USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Dr atafanuya kazi za chama, ubunge sio lazima kwake
 
LISTI KAMILI ZA WABUNGE WA CHADEMA:
1. Lucy Owenya - Kilimanjaro
2. Esther Matiko - Mara
3. Mhonga Luhanywa - Kigoma
4. Anna Mallac - Katavi
5. Paulina Gekul - Manyara
6. Konchesta Rwalumulaza - Kagera
7. Suzan Kiwanga - Morogoro
8.Grace Kiwelu - Kilimanjaro
9. Suzan Lyimo - Kilimanjaro
10. Regia Mtema - Morogoro
11. Christowaja Mtinda - Singida
12. Anna Komu - Dar Es Salaam
13. Mwanamrisho Abama - Zanzibar
14. Joyce Mukya - Arusha
15. Leticia Nyerere - Mwanza
16. Naomi Kaihula - Dar Es Salaam
17. Chiku Abwao - Iringa
18. Rose Kamili - Manyara
19. Christina Lissu - Singida
20. Raya Ibrahim - Zanzibar
21. Philipa Mturano - Dar Es Salaam
22. Mariam Msabaha - Zanzibar
23. Rachel Mashishanga - Dar Es Salaam

CHADEMA wameangalia zaidi elimu na uzoefu, na kwa idadi hii hakuna kitakachoizuia hiki chama kuwa chama kikuu cha upinzani, na zito au mbowe kuwa kiongozi wa upinzani bungeni kutokana na idadi kubwa kuliko chama chochote cha upinzani. CHADEMA 45, CUF 34, NCCR 4, TLP 1, UDP 1.
Hata CUF wakitaka kuungana na NCCR pamoja na TLP na UDP hawataweza kufikisha idadi ya CHADEMA.
 
Kama Mungu asingekuwa upande wa CHADEMA hawa wasingepatikana! Basi Bwana akiwa upande wa CHADEMA ni nani aliye juu yao? HAKUNA
 
Mungi,
Hivi ni kweli au nimechanganya majina? Rose Kamili... si yule diwani wa zamani wa CCM kule karatu aliyekuwa mke/mchumba wa weapon?
 
Batilda Burian alikuwa ni mgombea wa kiti cha Ubunge Arusha mjini kwa tiketi ya CCM.
Kwanini uhoji kuwa hajakuwemo kwenye list ya Wabunge wa kuteuliwa?
Huwezi kuwa candidate kwenye nafasi 2 at a time.

Nafikiri wewe hufuatilii taarifa zaidi, kucontest nafasi mbili inawezekana, ila kutokana na ratiba ya ccm wao waliiweka wazi mapema hata kabla ya kampeni kuanza.

Angalia list ya CHADEMA, Rose Kamili alikuwa anagombea jimbo la Hanang, lakini sasa ameteuliwa viti maalum, Regia Mtema alikuwa anagombea jimbo la Kilombero, naye ameteuliwa viti maalum.

Jambo ambalo CHADEMA wamefanya ni kutokuweka majina ya viti maalum hadharani. Mfano hata Halima Mdee asingeshinda jimbo angekuwepo na yeye viti maalum.
 
ENGINEER?!!!!!!!!!!!!!! USIWE NA NEGATIVE ATTITUDE........HAWA WAWILI ULIO HIGHLIGHT WANAUHUSIANO FULANI NA BAADHI YA VIONGOZI WA CHADEMA...LAKINI KWA TAARIFA YAKO WALIPELEKA MAOMBI YAO KAMA WENGINE NA WANAVIGEZO KAMILIFU..SI UPENDELEO WALA NINI?!! MBONA HATA VYAMA VINGINE KUNA WATU WANA MAHUSIANO NA WAGOMBEA WA UBUNGE,URAIS,MAWAZIRI LAKINI WANANAFASI VITI MAALUMU.....Wakati mungine wadau tujenge hoja ni si kujenga hisia hisia tu!
 
Hivi ni kweli au nimechanganya majina? Rose Kamili... si yule diwani wa zamani wa ccm kule karatu aliyekuwa mke/mchumba wa weapon?

Ni kweli Rose Kamili alikuwa Diwani wa Kata ya Basotu kwa tiketi ya CCM, lakini ndiyo hivyo kahamia chadema kuwa Mbunge, na Christina Lissu ni Ubavu wa mpiganaji Lissu.
 
