USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Gaijin, Ningesema 'kuwashawishi' au kuweka mazingira yanayofaa na sio 'kuwalazimisha'. Angalau tunakubaliana kuwapo kwa tatizo la kimfumo. Na ukitizama sana mfumo huo umeathiri sana hata namna ya kufikiri na hivyo maamuzi....so ukisema wanawake hawataki au hawapendi kitu fulani....bear in mind athari za mfumo uliopo. Nakubaliana na wewe kwenye suala la kuanzia kwenye elimu lakini kumbuka maamuzi hayo yanatakiwa kufanyika sasa katika mazingira ambayo unasema hatuhitaji viti maalumu au 'uwezeshaji'/upendeleo.
 
Ningesema 'kuwashawishi' au kuweka mazingira yanayofaa na sio 'kuwalazimisha'. Angalau tunakubaliana kuwapo kwa tatizo la kimfumo. Na ukitizama sana mfumo huo umeathiri sana hata namna ya kufikiri na hivyo maamuzi....so ukisema wanawake hawataki au hawapendi kitu fulani....bear in mind athari za mfumo uliopo. Nakubaliana na wewe kwenye suala la kuanzia kwenye elimu lakini kumbuka maamuzi hayo yanatakiwa kufanyika sasa katika mazingira ambayo unasema hatuhitaji viti maalumu au 'uwezeshaji'/upendeleo.

Nikubali kitu kimoja. Labda mimi sio mtu sahihi wa kuzungumzia mfumo dume. Sijawahi kuzuilika kufanya kitu chochote kile nilichotaka kwa sababu ni mwanamke.

Juu ya hivyo nadhani mimi sikubaliani na dhana ya kuwezeshwa. Nadhani ni wakati wa kumpa mwanamke haki yake ya msingi tu kama wanavyopata wanaume na yeye mwenyewe atajiwezesha na sio kumuwezesha.

Anayewezeshwa hawezi kuweza, kwa sababu huwa hajaweza yeye mwenyewe. Mpe haki zake za msingi na umuwache mwenyewe aweze na aamue kile anachotaka kufanya, be it kugombea ubunge au kuwa mama wa nyumbani. Usimuwezeshe kuwa mbunge kwa sababu ina maanisha hajaweza.
 
W. J. Malecela,
Kwa hili tupo pamoja,

Kuna mengi sana ya kuangaliwa kwenye katiba yetu, raisi ni kama dictator madaraka yake ni mengi sana.....teuzi zake basi zipitie bungeni, Tume ya Uchaguzi iwe huru na isteuliwe na raisi. Vyeo vya UDC na RCs vipoteee. Raisi asiwe na Kinga ya kushitakiwa avunjapo katiba basi nchi akabidhiwe Mwanasheria mkuu na uchaguzi mkuu uitishwe. Kuna mengi sana kwa kifupi Tanzania hatujawahi kuwa na Katiba ya watanzania tangia taifa hili liasisiwe. Napinga ujanja ujanja wa wajinga wachache kutaka pora agenda ya katiba watuaandalie, ni vyema watanzania wa kad zote tushiriki kwenye mchakato wa kupata katiba.

Rais kwa katiba yetu ya sasa ni kama Mungu Mtu

Mch
 
Legitimacy ni vidole sio? ameingiaje bungeni bila legitimacy? basi Tanzania haifai, anyway.....
Demokrasia ni pana ni zaidi ya kupiga kura. Unaweza piga kura kumchagua mtu usiyemtaka vilevile, kwako likaonekana ni demokrasia kisa wamepiga kura. tunahitaji elimu ya uraia tz, walahi tena.

Mkuu kwa aina ya demokrasia tunayotumia Tanzania katika suala la maamuzi na kutunga sheria (representative democracy - a form of government founded on the principle of elected individuals representing the people, as opposed to autocracy and direct democracy), ndio anakua hana legitimacy.

Suala linalozungumziwa hapa ni viti maalumu; sasa unavyosema demokrasia ni zaidi ya kupiga kura, unakua unaenda nje ya mada! Upigaji wa kura hauwezi kwepeka katika context hii.

