Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Para ya ngapi hii? / kipengere namba ngapi hiki ?
1 2 3 .................
Ni hoja nzuri sana
Wangeweza kutumia kigezo walichotumia kumpata speaker mwanamke kama haja ni kuongeza uwakilishi. Yaani kuna kuwa na maazimio kabisa kuwa jimbo fulani msimu huu lisimamishe wagombea wanawake tu kwa vyama vyote na kuwa na circulation kila baada ya miaka mitano. Vinginevyo kama wanataka kuku democrasia basi wote bila kujali jinsia wala rangi wakapigane majimboni. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi sasa wabunge wa viti maalum na kuteuliwa ni wawakilishi wa kina nani?. Yaani bunge linaonekana sasa ni sehemu ya kugawana ulaji zaidi badalaa ya kutumikia wananchi. Gharama za serikali zimekuwa kubwa zaidi ya matokeo ya kuwa na msululu wa watu wanaosubiri posho tu.
Kwa nini tutumie muundo huo hapo juu? Wanawake wangapi wamemaliza vyuo na wanaujuzi wa kutosha kushindana na wanaume. Sidhani kabisa kwamba swala ni elimu au nini. Nadhani swala ni dhana potofu ya kwamba wanawake hawawezi kusimama majimboni. Ukweli ni kwamba Wanawake wa Tanzania ni washupavu ambao wanaweza kuleta mabadiliko wakipewa chance, tuwapeni chance kwa kuwaacha washindane na wanaume. Halima Mdee kashindaje? Spika Kashindaje? Mama Anna Kilango? Mama Tibaijuka? Hawa wote wamewashinda wanaume tena wengine wenye majina ya juu kabisa. Nadhani ni muda muafaka wa kukomesha hii siasa baguzi.