USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!


Nashukuru mkuu kwa mawazo, kwenye hiyo katiba mpya ungependa hili jambo lisomeke vipi mkuu ili kufanikisha ushauri wako?
 
wabunge wa viti maalum ni ubadhirifu wa hela tu. Waliochaguliwa na wananchi wanatosha. Ni kuliongezea taifa mzigo wa matumizi yasiyo na maana

Lakini mkuu kuna idadi kubwa ya waliochaguliwa na wananchi ambao ufanisi wao bungeni ni finyu kuliko wabunge wa viti maalumu. Kwenye hoja yangu ya msingi nimeomba tuchangie mawazo ni namna gani ya kuwajibisha wabunge waliochaguliwa ambao hawana tija wala ufanisi. Wengi wakishachaguliwa basi, wanajua hata kama wakiboronga namna gani ni mpaka uchaguzi ujao. Na sisi wote tunajua uchaguzi ni kanga na t-shirt ndiyo maana tunao wabunge waliochaguliwa kwa kishindo siyo kwa uwezo wao kiuongozi bali uwezo wao kifedha

hebu tusaidie mawazo mkuu
 

Tatizo ni kwamba wabunge wengi wa viti maalum ni vigogo na hivyo hawajui matatizo ya wanawake watz. Pengine tatizo ni mchakato wa kuwapata hawa wabunge wa viti maalum. Lakini tunahitaji wengi hivyo kweli kutetea mambo ya wanawake? Mbona yule mbunge mwanamke mlemavu wa ngozi ametetea sana albino bungeni na yuko peke yake? mbona yule mama mlemavu, alitetea sana mambo ya walemavu bungeni na sheria nyingi sasa zina mtazamo chanya kwa walemavu, na yuko peke yake?
 

Njia moja muhimu na ya kwanza ni kuondoa incentive ya pesa katika cheo cha ubunge maana ubunge si profession ni siasa, mbona madiwani hawapewi package kama ya wabunge na bado wanachapa kazi? Ku attach cash value kwenye cheo cha ubunge kimefanya ubunge uingiliwe na watu ambao kimsingi si wanasiasa bali ni sehemu ya kuondoa poverty kwa haraka kwani inalipa kuwa mbunge kuliko kuwa professional; pia rushwa ni sababu ya pili ya wafanya biashara kukimbilia wote bungeni kwani cost ya kufanya biashara na ku break even ni kubwa kwa mfanya biashara ambaye si mwanasiasa na speicifically mbunge.....maana biashara kubwa Tanzania ni Tender za serikali na zinapatikana kwa urahisi ukiwa mbunge kuliko mfanya biashara wa kawaida as one factor lakini pia kusumbuliwa na TRA plus system in general kunapungua ukiwa katika domain hiyo ya siasa kuliko vingine....One important factor ya ku punguza ni kuangalia leagal enforcement ambayo ndiyo italeta equity katika production function ya uchumi wa nchi

In general muundo wetu mzima unaathiriwa na UFISADI; Poverty and poor governance kama means ya ku combat the two.
 
According to ccm wanataka wananchi waamini hii formula:
C = M + U + D + C + H + L
Details:
C = Bunge la Tanzania
U = uganga wa kienyeji
C = Deals za mafisadi
H = Hongo ya ccm
L = Lazima uhakikishe unatumia hii pesa kuchaguliwa tena kumlinda Rostam
 
Wana JF

Ndio kuna wabunge wachache wa viti maalumu waliofanya mambo makubwa ya kuwatetea wanawake. Ninasema wachache, lakini wengi wamekuwa mzigo mkubwa kwa sisi walipa kodi. Wabunge hao wa viti maalumu hata ukisikia michango yao bungeni kusema kweli hata kujenga hoja hawawezi kabisa. Hivyo basi hao wengi ambao ni unproductive wanawameza wachache ambao ni productive hivyo kama ni ku strick the balance wabunge wa viti maalumu ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi coz wengi wanawajibika kwa chama na wananchi hatuna njia ya kuwa wajibisha.