Mungi,
Mkuu in addition to that, wameangalia pia ujamaa, undugu na uswahiba. Tuliwalaumu CCM kwa hili lakini CHADEMAnao wanakula matapishi yao, Baba, mtoto, mkwe, mzazi mwenza (former wife), n.k. CHADEMA duuh! yaani kwa vinafasi hivi vichache wamejaza ndugu na jamaa jee wakipewa nchi nzima si kila kiongozi atabeba jamaa na ndugu yake. Mwnanchi zinduka CHADEMA chama cha KIFAMILIA!!!!
 
Ni kweli Rose Kamili alikuwa Diwani wa Kata ya Basotu kwa tiketi ya CCM, lakini ndiyo hivyo kahamia chadema kuwa Mbunge, na Christina Lissu ni Ubavu wa mpiganaji Lissu.

Asante Mungi kumbe mchumba finally alirudi kundini, sikuwa na taarifa. sahihisho dogo christina ni dada wa Mpiganaji Tundu na si ubavu, google utapata habari hii
 
Kwanini Musiweke na wa CCM kama wapo nao tukawajua ama waliochaguliwa ni wa CHADEMA tu?
 
Hongera sana mwenyekiti wangu Rachel Mashishanga, wewe ni mpiganaji wa kweli na Jiwe la Pembeni lisiloweza kuachwa na Waashi. Ulimshinda Mpendazoe kwenye kura za maoni jimboni kwetu lakini ukamwachia ili apambane na ukamsaidia atwae jimbo kama si kuchakachuliwa, hivi sasa tungekuwa tunaongozwa na mbunge wa CHADEMA.

Nenda Rachel nenda, nenda mjengoni ukatuwakilishe vizuri. Nakuomba usituache wanaJF ili tuendee kulijenga taifa kwa pamoja!
 
Mkuu in addition to that, wameangalia pia ujamaa, undugu na uswahiba. Tuliwalaumu CCM kwa hili lakini CHADEMAnao wanakula matapishi yao, Baba, mtoto, mkwe, mzazi mwenza (former wife), n.k. CHADEMA duuh! yaani kwa vinafasi hivi vichache wamejaza ndugu na jamaa jee wakipewa nchi nzima si kila kiongozi atabeba jamaa na ndugu yake. Mwnanchi zinduka CHADEMA chama cha KIFAMILIA!!!!

Ndugu yangu hiki si kipindi cha kujadili nani ni ndugu wa nani, tuangalie watatuteteaje hawa walioteuliwa. Kutokana na mwamko mdogo wa watanzania kwenye upinzani, wao ndiyo wamepata nafasi hizo, isitoshe kidogo elimu nayo imewasaidia. Sidhani kama wamefanya kama unavyofikiri wewe.

Kwa wale ambao majina yao yaliondolewa mwanzoni, ilitokana na elimu yao ndogo pamoja na kutokuwa na uzoefu ndg yangu.

Kwa sasa wasomi wengi wanawake bado hawajajitokeza kugombea CHADEMA kama ilivyo chama tawala.
 
Kwanini Musiweke na wa CCM kama wapo nao tukawajua ama waliochaguliwa ni wa CHADEMA tu?

Hatuna shida nao, kama unataka kujua wa CCM kanunue gazeti la UHURU utawakuta huko.
 
Batilda Burian alikuwa ni mgombea wa kiti cha Ubunge Arusha mjini kwa tiketi ya CCM.
Kwanini uhoji kuwa hajakuwemo kwenye list ya Wabunge wa kuteuliwa?
Huwezi kuwa candidate kwenye nafasi 2 at a time.

Sure? I was not aware of this "RULE" - yes for sure!
 
Kujadili undugunazesheni ni hoja muhimu wala si kubomoa,ni changamoto kwa Chadema NA DEMOKRASIA pia ,kwa mfano Mkoa wa SIngida umetoa wabunge wawili je ,wamezingatia jiografia na mgawanyiko wa majimbo!kama wanataka kujenga chama wamengechagua na majimbo ya Iramba ambako CCM imweka kambi!
 
Hayo Majimbo uliyosema una uhakika walituma maombi yao? Usiwe unakurupuka wakati hakuna hata mtu aliyetuma maombi. Ninachosema ni kwamba mwamko ni mdogo kwa baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na singida. Mikoa ambayo mwamko ni mkubwa ni pamoja na Kilimanjaro, Arusha, Dar es salaam, nk. katika mikoa hiyo wanawake wengi waliomba nafasi, ilibidi vigezo viwe vitu vya msingi bila kuangalia huyo mtu ni nani na anauhusiano na nani. Mfano Nakaaya aligombea kupitia Arusha lakini kagonga mwamba kutokana na elimu yake.
 
