USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Ndio maana wanadai katiba Mpya. Hujawasikia wakipinga Wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri bila bunge kupitisha, Uchaguzi wa majaji wakuu upitishwe bungeni, Kuondolewa nafasi za Ma RC, Ma DC, Kiti cha rais na Waziri mkuu kimoja wapo kiondolewe..Mgombea Urais wa chama cha siasa kushiriki pia ktk kugombea Ubunge jimboni au kupewa kiti maalum bungeni na mengine mengi tu..

Hata hivyo wakikataa wao mtawaita wajinga kama wanavyoitwa leo kutoka Bungeni. Kama wangekaa bungeni na kupinga wakati mchezo unaendelea wasingeweza kuwashinda wabunge 300 wa CCM.. Hilo wananchi na wapenzi wa CCM hawalioni..Kifupi ni kwamba wabunge wote bungeni ni wawakilishi wa vyama kiutendaji na sio wananchi hata kidogo.. huu ndio mfumo tunaoupiga vita wananchi.
 
hawana umuhimu wowote naona wanakula bure bila ya sababu yoyote..
 
Hayo ni maswala ya chama CCM lipeleke huko nalo litajadiliwa na mahusika.. hapa tunazungumzia mustakabali wa nchi yetu na sio CCM...
 
tofautisha kati ya mambo ya chama na yale ya kitaifa
 
Ni maswala gani ya Kitaifa unayokwenda bungeni kama mwakilishi wake? - Je Bungeni ni sehemu ya Ajira?
 
Na wakatae wahesabiwe. Kama tayari wanaitwa wajinga, kuongelea msimamo wao haitabadili kitu kwenye hilo. Wasipoliongelea tunashindwa kuwatofautisha na CCM. Tunaomba msimamo wao uwe wazi kwenye hili.
 
Hayo ni maswala ya chama CCM lipeleke huko nalo litajadiliwa na mahusika.. hapa tunazungumzia mustakabali wa nchi yetu na sio CCM...

Ukiangalia kwa Undani NEC ya CCM ni sawasawa na Bunge la Tanzania... na Ujue CCM ilifanya NEC kuwa na NGUVU zaidi ya BUNGE

Kwa CCM kurekebisha ulaji wao ni lazima waanzie NEC then BUNGENi sababu nia ilikuwa kuwaweka wateule kuchunguza Wabunge halafu kupeleka mapendekezo yao NEC; Angalia Anna Abdalla haendi bungeni ni Mbunge wa kuteuliwa ni yeye aliyependekeza Mbunge kuwa Mwanamke Anna Makinda na kila Mbunge wa CCM alipiga kura ya Ndio... Sasa Uchawi Upo wapi???

UCHAWI UPO NEC then BUNGENI...
 
Waafrika ndivyo tulivyo!!

Bado hujajibu swali langu? Viti maalumu wanawakilisha kina nani? Mfano, Regia Mtema, Kilombero kuna mbunge pale; sasa yeye anawakilisha kina nani? Utasema wanawake; je, hao wanawake hawakumpigia kura mbunge aliyeshinda?
 
Hivi unajua kuwa sasa hivi wapiga kura tanzania wengi ni wanawake? Sasa wameshindwa nini kuwapigia kura wanawake wenzao? Na akina Makinda na Mdee wanashinda kwa kura za akina nani? Hoja yako dhaifu ndugu.
Inawezekana hoja yangu ni dhaifu kwa mtazamo wako, to me is very strong u know. Kwani unafikiri mfumo dume upo kwa wanaume tu? Ukweli utabaki kuwa ukweli tuna mfumo dume.
 
Ni maswala gani ya Kitaifa unayokwenda bungeni kama mwakilishi wake? - Je Bungeni ni sehemu ya Ajira?

Hiyo miswada inayopitishwa ni majimbo sio? hivi huji kuwa bunge ni sehemu ya ajira? duuu au unafikiri ni utetezi wa majimbo? au wito? lahaula watu wasingetoana roho ati.
 
Na wakatae wahesabiwe. Kama tayari wanaitwa wajinga, kuongelea msimamo wao haitabadili kitu kwenye hilo. Wasipoliongelea tunashindwa kuwatofautisha na CCM. Tunaomba msimamo wao uwe wazi kwenye hili.
Mkuu wangu kuwa na fikra za Utaifa kwanza..Chadema wakae na kuzungumzia kitu gani ikiwa muswada huu ulitakiwa upite kwako kwanza! CCM hawajui kwa nini tunahitaji katika Mpya na wamesema siku zote kwamba katiba iliyopo haina makosa na kama yapo basi yafanyiwe marekebisho. Unategemea JK atachagua tume gani ikiwa yeye mwenyewe haelewi tatizo au kama analielewa hataki kubadilishwa. Katika nchi ilojaa Ufisadi wewe mwananchi unategemea ni majibu gani yatakuja kutoka kundi la watu wanaofikiria Katiba iliyopo haina tatizo?..Kwa nini Chadema wapoteze muda wao kubishana Bungeni ktk vitu ambavyo havilingi akilini. Kwa nini swala la Katiba mpya liwe la CCM/CDM/NCCR na vyama vingine badala ya wananchi?
 
Hiyo miswada inayopitishwa ni majimbo sio? hivi huji kuwa bunge ni sehemu ya ajira? duuu au unafikiri ni utetezi wa majimbo? au wito? lahaula watu wasingetoana roho ati.
Kama ndivyo basi sisi wananchi hatutaki watoane roho tunawapenda sana..viti hivi viondolewe kabla hesabu ya wanawake nchini haijapungua..
 
Waafrika ndivyo tulivyo!!

Bado hujajibu swali langu? Viti maalumu wanawakilisha kina nani? Mfano, Regia Mtema, Kilombero kuna mbunge pale; sasa yeye anawakilisha kina nani? Utasema wanawake; je, hao wanawake hawakumpigia kura mbunge aliyeshinda?

Hivi tatizo lako ni uwakilishi tu? yaani nani wa kumtetea si ndio? siwezi kujieleza wee hapa kwani siwezi kuiondoa mind set yako iliyokwisha pevuka kwa mawazo kuwa wanamwakilisha nani. Hivi hujaona kazi anayoifanya Regia juu ya watu wa Kilombero? Huyo Mteketa kafanya nini hasa? hebu toa hesabu hapa mbele za Mungu mpaka sasa, maswali mangapi kauliza kuwatetea hao wana Kilombero?au hata speech ngapi kachangia bungeni kutetea wana kilombero? Anyway viti maalumu viondolewe kwani imekuwa kero, chuki, wivu na dharau kwa wanawake.
 
Bro mimi huko kwenye katiba mpya sijafika mbona. Nnachozungumzia ni kuwa Chadema haijawahi kupinga hadharani mfumo ulipo wa viti maalum vya wanawake. Siwategemei wao walizungumzie sasa hivi Bungeni suala hili, lakini kama tunavyojua misimamo yao mengine kwenye masuala mbali mbali kwenye taifa hili, nilidhani tungejua msiamamo wao ukoje.

Wanakubaliana na mfumo uliopo wa viti maalum kwa wanawake au la?
 
Kama ndivyo basi sisi wananchi hatutaki watoane roho tunawapenda sana..viti hivi viondolewe kabla hesabu ya wanawake nchini haijapungua..

Ha ha ha @ hesabu ya wanawake nchini haijapungua!

Uskute wanaopigania ni wanaume wanaowawezesha
 
Ni pigo kubwa kwa Regia Mtema na Rose Kamili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…