Katika katiba mpya tutakayojiwekea sipendi kabisa vyeo vifuatavyo viwemo
  1. Wambunge wa viti maalumu
  2. Wabunge wa kuteuliwa na Rais
  3. Wakuu wa mikoa
  4. Wakuu wa wilaya
  5. Waziri mkuu (kwasababu tunafuata president system. (Rais na VP wanatosha)
  6. Wabunge kuwa Mawaziri
  7. Mameya/Wenyeviti wa halmashauri kuchaguliwa na madiwani (Tufanye direct election)
  8. Muundo wa Wizara za serikali uainishwe kabisa kwenye katiba (sio rais kujiundia wizara zake)
Samahani ninaanza kutoka kwenye maada wabunge wa viti maalumu plus wa kuteuliwa is a wastage of resources. Jamani nchi yetu hii bado ni masikini hatuna hizo resources za kuwakirimu hawa wa viti maalumu na kuteuliwa
 
what's the point?
 
Wakuu
nimejaribu kufuatulia kwa karibu sana juu ya umuhomu wa viti maalumu mbele ya matumizi yake yapasayo kwa watanzania.
nilichokuja kugundua ni kwamba hivi viti ni mzigo mkubwa kwa Taifa kwani wanawake hawa wanalipwa mabilion ya pesa kila mwezi bila kuzalisha kitu chochote.
mfano kwa sasa kila mmoja amepewa milioni 90 kwa ajili ya kununa gari la kifahari, wabunge hawa wapo zaidi ya 100 hivyo kufanya hela pekee waliyochota wao ni zaidi ya bilion 9 ambazo wanafunzi wa vyuo vikuu wanazidai wapatiwe BOOM la kumi elfu kila siku...
najua wanaonufahika na hivi viti hawatanielewa lakini huo ndio ukweli na sitajali ni mchungu au mtamu kiasi gani.

BAADA YA DOWANS JANGA LINGINE LA TAIFA NI VITI MAALUM
 
Tulishajadili hili swala hapa JF,search hiyo thread alianzisha Msando Alberto.....nakubaliana na wewe viti maalum ni mzigo kwa taifa ila vina umuhimu wake katika harakati za kumuinua mwanamke na kumfanya ashiriki katika maamuzi...tatizo lipo kwenye idadi na namna wanavyopatikana hao wabunge.....swali langu ni je hao wabunge wasio wa viti maalum wanafanya lipi la maana sana??? tuchukue mfano wa Halima Mdee akiwa bado viti maalum na Idd Azan akiwa mbunge wa kuchaguliwa wa Kinondoni??

Kuna haja ya kupunguza idadi na kurekebisha namna wanavyopatikana kikatiba,ila kwenye suala la kuzalisha chochote hata hao waliochaguliwa wengi ni useless tu.soma maoni yetu zaidi kwa hiyo thread ukiipata.....
 

Maoni yangu viti maalumu viwepo tu ngazi ya madiwani tuu na halmashauri ziimarisha zifanye kazi zake kwa ufanisi kama yalivyo majimbo ya Marekani
 
Maoni yangu viti maalumu viwepo tu ngazi ya madiwani tuu na halmashauri ziimarisha zifanye kazi zake kwa ufanisi kama yalivyo majimbo ya Marekani

kwanini viwepo ngazi ya udiwani na halmashauri na si bunge na executive?? is it because ni wanawake walio kwa viti maalum?give us your reasons.....:A S 13:
 
Swala cio viti maalum tatizo ni ufanisi wa mbunge yoyote mi naona idadi ya wabunge ipungue 360 too much,chukulia wengine wapo kwa ajiri ya kuzomea wenzao kama majuha na wengine kazi kusinzia kama yule ko....ba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…