Hakika kama unaweza kumpigia kura mtu husiemtaka, hapo hakika elimu ya uraia itahitajika wallah tena!!
 
Kwamba wao hawatokani na muunganiko wa mbegu na yai kama ilivyo wanaume? Kama lengo lako ni kusema wanawake ni tofauti na wanaume....hilo nakuunga mkono......na ndio mojawapo ya sababu uwiano wa kijinsi unahitajika!

Asante kwa kuelewa lengo langu. Ila hapo kwenye kuhitaji uwiano wa kijinsia ndio unajichanganya tena;kama umeshakubali kwamba hawa viumbe wawili ni tofauti, unafutaka uwiano wa kijinsia wa nini? Uwiano wa kijinsi (jinsi inamaanisha gender kwa kiingereza; jinsia ni sex kwa kiingereza) utapatikana vipi iwapo hawa viumbe ni tofauti hata kijinsi?!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
... Uwiano wa kijinsi (jinsi inamaanisha gender kwa kiingereza; jinsia ni sex kwa kiingereza) utapatikana vipi iwapo hawa viumbe ni tofauti hata kijinsi?!
Thanks and sorry for the confusion. Kwa hakika nilikusudia kusema uwiano wa 'kijinsia' (na sio kijinsi) ambayo kwa uelewa wangu neno 'jinsia' lina maana ya 'gender'.
 
Remmy,

Bado hujajibu maswali yangu:-

Kwasababu unasema viti maalum vilianzishwa baada ya kufanyika study but mie naweza kukwambia kuwa hakuna study iliyofanyika zaidi ya kupitisha yale mapendekezo ya Beijing conference yaliyokuwa yanahamasisha kuwepo uwiano wa wanawake na wanaume katika taasisi mbali mbali. Lakini mapendekezo hayo vile vile yanasema mahitaji yakiwapo sasa tuulizane bungeni kuna haja gani ya kuwepo uwiano?

Ukitaka tuweke uwiano katika chombo cha kutunga sheria labda nikurudishie swali lipi la muhimu kuweka watu makini bungeni wanaoweza kuchanganua masuala mbali na kuweza kututungia sheria au kujaza vimada au wabunge wapambe ambao hawajui hata kimeandikwa nini katika muswada mbali inayopita mbele yao?

Vile vile mbona hivyo viti maalumu hatuvioni katika ulimwengu mnaouona umeendelea mfano Uingereza, USA na Germany. Germany bunge limetawaliwa na wanaume wengi kuliko wanawake. Twende Bunge la Uingereza, Bunge la Marekani vile vile both congress and house of representative.

But why do you think wenzetu hawajaona umuhimu wa uwiano katika mabunge yao but sisi tumeona uwiano katika mabunge?

Umeniuliza kuhusu wabunge waliochaguliwa kuwa vilaza but wana sifa moja ambayo wabunge wa kuteuliwa hawana nayo ni WAMECHAGULIWA NA WANANCHI. Hivyo wanajua matatizo yanayowasumbua wananchi na wamemchagua mwakilishi wao ayawakilisha bungeni. Mbunge wa kuteuliwa anayafahamu matatizo ya wananchi wapi? Vile vile hata kama ni kilaza ni tatizo la wananchi wa jimboni mwake na sio aliyemteua ubunge.

Vile vile kwanini utake uwiano badala ya competence? Uwiano huu ndio unaopelekea kuwepo conflict of interest na watu kushindwa kutetea maslahi ya wananchi na kubakia kutetea maslahi yao binafsi.

Viti maalum vinaharibu demokrasia vya kufutiliwa mbali.
 
Mh. My Friend Regia Mtema, thaanks for your Reach out, you know that I always Love you and Respect you sana, So lets go to work ndugu yangu taifa mbele!

William @ NYC, USA. Mutuz Le Baharia!
 
