USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Dogo, Batilda aligombea Jimbo na hawezi kuwemo kwenye vit maalum. Labda kama ni lazima sana Prezidaa atamteua kwenye zile nafasi zake 1o. Narudia kama ni lazima sana Batilda awe mbunge. Vinginevyo aje tuchimbe viazi pamoja huku Ludewa
 
Ni upuuzi,fikiria yule mama wa cuf bariadi ktk bunge la 9, kwa miaka 5 alichangia mara moja,cku bunge lilipovunjwa akamfata kikwete amrudishe ccm palepale dodoma upuuziii....!
 
Ni viti maalum vya kukalia wakati wa kula na kupindisha hoja na pia kumchagua chenge kuwa spika. Unadhani da sofi angesimama jimbo gani ili aweze kuchaguliwa?
 
Wanapewa viti maalum waliopigana kusaidia chama hata kama wana udungu na viongozi sio zawadi,isiwe kama cuf walimzawadia mama mmoja wa bariadi ktk bunge lilipita hakuongea kitu kwa miaka 5 then siku ya mwisho akarudi ccm,hiyo hasara ya kuwapa watu wasio na uchungu na chama kisa eti isionekane wametoka sehemu moja ya nchi
 
Mkuu in addition to that, wameangalia pia ujamaa, undugu na uswahiba. Tuliwalaumu CCM kwa hili lakini CHADEMAnao wanakula matapishi yao, Baba, mtoto, mkwe, mzazi mwenza (former wife), n.k. CHADEMA duuh! yaani kwa vinafasi hivi vichache wamejaza ndugu na jamaa jee wakipewa nchi nzima si kila kiongozi atabeba jamaa na ndugu yake. Mwnanchi zinduka CHADEMA chama cha KIFAMILIA!!!!

Very good observation.
.... it is a shame to this party!
 
wako kwenye biashara zao hao.. hawana lolote.. kuna watu kaka ester bulaya.. kadanganya ana elimu ya chuo lakini ni darasa la kumi.... vicky kamata.. jamani.. kila mtu anataka kwenda mjengoni.. naona suruhisho wabunge walipwe mshahara mdogo kuloki waalimu..... sasa watu kama anna abdallah anatafuta nini.. hii ni kuwazibia tu wengine
 
Ushindi, hata wa kura moja, katika urais na ubunge vinakubalika kutokana na sheria iliyotungwa baada ya 1995, kwa kufikiria kuwa umaarufu wa Mkapa ungeshuka kiasi cha kupata kura chini ya asilimia 50%. Sheria hii ilitungwa kwa hofu ya CCM kushindwa kupata kura zaidi ya nusu katika uchaguzi wa mwaka 2000. Hii ilikuwa ni baada ya kufanya tathmini ya nguvu ya Mh. Lyatonga Mrema, na wizi wote wa kura mwaka 1995.

Tusiongolee ubaya wa sheria ya "simple majority". Tuangalie sasa ni kwa vipi viti maalum vinachangia wizi wa kura. Fikiria kama CCM wangeshinda kwa asilimia 50.001%. Moja kwa moja, kwa mujibu wa sheria, Rais angekuwa JK. Lakini sasa, ushindi huu mwembamba ungesababisha CCM ipate "wabunge wa bure" wachache. Kwa maana nyingine, unapoiba kura 1% unaongeza "wabunge wa bure" 1%.

Mchakato wa kampeni na uchaguzi unapokuwa unaendelea kunakuwa na washangiliaji nje wanaosubiri 'mgawo sawa' na wachezaji. Washangiliaji hawa, ndio wanawachochea walio uwanjani kukiuka hata sheria za mchezo, hata kama ni kumnunua refa, ili mradi washinde, ili kundi la washangiliaji lifurahi.

Inasikitisha sana. Viti maalum vingebaki kwa ajili ya makundi maalum, hasa walemavu (wa kike na wa kiume). Sioni sababu ya mtu kama Magreth Sitta kuingia bungeni sawa na Mwalimu Magreth Mkanga, ambaye ni mlemavu. Ni aibu sana; na hakika usawa hautafikiwa kwa njia hii.

Naunga mkono wazo kwamba 'wabunge wa bure' wasizidi mihula miwili, yaani miaka 10.
 
Kujadili undugunazesheni ni hoja muhimu wala si kubomoa,ni changamoto kwa Chadema NA DEMOKRASIA pia ,kwa mfano Mkoa wa SIngida umetoa wabunge wawili je ,wamezingatia jiografia na mgawanyiko wa majimbo!kama wanataka kujenga chama wamengechagua na majimbo ya Iramba ambako CCM imweka kambi!

Tena Mr and Mrs......
2015 first born wao ataingia pia kwenye ubunge ..to make it 3 from one family.