Batilda Burian alikuwa ni mgombea wa kiti cha Ubunge Arusha mjini kwa tiketi ya CCM.
Kwanini uhoji kuwa hajakuwemo kwenye list ya Wabunge wa kuteuliwa?
Huwezi kuwa candidate kwenye nafasi 2 at a time.

Wewe ni mgonjwa, nafasi 2 at a time, Regia Mtema, Komu, Halima Mdee, nk. walikwenda majimboni na huku wamo viti maalumu. bisha ukimaanisha kubisha.
 
Mkuu in addition to that, wameangalia pia ujamaa, undugu na uswahiba. Tuliwalaumu CCM kwa hili lakini CHADEMAnao wanakula matapishi yao, Baba, mtoto, mkwe, mzazi mwenza (former wife), n.k. CHADEMA duuh! yaani kwa vinafasi hivi vichache wamejaza ndugu na jamaa jee wakipewa nchi nzima si kila kiongozi atabeba jamaa na ndugu yake. Mwnanchi zinduka CHADEMA chama cha KIFAMILIA!!!!

KWANZA UMEJIUNGA LAST MONTH ILA ULITAKIWA UWE NA POST HATA 20 NA MENGINEYO,LAKINI WEWE NI WA MSIMU HUJUI UNACHOANDIKA WAVAMIA TU POST.. HIVYO KAA MBALI NA SISI USITUAMBUKIZE UPUMBAVU... JAPO SINA MDA MREFU KWENYE JF LAKINI UMEANDIKA UJINGA..
CAH MUIMU KUFANYA KAZI NA SIO KUANGALIA KWAMBA NI UKABILA, UDINI,UFAMILIA , WEWE NI WA WAPI??
NAZANI HUMKUMBUKI NYERERE MANA ALIPINGA SANA AYO MANENO YAKO YA SHOMBO NA YA UPUMBAVU
shkh Yahya

Junior Member

Join Date:
Fri Oct 2010
Posts:
4
Thanks:
0
Thanked 0 Times in 0 Posts
 
Nafikiri ifike mahali sasa viti maalum vitengwe tu kwa ajili ya watu maalum kama Walemavu, Wazee na makundi mengine ambayo hayawezi kustahimili kampeni katika majimbo.

Tunashangaa kuona watu wenye afya zao na uwezo mkubwa wa kuingia kwenye kinyanganiro cha majimboni kama akina Sofia Simba, Rita Mlaki, Anna Abdalah na wengine hawana aibu wanakaa na kusubiri viti maalum. Hivi wana matatizo gani hawa mpaka wapewe umaalum. Cha ajabu hawa ndio wanao fight kuwepo usawa wa jinsia kuwa wanaume na wanawake lazima wawe katika level. Nilitegemea hawa akina mama ambao ni very vocal kuwa wakwanza kujitosa majimboni ili wagombee kudhihirisha usawa wanaosema. Lakini cha ajabu inapowadia wakati wa ku-fight hawa wanarudi kinyume nyume kuja kuvizia viti vya kupewa bure.

Viti maalum( isipokuwa walemavu na makundi maalum) vinakera sana kwani mimi binafsi sioni kama vina maslahi kwa watanzania bali vinaliongezea taifa mzigo wa gharama za uendeshaji.

Wengi wao wanarudi bungeni mara ya pili kupumzika kwani wanajiwakilisha wenyewe na performance yao huwezi kuipima kwa sababu hawana goals za kufanikisha.

Hivi kwa mfano tukiwauliza wale waliomaliza muda wao last time watuambie tu kwa kipindi chao wamewapatia watanzania mafanikio gani.

Inabidi serikali ifanye vitu objectively na siyo tu kwa mazoea. Viti maalum 95 wote wanalipwa na kodi za wananchi for what wakati Madaktari na wataalam wengine wanakimbia nchi kutokana na mishahara duni. hela ya kuwalipa hawa ingetosha kabisa kuwalipa hawa madaktari wakamsaidia mtanzania kupata afya akaweza kuzalisha na kuinui uchumi.

Hawa viti maalum wana mchango gani katika kuinua uchumi wa mtanzania. Inabidi tufike mahali tupime mafanikio kwa kutumia indicator zinazoeleweka kuliko kutumia tu maneno ya kisiasa.

Tunahitaji kuijenga Tanzania kwa kuinua uchumi wa wananchi wa vijijini walio maskini na siyo kwa kuwapa wabunge wengi wa viti maalum wanaopunguza bajeti ambayo ingeweza kuwafikia hata kupata ruzuku za pembejeo au kupunguza gharama za afya n.k
 
Back
Top Bottom