Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nafikiri ifike mahali sasa viti maalum vitengwe tu kwa ajili ya watu maalum kama Walemavu, Wazee na makundi mengine ambayo hayawezi kustahimili kampeni katika majimbo.
Kwa kweli mkuu hivi viti maalumu havina tija kwa watanzania, hizi ni gharama za kupuuzi embu angalia hapa chini mishahara pamoja na marupurupu yao;
12,000,000 x 95 kwa mwezi = 1,140,000,000 kwa mwaka 1,140,000,000 x 12=13,680,000,000 kwa miaka mitano 13,680,000,000 x 5=68,400,000,000/= ukichanganya na kiinua mgogngo itakuwa 40,000,000 x 95 =3,800,000,000+68,400,000,000= 72,200,000,000/=
Kwa hiyo taifa linapoteza bilioni 72 kwa wabunge wa viti maalumu
My take: serikali inatakiwa ituambie ni kazi gani hawa watu wanafanya ambayo inaweza kuzalisha zaidi ya Bilioni 72 kwa miaka mitano ili waweze kupata mishara yao na taifa lipate faida pia.
Hivi Kenya na Katiba yao ya zamani na mpya walikuwa na viti maalum? Wanawake wa Kenya wanaeleweka duniani kwa kazi zao jasiri na sio kwenda bungeni kulala na kufitiana
Mfano Mzuri Prof. Waangari
Mungu wanguuuuuuuuuuuuuuu........................ Hivi hii hesabu shangingi limo humooooooooooooo................. Mshahara wa dereva......... Mafuta ya shangingi................... YAAANIIIIII HIVI VITI VIFUTWE..............Kwa kweli mkuu hivi viti maalumu havina tija kwa watanzania, hizi ni gharama za kupuuzi embu angalia hapa chini mishahara pamoja na marupurupu yao;
12,000,000 x 95 kwa mwezi = 1,140,000,000 kwa mwaka 1,140,000,000 x 12=13,680,000,000 kwa miaka mitano 13,680,000,000 x 5=68,400,000,000/= ukichanganya na kiinua mgogngo itakuwa 40,000,000 x 95 =3,800,000,000+68,400,000,000= 72,200,000,000/=
Kwa hiyo taifa linapoteza bilioni 72 kwa wabunge wa viti maalumu
My take: serikali inatakiwa ituambie ni kazi gani hawa watu wanafanya ambayo inaweza kuzalisha zaidi ya Bilioni 72 kwa miaka mitano ili waweze kupata mishara yao na taifa lipate faida pia.
Naunga mkono hoja. Tena kama Anna yuko bungeni tangu awamu ya kwanza, ameshajenga uzoefu mpaka akapata uzeefu baado anazuia watu wengine kuleta mawazo mapya bungeni. kuna haja ya kutunga sheria kuwa mtu anapendelewa kipindi kimoja, vingine aingie Jimboni kama alivyo fanya Halima Mdee.
Nafikiri ifike mahali sasa viti maalum vitengwe tu kwa ajili ya watu maalum kama Walemavu, Wazee na makundi mengine ambayo hayawezi kustahimili kampeni katika majimbo.
Tunashangaa kuona watu wenye afya zao na uwezo mkubwa wa kuingia kwenye kinyanganiro cha majimboni kama akina Sofia Simba, Rita Mlaki, Anna Abdalah na wengine hawana aibu wanakaa na kusubiri viti maalum. Hivi wana matatizo gani hawa mpaka wapewe umaalum. Cha ajabu hawa ndio wanao fight kuwepo usawa wa jinsia kuwa wanaume na wanawake lazima wawe katika level. Nilitegemea hawa akina mama ambao ni very vocal kuwa wakwanza kujitosa majimboni ili wagombee kudhihirisha usawa wanaosema. Lakini cha ajabu inapowadia wakati wa ku-fight hawa wanarudi kinyume nyume kuja kuvizia viti vya kupewa bure.
Viti maalum( isipokuwa walemavu na makundi maalum) vinakera sana kwani mimi binafsi sioni kama vina maslahi kwa watanzania bali vinaliongezea taifa mzigo wa gharama za uendeshaji.
Wengi wao wanarudi bungeni mara ya pili kupumzika kwani wanajiwakilisha wenyewe na performance yao huwezi kuipima kwa sababu hawana goals za kufanikisha.
Hivi kwa mfano tukiwauliza wale waliomaliza muda wao last time watuambie tu kwa kipindi chao wamewapatia watanzania mafanikio gani.
Inabidi serikali ifanye vitu objectively na siyo tu kwa mazoea. Viti maalum 95 wote wanalipwa na kodi za wananchi for what wakati Madaktari na wataalam wengine wanakimbia nchi kutokana na mishahara duni. hela ya kuwalipa hawa ingetosha kabisa kuwalipa hawa madaktari wakamsaidia mtanzania kupata afya akaweza kuzalisha na kuinui uchumi.
Hawa viti maalum wana mchango gani katika kuinua uchumi wa mtanzania. Inabidi tufike mahali tupime mafanikio kwa kutumia indicator zinazoeleweka kuliko kutumia tu maneno ya kisiasa.
Tunahitaji kuijenga Tanzania kwa kuinua uchumi wa wananchi wa vijijini walio maskini na siyo kwa kuwapa wabunge wengi wa viti maalum wanaopunguza bajeti ambayo ingeweza kuwafikia hata kupata ruzuku za pembejeo au kupunguza gharama za afya n.k
Unajua wanawake wenyewe kwa wenyewe hawapendani!
Maana % kubwa ya wapiga kura ni akina mama! sasa wenyewe huwa huchagua wanaume ktk majimbo...halafu eti kukaa kusubiria usawa wa viti vya upendeleo! Yaani viti 95!!
Yaani Haiingii akilini!
Mama lao mko hapo?