Nadhani ni wakati wa kumpa mwanamke haki yake ya msingi tu kama wanavyopata wanaume ...
Ndio kuwezeshwa huko! Oh my God! Na wewe ume fall kwenye hii trap, mtumeeee! Ulikuwa the last woman standing hapa, I can't believe it. Umeandika kwa mkono wako mwenyewe kwamba maishani mwako hujawahi kukosa/kunyimwa kitu kwa sababu ni mwanamke. Halafu unatumia the backdoor way kuchomekea madai ya kuwezeshwa! Ndo maana nilikwambia, Gaijin, even the most vehement voices of gender advocacy in the country nimewasikia wakiomba na kusubiri kuwezeshwa.

"Ni wakati wa kumpa mwanamke haki yake," nani ampe?

... kuzungumzia mfumo dume. Sijawahi kuzuilika kufanya kitu chochote kile nilichotaka kwa sababu ni mwanamke.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wabunge wa viti maalum ni kero kero kero. Na kipindi hiki wale wa viti maalum - CCM wanatisha. They look/behave kama vile wametoka red-district. It is sickening na historia itawakumbuka.

Kuhusu mwanasheria mkuu, nadhani kazi yake ibakie kuishauri serikali, na kwa vyovyote vile ASIRUHUSIWE ku-debate bungeni. Kazi yake itaishia kwenye baraza la mawaziri na sio hii ya kujibizana na wawakilishi wa wananchi. Kama wabunge wanataka ufafanuzi basi aitwe kwa utaratibu maalum lakini mwanasheria abaki ofisini kwake. Bunge ni kwa ajili ya wabunge na yeyote anayekwenda bungeni lazima apitie sanduku la kura. No exemption. Yule Mama albino kasaidiaje maalbino wengine kwa kuwepo kwake bungeni? Sanduku la kura. basi.
Wakuu yote haya yanakuja kwa kasi baada ya kazi hii ya ubunge kubadilishwa dhana kutoka kwenye ile ya uwakilishi kwa wananchi iliyokuwa na posho tu ya kutosheleza mahitaji muhimu ya mtumishi huyu wa wananchi mpaka kufikia sasa ambapo nafasi ya mtu kupata ubunge ni nafasi ya kuuaga umaskini kwani wanapata rundo la pesa, mishahara, marupurupu, na ahadi ya ya mafao ya kukufuru pale mwenye nafasi hii atakapokoma kuitumikia nafasi hii, na pia kwa hulka ya mabinti wengi ya uvivu wa kupindukia na ile fikra ya kwamba wao wanauwezo wa kutumia maumbile yao kwa vyovyote iwavyo ili kupata kipato kwani dhana yao ya kujaribu kushindana wao kwa wao na pengine kushindana na wanaume.

Kama ilivyo asili yao imekakamaa na kuitoa hiyo itachukua an effort to change their culture which is of the essence, ukweli uwekwe wazi kwa kuwapongeza wanawake wale wanaothamini haki sawa kwa kupigania hiyo haki kihalali na siyo kwa kujirahisisha rahisisha upande mmoja wanadai wako sawa na wanaume huku upande wa pili wnaregea regea na kugawa na kuumwaga utu wao bila kugundua ni namna gani utumwa huu wa kujitakia unavyo watawala na hautakuja kuondoka iwapo wao wenyewe ni rahisi rahisi na wa burebure namna hii.

Wagundue kwamba kila mwanamke mwenye uke asio uthamini atakapotumia hiyo ati nafasi kupata manufaa isvyo halali, hata wale wnaowatumia watakuwa na uchaguzi na kuwathaminisha kama vile iwapendezavyo na hii hali itaendelea mpaka wanawake wenyewe watakapoiga mifano ya wanawake ngangari kama Mh. Halima Mdee, Mh. Asha Rose Migiro na wengine wanawake ambao hawadeki deki ili waachiwe nafasi.

Historia inaonyesha viongozi na wale wenye heshima kimataifa mfano waziri mkuu wa Australia, Rais wa Liberia na wengine wako ngagari, akina mama tunawapenda sana, ni mama zetu, dada zetu n.k. lakini hili la ati viti maalumu kuwawakilisha mlikatae kwa sababu hao machangudoa wanawawakilisha kinyume nyume and it is really an anarchy!

