Ndio maana wanadai katiba Mpya. Hujawasikia wakipinga Wabunge kuteuliwa kuwa mawaziri bila bunge kupitisha, Uchaguzi wa majaji wakuu upitishwe bungeni, Kuondolewa nafasi za Ma RC, Ma DC, Kiti cha rais na Waziri mkuu kimoja wapo kiondolewe..Mgombea Urais wa chama cha siasa kushiriki pia ktk kugombea Ubunge jimboni au kupewa kiti maalum bungeni na mengine mengi tu..Ni kweli kuwa Chadema walilazimika kuchagua hao kwa sababu mfumo upo tayari, lakini chama hakijaonyesha kutokubaliana na mfumo huo uliopo.
Katika sera na ajenda zao za hatua zinazofaa kuchukuliwa ili serikali ibane matumizi, hatujawasikia kulitaja hili hata wakati mmoja ikitoa picha kuwa wapo sambamba na CCM katika kuukubali mfumo huo. Ukiangalia pia wabunge waliochaguliwa na Chadema kushika nafasi hizo, huoni tofauti yoyote na CCM. Wote wamejaza ndugu, jamaa na marafiki
Hata hivyo wakikataa wao mtawaita wajinga kama wanavyoitwa leo kutoka Bungeni. Kama wangekaa bungeni na kupinga wakati mchezo unaendelea wasingeweza kuwashinda wabunge 300 wa CCM.. Hilo wananchi na wapenzi wa CCM hawalioni..Kifupi ni kwamba wabunge wote bungeni ni wawakilishi wa vyama kiutendaji na sio wananchi hata kidogo.. huu ndio mfumo tunaoupiga vita wananchi.