuumiza sana na hii sioni kama ni option nzuri.

Kwa wazoefu wa mambo, nitumie njia gani kumfanya huyu mwanamke aendelee na maisha yake, najua anadeserve furaha na kupendwa, but kwangu hivyo havipo na kamwe hatakuja kuvipata. Je nitumie njia gani kumuweka ajue kwamba hana nafasi kwenye maisha yangu.
Umemdanganya binti wa watu na ukaona haitoshi umekuja kutudanganya Great Thinkers hapa jukwaani.

Kiufupi unampenda, lakini baada ya kumzalisha ushapata demu mpya na sasa unatafuta mbinu ya kummwaga mzazi mwenzio.

Mtoto kosa lake ni nyie wazazi kuamua kutumia njia za mkato kumpata au nini?

Nipe kazi ya ushenga tukachukue jiko
 
Mkuu acha ujinga....nasema tena acha ujinga....yaani umzalishe mtoto wa watu then unataka kumuacha kirahisi hivyo then unatafuta ambaye hajazaaaaa....

Hapo unafanya makosa, sikia jipe muda endelea kumchunguza unaweza kuta huyo ni bora kuliko huyo wa advance atakayeenda chuo akakutane na wajuba baadaye aje akuumize kichwa.......
h
 
Nikwambie tu ukweli ulifanya jambo la kipumbavu kucheza na hisia zake. If you are not happy just leave,why playing with people's feelings, mm sikushauri ila ujue umefanya makosa
 
Umemdanganya binti wa watu na ukaona haitoshi umekuja kutudanganya Great Thinkers hapa jukwaani.

Kiufupi unampenda, lakini baada ya kumzalisha ushapata dem mpya na sasa unatafuta mbinu ya kummwaga mzazi mwenzio.

Mtoto kosa lake ni nyie wazazi kuamua kutumia njia za mkato kumpata au nini?

Nipe kazi ya ushenga tukachukue jiko
Angekuwa hampendi au hana shida ya kuzaa naye angemwambia atoe mimba.....
 
Wewe bado ni mtoto mdogo na haujitambui. Unapenda mambo makubwa kuliko uwezo wako. Baadaye utajutia uamuzi wako kwa kumpoteza mtu sahihi atakayekupa amani katika ndoa. Pole kijana, ila unayo nafasi ya kurejesha. Tafuta msaada wa kiroho.
 
Nikwambie tu ukweli ulifanya jambo la kipumbavu kucheza na hisia zake. If you are not happy just leave,why playing with people's feelings, mm sikushauri ila ujue umefanya makosa
Mkuu nakiri kweli nilifanya makosa, hata mimi nilikuwa na mawazo ya kusema et nitampenda tu kumbe wapi nilikuwa najidanganya..
 
Kwa kuwa umekiri kosa,unachoweza kufanya ni kutubu kwa Mungu kwa nia na kweli na katu kutokuja kurudia tena kosa hilo kwa mtu mwingine. Ukifanya hivyo ni nia kutoka moyoni trust me utajiona mwepesi sana moyoni na hata nafsini, kisha mtafute huyo mwanamke mueleze ukwel kuwa hujisikii na wala hauko tayar kuwa naye japo usimwambie kwa namna itakayomfanya ajione mkosaji au ana mapungufu kwasababu ukwel unaujua ww. Lakn pia uwe tayar kumhudumia mtoto kwa hali zote kadri ya uwezo wako na kumuwezesha kimaisha mama wa mtoto pale atakapokwama. Unatakiwa ukabiliane na hili swala kisaikolojia sana hivyo silent treatment za kukaa kimya,kuzira,kukasirika,kununa hazitasaidia ila ukitumia utuuzima basi naamini kila kitu kitakuwa sana na atakuelewa.
Always remember this,hurting someone is like throwing a stone into the ocean, just simple as that,but you have no idea how deep that stone can go. Live peacefully with people and never cause harm to a living soul.
 
Maisha ya ndoa au niseme kuishi na mtu inahitaji zaidi ya upendo. Upendo ni jambo moja, tena kubwa lakini kuna mengi yanaambatana na huko kupendana.
Kama yapi..Hebu nijuze.
 
Sasa umemuacha aondoke na binti yako?! Ujinga wa kutotumia condom wakati unajua huna malengo wala mapenzi kwa wanawake zenu ...unapelekea watoto wengi kulelewa na mama/baba wa kambo(hii ni mbaya).
Na hapo umejifikiria wewe umesahau kuna mtoto ako.
Ni kweli mkuu. Jamaa hapo ana hatia tayari. Swala la kuzaa linahitaji umakini mkubwa imagine msichana wa watu amempotezea muda unadhani hili kovu litapita kirahisi? Hapana.
 
Back
Top Bottom