VAENI NGUO ZENU ILI MPATE HESHIMA! DHARAU MNAJITAKIA WENYEWE KWA KUJIRAHISI!
 
Ndio kuwezeshwa huko! Oh my God! Na wewe ume fall kwenye hii trap, mtumeeee! Ulikuwa the last woman standing hapa, I can't believe it. Umeandika kwa mkono wako mwenyewe kwamba maishani mwako hujawahi kukosa/kunyimwa kitu kwa sababu ni mwanamke. Halafu unatumia the backdoor way kuchomekea madai ya kuwezeshwa! Ndo maana nilikwambia, Gaijin, even the most vehement voices of gender advocacy in the country nimewasikia wakiomba na kusubiri kuwezeshwa.

"Ni wakati wa kumpa mwanamke haki yake," nani ampe?

Hahaha @ Oh my God...Mtumee

Mimi binafsi sijawahi kukutana na mfumo dume wala siuelewi ukoje Tanzania lakini labda mimi sio a typical example na wengi wanakabiliwa na tatizo hilo. The key word here being "labda"

Kwa hiyo kama ni hali ni hiyo, serikali ina wajibu wa kuhakikisha wanawake wanapata haki za msingi za binaadamu kama wanavyopata wanaume (kama nao wanapata).

Kila mtu ana haki ya kupata elimu, lakini siafiki wanawake kuchukuliwa kusoma science or engineering kwa alama za chini na wakaachwa kupewa fursa wanaume wenye alama bora zaidi.

Si haki kwa mwanamke kupewa nafasi ya kutunga sheria Bungeni kwa sababu tu ya uanauke wake.
 
Mimi nakubaliana na wewe kabisa mkuu. Spirit ya kuwa na wabunge wa kuteuliwa ilikuwa kujaribu kuingiza wanamama strong kwenye system kama njia ya kuwawezesha, kwa sababu ku-compete kwenye majimbo ya uchaguzi na wanaume kwenye jamii ambayo ni gender biased ingekuwa vigumu. LAKINI LENGO LILIKUWA KUWAPA NAFASI WANAWAKE WENYE MTIZAMO WA KIMAENDELEO.

Sasa hawa wanaoingizwa sasa hivi hata mimi sielewi anaewaingiza humo bungeni. Ni wale wanaoenda kushindana kuvaa na kusukuma mikoko ya maana. Nchi haiendelei kwa kuagiza sana kutoka nje, bali kwa kuzalisha. Hii ni changamoto kubwa sana kwetu kwa sababu tunahitaji viongozi wa kike wengi tu (reasons are obvious, Madingi zetu walioko madarakani wametu-let down kwa kuwa wezi.

Wote ni wezi ambao kila mmoja anajitahidi awezavyo kuchota kwa ajili ya familia yake tu na wala hafikirii nchi itakuwa wapi 50 years later kila mtu akifanya hivyo). Sasa hatuwezi kuwa na wezi tupu kwenye safu ya uongozi!!! Wamama walau wana uoga kidogo. Nadhani wabunge wa kuteuliwa wateuliwe kwa kuwapima IQ kwanza!!! Sijui tufanyeje, lakini tunahitaji viongozi wanawake, kwa sababu nchi zote zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi ni zile zilizowawezesha wanawake mapema.
 
Mdondoaji,
Well said mkuu!! Nimeuliza sana nini faida ya hivyo viti maalumu; mkuu Remmy akasema vinaleta uwiano wa kijinsi. Nikamuuliza kwani ni lazima kuwa na uwiano? Akasema haitaleta picha nzuri kwavile bunge litajaa wanaume!!. Hivi bunge likijaa wanaume wanaofanya kazi kwa manufaa ya taifa (ya watu waliowachagua) kuna ubaya wowote?!!? Au bunge lenye uwiano (wakiwepo wanawake) ambalo halina tija kwa taifa?!

Naona ameshakimbi tena.....

