Mimi si Mwanasiasa, na si mtu wa kupigia debe haya mambo ya siasa za Kiafrika... Lakini kuna mambo ambayo uwa nayaona kama si lazima sana yawepo na haswa kwenye safu ya uongozi wa nchi.
Haya mambo ya kuwa na
Wabunge wa viti maalum ,
Wabunge kuwa Mawaziri,
Wakuu wa mikoa kuchaguliwa n a Rais...
Mikoa kuwa na Meya hapo hapo kuna
Mkuu wa Mkoa... Yote haya ni maswala ambayo yanapaswa kuangaliwa upya.
Kwa sababu mtu akigombea ubunge kisha anachaguliwa tena kuwa Waziri, kunapunguza uwakilishi wake Bungeni. Na kama wabunge kubaki kuwa wabunge kutaondoa tamaa ya Wabunge kujipendekeza kwa serikali ili wachaguliwe kuwa mawaziri....
Kuhusiana na muda au vipindi vingapi kwa maoni yangu mimi as long as wananchi wanakupenda na uwezo wa kuwakilisha na kutatua matatizo ya wananchi unayo basi endelea kugombea... Hii ni kwa ngazi ya ubunge... Na wanapaswa kuwa na ofisi kwenye majimbo yao au hata ofisi ndogo uko vijijini, na iwe lazima mbunge kutembelea jimbo lake na vitongoji mwake kila mwaka, na hakishindwa basi hawajibishwe na atumie pesa au posho anazolipwa uko bungeni (
yaani kusiwe na pesa za ziada kutoka serikalini wala asiombe kwa wananchi, labda wananchi wapende wenyewe kumchangia au chama chake kifanye utaratibu wa kumpatia)
Vilevile kwenye Ukuu wa Mikoa ingependeza zaidi kama hawa wakuu wa mikoa nao wakagombea au kupigiwa kura kama wanavyo pigiwa kura wabunge.... Hii kutawalazimisha kuwajibika kwa raiya zao... Au hao wabunge wa Mkoa au jimbo ndio wanapaswa kugombea nafasi ya Ukuu wa mkoa, hapa ina maanisha kuwa Wabunge wakishirikiana na mkuu wao wa mkoa (ambaye naye ni mbunge) wanakaa katika baraza ambalo wao pamoja na viongozi wachache wa kiraiya, wakiwemo wakuu wa wilaya na raiya waliochaguliwa kuingia kwenye kamati ya kujadiri matatizo ya wananchi, ndio wataamua nini kipelekwe uko bungeni na ikiwezekana miswaada ya bunge inapitia ngazi hii kwanza na kupata maamuzi wa kila mkoa na kisha ndio uko bungeni kunapelekwa mapendekezo au maamuzi ya kimkoa, kwa sababu wananchi washa shirikishwa na uwamuzi ushatolewa.
Kama haiwezekani basi iwepo serikali ya majimbo, ambayo itakuwa na uwajibikaji mkubwa wa majimbo...
Mfano:
Dar Es Salaam, Pwani na Morogoro, linaweza kuwa ni jimbo Moja.
Kagera, Kigoma, na Mara,
Singida, Dodoma na Iringa
Rukwa, Mbeya
Ruvuma, Mtwara na Lindi
Kilimanjaro, Manyara na Tanga
Zanzibar
Pemba
Au ikachaguliwa mikoa yenye kupakana na yenye ukaribu zaidi.
Gonga Hapa:
Dhuluma Haiondoki Bila Kubadili Mfumo