Ushauri: Roho inaniuma, nimezaa na mwanamke nisiyempenda. Bado anataka kuishi na mimi

Umemdanganya binti wa watu na ukaona haitoshi umekuja kutudanganya Great Thinkers hapa jukwaani.

Kiufupi unampenda, lakini baada ya kumzalisha ushapata demu mpya na sasa unatafuta mbinu ya kummwaga mzazi mwenzio.

Mtoto kosa lake ni nyie wazazi kuamua kutumia njia za mkato kumpata au nini?

Nipe kazi ya ushenga tukachukue jiko
 

Mkuu acha ujinga....nasema tena acha ujinga....yaani umzalishe mtoto wa watu then unataka kumuacha kirahisi hivyo then unatafuta ambaye hajazaaaaa....

Hapo unafanya makosa, sikia jipe muda endelea kumchunguza unaweza kuta huyo ni bora kuliko huyo wa advance atakayeenda chuo akakutane na wajuba baadaye aje akuumize kichwa.......
h
 
Nikwambie tu ukweli ulifanya jambo la kipumbavu kucheza na hisia zake. If you are not happy just leave,why playing with people's feelings, mm sikushauri ila ujue umefanya makosa
 
Angekuwa hampendi au hana shida ya kuzaa naye angemwambia atoe mimba.....
 
Usimwache mwanamke anayeonyesha kwa dhati kuwa anakupenda. Utakuja kukutana na kimeo utakumbuka huo upendo hakyanani!
 
Wewe bado ni mtoto mdogo na haujitambui. Unapenda mambo makubwa kuliko uwezo wako. Baadaye utajutia uamuzi wako kwa kumpoteza mtu sahihi atakayekupa amani katika ndoa. Pole kijana, ila unayo nafasi ya kurejesha. Tafuta msaada wa kiroho.
 
Nikwambie tu ukweli ulifanya jambo la kipumbavu kucheza na hisia zake. If you are not happy just leave,why playing with people's feelings, mm sikushauri ila ujue umefanya makosa
Mkuu nakiri kweli nilifanya makosa, hata mimi nilikuwa na mawazo ya kusema et nitampenda tu kumbe wapi nilikuwa najidanganya..
 
Mkuu nakiri kweli nilifanya makosa, hata mimi nilikuwa na mawazo ya kusema et nitampenda tu kumbe wapi nilikuwa najidanganya..
Kwa kuwa umekiri kosa,unachoweza kufanya ni kutubu kwa Mungu kwa nia na kweli na katu kutokuja kurudia tena kosa hilo kwa mtu mwingine. Ukifanya hivyo ni nia kutoka moyoni trust me utajiona mwepesi sana moyoni na hata nafsini, kisha mtafute huyo mwanamke mueleze ukwel kuwa hujisikii na wala hauko tayar kuwa naye japo usimwambie kwa namna itakayomfanya ajione mkosaji au ana mapungufu kwasababu ukwel unaujua ww. Lakn pia uwe tayar kumhudumia mtoto kwa hali zote kadri ya uwezo wako na kumuwezesha kimaisha mama wa mtoto pale atakapokwama. Unatakiwa ukabiliane na hili swala kisaikolojia sana hivyo silent treatment za kukaa kimya,kuzira,kukasirika,kununa hazitasaidia ila ukitumia utuuzima basi naamini kila kitu kitakuwa sana na atakuelewa.
Always remember this,hurting someone is like throwing a stone into the ocean, just simple as that,but you have no idea how deep that stone can go. Live peacefully with people and never cause harm to a living soul.
 
Maisha ya ndoa au niseme kuishi na mtu inahitaji zaidi ya upendo. Upendo ni jambo moja, tena kubwa lakini kuna mengi yanaambatana na huko kupendana.
Kama yapi..Hebu nijuze.
 
Sasa umemuacha aondoke na binti yako?! Ujinga wa kutotumia condom wakati unajua huna malengo wala mapenzi kwa wanawake zenu ...unapelekea watoto wengi kulelewa na mama/baba wa kambo(hii ni mbaya).
Na hapo umejifikiria wewe umesahau kuna mtoto ako.
Ni kweli mkuu. Jamaa hapo ana hatia tayari. Swala la kuzaa linahitaji umakini mkubwa imagine msichana wa watu amempotezea muda unadhani hili kovu litapita kirahisi? Hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…