Hatuhitaji taifa lenye kujaa huruma kwa wanawake wasiokua na tija kwa taifa lenyewe; kama mwanamke anahisi anaweza kuwa kiongozi mzuri hazuiliwi kwenda kuomba kura na kuwashawishi wananchi kwamba anaweza kuwaongoza. Na si kukaa kusubiri kupewa ubunge wa bure husio na uwakilishi halisi na halali wa wananchi.
 
Picha nzuri kivipi? Kwa vile wao ni wanawake?! Ufike wakati watu (wanawake kwa wanaume) waingie bungeni kwa merits aisee. Kwaiyo kama ana uwezo wa kusimama jimboni na kuweza kuwashawishi wananchi kwamba anaweza, basi hakuna shida. Lakini hili la kutaka eti bunge lilete picha nzuri kwa kujaza wanawake ambao wanakua hawako worthy kuingia bungeni, haliko sawa hata kidogo.
Wapo wenye picha nzuri kabisa, mfano Halima Mdee,Prof.Anna Tibaijuka tena ni prof! Akina Makinda hawa wanapambana majimboni na tena wanaheshimiwa, picha nzuri maanake nini? Angalia rais wa Liberia! these women have to be watu kwanza ndiyo wawe wanawake, wanatanguliza uke mbele ndo maana wanatumiwa ovyo!
 
Hakuna ubaya wa viti maalum na tutapigania haki viendelee kuwepo ila tutapigania mfumo uliowazi, wenye heshima na ukweli katika kuteua wabunge hao.

Wanawake walio wengi na vijana bado hawana uwezo (kifedha, na vinginevyo) wa kushindana katika majimbo na midume na wenye fedha. Equal opportunity bado inahitajika pamoja na kwamba imekuwa abused na Chama Tawala na hata vyama vya upinzani. Tufikirie ni mfumo gani utahakikisha na kuondoa upendeleo usio na tija kwa taifa katika kuteua wabunge wa viti maalum.

Ofcourse mahawara na vimada (ama kwa maana ya uhusiano wa kimapenzi na viongozi ama uhusiano wa upambe na kujipendekeza kwa viongozi) bado wataendelea kufaidika kama hatutapigia kelele muswada wa sheria ya kubadilisha katiba uliopo mbele yetu. Yaliyojitokeza katika bunge hili ikijumlisha wanawake kupandikizwa kusema maneno yaayoonyesha upeo wa mdogo katika siasa ni matokeo ya mfumo wetu uliojaza mamlaka kwenye mhimili mmoja wa dola na kuendekeza dhana ya chama kushika hatamu. Na hii itaendelea kututafuna kama nchi hata kama CHADEMA wataingia madarakani.

Katika mfumo uliopo hata ukinipa mimi madaraka sintafanya lolote tofauti kwani mfumo hautoruhusu.

Suluhisho letu ni kubadili mfumo na kufungua fikra za wananchi kama kina Anna Kilango ambao katika maisha yao hawajawahi kuishi na kuona utaratibu mwingine wa utawala zaidi ya ule waliokulia na uliowatoa kutoka kusikojulikana na hata kujulikana nani anaweza kutaka mfumo huo ubadilike wakati yeye anafaidika nao?
 
Mi nadhani wanawakilisha viti ndo maana wameitwa wabunge wa viti.

Bunge letu lina zaidi ya wabunge 120 wa hivyo viti maalum na kila mmoja analipwa takriban mil 7 kila mwisho wa mwezi, unakutana na mbunge shangingi kabisa, kichwani ni bogus yaani ni matope na wengine hata kidato cha sita hawajamaliza ni kuunga unga tu na vikozi uchwara halafu anaingia bungeni. Hivi anafanya nn huko?

Billions zinapotea kwa kuwalipa na kuwapa mikopo hawa wabunge wanaowakilisha viti.

aaah vitu vingine vinaboa jamani.
 