It is a family business, full stop.
 
wako kwenye biashara zao hao.. hawana lolote.. kuna watu kaka ester bulaya.. kadanganya ana elimu ya chuo lakini ni darasa la kumi.... vicky kamata.. jamani.. kila mtu anataka kwenda mjengoni.. naona suruhisho wabunge walipwe mshahara mdogo kuloki waalimu..... sasa watu kama anna abdallah anatafuta nini.. hii ni kuwazibia tu wengine

kuwa zibia wengine kufanya nini? hizi mentality za kuwa bungeni kuna mgao wa riziki za bure ndio kunakowafanya wanawake wasio uwezo kukimbilia huko.

vifutiliwe mbalini tu
 
hapo kwenye red&bold ndipo mafisadi wasipotaka kusikia mtu, ama anaota au anasema laivu

Mkuu hakuna jinsi inabidi sheria itungwe kama si kuondolewa kabisa kwa viti maalumu hawa wanaochaguliwa wasiwe wanarudia mara mbili ili na wengine waweze kuleta changamoto mpya. Atakayenogewa na ubunge atafute jimbo na agombeeeee.
 
naunga mkono hoja kwa kweli hivi viti maalum ni mzigo mzito mno kwa serikali hata kama nikuleta usawa this is too much kwa kweli sidhani kama ina faida yoyote ile hata kwa sisi wanawake sana sana inatufaanya tuzidi kutojiamini na hata kushindwa kuthubutu kwa kujua tu tuna nafasi maalum,nashauri viondolewe tukapambane majimboni vibaki vichache sana kwa ajili ya makundi maalum kama vile wasiojiweza ila akina mama tukapambane majimboni hii ndio itatupelekea sisi kujiamini badala ya kukaa kutegemea upendeleo ambao muda mwingine unatucost
 
ndio maana nimeamuak kwenda rwanda kufanya kazi.
huku nyumbani tunazinguana tu.
 
Inawezekana wananchi tulikuwa tumeona ni kawaida ,lakini hebu angalia huyu mdau wa JF alivyokokotoa akapata Tshs 72 Bilion kwa miaka mitano hapo hujaweka shangingi. Ni kwamba tunadhulumiwa watanzania na viongozi wetu wanaotanguliza Uswahiba na Uhawara mbele kuliko matatizo ya wananchi.

Tutalia kilio cha namna gani tusikike au mpaka tutoe machozi ya damu ndo wajue tunaumia?
Ila najua hawa jamaa wameshakuwa sugu na la kufanya ni kupiga kelele ingawa JK huwa ansema kelele hizo ni za mlangoni na wala hazimnyimi usingizi!!!!

Sisi tudai kurudishiwa nchi yetu kama wamarekani . ALL of us Let's aim for Change
 
Wakuu,hivi ukifikiria viti maalum haraka haraka unapata picha gani? Mi huwa nikisikia viti maalum nafikiria sana sana kuwa ni kuwatengenezea wakubwa ulaji,sana sana watoto wa wakubwa. Hatuwezi kwenda mbali na ukweli kwamba kwa vyama vyote,ukiangalia majina ya viti maalum,%kubwa ni watoto wa vigogo japo wana sifa zinazotakiwa. Taifa lifike wakati flani wafute viti maalum,mi nahisi viti vyote havina maana. Kwa nini? Jibu: ukisema walemavu,ina maana mtu asiye na mguu anashindwa kwenda jukwaani kujieleza? Je asiye na mkono?jibu anaweza,mlemavu wa ngozi albino? Jbu:mbona 2010 mmoja wao kapanda jukwaani na kashinda kuwa mbunge? Je asiyeweza kuongea? Sasa vp bungen atachangiaje?kwa kuandika? Sa si sawa na kuandika ujumbe akampa waziri au mkurugenzi yeyote na ujumbe wake utakuwa umefika bila ya kwenda bungeni? Mi nahisi tufike wakati tujenge nchi tuache kufanya usanii. Kumbuka watz wanakosa huduma muhimu,wanafunzi vyuoni wanapewa mkopo 20%, 30% kwa mwaka ambayo ni sawa na 300,000/= wakati hii ni 0.00...% ya mbunge kwa mwezi na si kwa mwaka. Jaman Tz aibu tupu,yani nchi nkikabidhiwa kwa miezi3 tu,mafisad wataishia jela. Hii dhana ya kupeana ubunge ni upuuzi mtupu.
 
Viti "Maalumu" ni kwa ajili ya kulipa fadhila "Maalumu"!

"... UKILA LAZIMA ULIWE, JAPO KIDOGO ..." Jakaya Kikwete
 
Back
Top Bottom