Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakuu naombeni mawazo yenu
wabunge wa viti maalum ni ubadhirifu wa hela tu. Waliochaguliwa na wananchi wanatosha. Ni kuliongezea taifa mzigo wa matumizi yasiyo na maana
Kama Ubunge wa viti maalumu ni ubadirifu vipi ule wa kuchaguliwa?
Naamini katika utaratibu huu wa kuwapatia wanawake sauti ili hatimaye na wao watoe mchango kwa taifa lao kwani kutokana na mfumo dume ambao umetawala conscious na subconscious mind yetu basi bila huu utaratibu pengine bunge lingekuwa na more than 80% wanaume na hali ya maisha ya mtanzania ingekuwa mbaya zaidi ya sasa.
Lakini napenda nikosoe utaratibu unaotumika kuwapata hawa wabunge wanawake na pia concept nzima ya gender katika siasa za Tanzania, kwani unafuata mfumo ule ule dume wa kupata hao wabunge; japo kuwa ni wanawake lakini wengi wao ni wanaume kimtazamo na hivyo kuendeleza mfumo ule ule dume ambao tunapingana nao.
Kwanini na sema hivyo kwa sababu hali inajionyesha kama hao hawana fikra dume basi maisha ya mwanamke na mtoto (kundi kandamizwa) wa tanzania yasinge kuwa kama yalivyo sasa kwani hali ni mbaya mahospitalini kwa wanawake wanaojifungua; watoto wanaokufa wakiwa wachanga; mimba za watoto wakike shule za msingi etc
Napenda niweke wazi kuwa tunapoongelea gender haina maana mwanamke tu, no na hii ni misconception ya concept hii ndiyo maana wanawake wenye mawazo ya mfume dume wamefanikiwa kuuteka na kuutumia kwa manufaa binafsi na hivyo ku abuse this precious opportunity ya kumkomboa mwanamke kama kundi moja wapo la jamii lililokandamizwa na mfumo dume.....
Ili kutoa ufafanuzi wa haya ninayo yaongea naomba wana JF walio na access na vyombo vya habari hasa star TV kwenye kipindi chake cha Asubuhi; ITV kwenye kipima joto wa waalike TGNP kuweka vizuri hii dhana na kuelimisha umma wa watanzania kuhusu nini maana ya Gender and Development (GAD) tofauti na concept za zamani I mean the whole process of how it came into existence and how has it evolved over time na vipi huu mfumo wa kisiasa unavyo fanikisha wanawake wenye mawazo ya kimfumo dume ku dominate hizo nafasi hivyo kusababisha lengo la hii affirmative measures kutofikiwa
Mimi ni activist wa Gender na kwa usongo basi nikiwa undergraduate was the best University student in DS mwaka wa pili; swali la gender ndo lilinipa maksi ya kupita wote na hatimae kupewa award ya Bank kuu....acha niji promote kidogo au siyo! Kwa hiyo kwa theory sihaba naifahamu Gender japo simzidi mama Usu Mallya ambaye pia ni mwalimu wangu wa Gender. I know for sure she can put this concept right kama hata ogopa siasa za Tanzania!
Miongoni mwa mambo yanayo ifilisi nchi hii, ni kuendekeza mifumo inayobuniwa kukidhi matakwa ya kisiasa. Jambo hilo limepelekea tuwa na serilikali kubwa mno, inayokula rasilimali yote ambayo vinginevyo ingeliwekezwa katika mipango ya maendeleo. Hii ni pamoja na kuwa na bunge kubwa lisilo na tija; kuwa na wilaya ambazo kwa kiwango kikubwa kazi zake zingeliweza kufanywa na halmashauri za wilaya; kuwa na msululu wa mawaziri na manaibu waziri wasiokuwa na kazi n.k. Itakuwa vema iwapo katiba mpya inayotarajiwa itaweka utaratibu mzuri wa kudhibiti mambo hayo.
Kama Ubunge wa viti maalumu ni ubadirifu vipi ule wa kuchaguliwa?
Kwanini na sema hivyo kwa sababu hali inajionyesha kama hao hawana fikra dume basi maisha ya mwanamke na mtoto (kundi kandamizwa) wa tanzania yasinge kuwa kama yalivyo sasa kwani hali ni mbaya mahospitalini kwa wanawake wanaojifungua; watoto wanaokufa wakiwa wachanga; mimba za watoto wakike shule za msingi etc
!
matumizi mabaya ya pesa za umma wabunge hawa wafutike period..katiba mpya iondoe kabisa