Nadhani Suala la hawa Mama zetu kuwepo Bungeni kwa hilo Linalosemwa VIti Maalum bado si baya kwa nchi kama yetu kuleta anagalau uwakilishi huu,lakini nadhani iwepo muda maalum wa Mbunge wa viti maalum kuendelea kuwa Mbunge kupitia huo Mgongo,Miminapendekeza Miaka mitano inatosha kuwapa na kuwajengea uwezo wa kupambana na Wanaume huko katika majimbo.

Mbona Halima mdee Kaweza,Mbona Regia Mtema ndiye Mbunge wa watu uliacha yule magamba aliyemchakachua?
hawa akina mama wanaweza!

Inshallah
 
Mimi si Mwanasiasa, na si mtu wa kupigia debe haya mambo ya siasa za Kiafrika... Lakini kuna mambo ambayo uwa nayaona kama si lazima sana yawepo na haswa kwenye safu ya uongozi wa nchi.

Haya mambo ya kuwa na Wabunge wa viti maalum , Wabunge kuwa Mawaziri, Wakuu wa mikoa kuchaguliwa n a Rais... Mikoa kuwa na Meya hapo hapo kuna Mkuu wa Mkoa... Yote haya ni maswala ambayo yanapaswa kuangaliwa upya.

Kwa sababu mtu akigombea ubunge kisha anachaguliwa tena kuwa Waziri, kunapunguza uwakilishi wake Bungeni. Na kama wabunge kubaki kuwa wabunge kutaondoa tamaa ya Wabunge kujipendekeza kwa serikali ili wachaguliwe kuwa mawaziri....

Kuhusiana na muda au vipindi vingapi kwa maoni yangu mimi as long as wananchi wanakupenda na uwezo wa kuwakilisha na kutatua matatizo ya wananchi unayo basi endelea kugombea... Hii ni kwa ngazi ya ubunge... Na wanapaswa kuwa na ofisi kwenye majimbo yao au hata ofisi ndogo uko vijijini, na iwe lazima mbunge kutembelea jimbo lake na vitongoji mwake kila mwaka, na hakishindwa basi hawajibishwe na atumie pesa au posho anazolipwa uko bungeni (yaani kusiwe na pesa za ziada kutoka serikalini wala asiombe kwa wananchi, labda wananchi wapende wenyewe kumchangia au chama chake kifanye utaratibu wa kumpatia)

Vilevile kwenye Ukuu wa Mikoa ingependeza zaidi kama hawa wakuu wa mikoa nao wakagombea au kupigiwa kura kama wanavyo pigiwa kura wabunge.... Hii kutawalazimisha kuwajibika kwa raiya zao... Au hao wabunge wa Mkoa au jimbo ndio wanapaswa kugombea nafasi ya Ukuu wa mkoa, hapa ina maanisha kuwa Wabunge wakishirikiana na mkuu wao wa mkoa (ambaye naye ni mbunge) wanakaa katika baraza ambalo wao pamoja na viongozi wachache wa kiraiya, wakiwemo wakuu wa wilaya na raiya waliochaguliwa kuingia kwenye kamati ya kujadiri matatizo ya wananchi, ndio wataamua nini kipelekwe uko bungeni na ikiwezekana miswaada ya bunge inapitia ngazi hii kwanza na kupata maamuzi wa kila mkoa na kisha ndio uko bungeni kunapelekwa mapendekezo au maamuzi ya kimkoa, kwa sababu wananchi washa shirikishwa na uwamuzi ushatolewa.

Kama haiwezekani basi iwepo serikali ya majimbo, ambayo itakuwa na uwajibikaji mkubwa wa majimbo...

Mfano:
Dar Es Salaam, Pwani na Morogoro, linaweza kuwa ni jimbo Moja.
Kagera, Kigoma, na Mara,
Singida, Dodoma na Iringa
Rukwa, Mbeya
Ruvuma, Mtwara na Lindi
Kilimanjaro, Manyara na Tanga
Zanzibar
Pemba
Au ikachaguliwa mikoa yenye kupakana na yenye ukaribu zaidi.

Gonga Hapa: Dhuluma Haiondoki Bila Kubadili Mfumo
 
Back
Top Bottom