Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimelipigia kelele hili muda mrefu tu humu. Tunaigharamia sana SIASA huku huduma muhimu kwa WATANZANIA ikidorora vibaya.
Bunge hili ni kubwa sana ndugu yangu. Majimbo ni mengi bila sababu. Kuna viti 10 vya Rais. Kuna viti 5 vya Baraza la Wawakilishi mbali Wabunge zaidi ya 50 toka NCHI ya Zanzibar! Kwa uchumi huu na ukubwa huu wa Bunge ambako tayari ndani ya miaka hii 50 ya uhuru tumeshajenga majengo makubwa mawili ya Bunge kwa gharama za ajabu, sasa hivi upo mpango wa kujenga nyumba zaidi ya 350 za Wabunge pale Dodoma. Umetengenezwa mfuko maalum wa kuwakopesha Wabunge wote magari kila baada ya miaka mitano. Nusu ya mikopo hiyo italipwa na serikali na riba ya huo mkopo nusu ni asilimia3 tu!NI muda wa kupiga kelele zaidi mkuu husichoke
maana wao hawatachoka kukutoza kodi kila mwezi kuna kila sababu
za kupiga kelele mpaka kilelewe , hii hoja inaitaji umoja wa wananchi maana naona kama
vyama vya siasa hazina mwitikio kabisa na mambo kama haya maana wao ndio wananufaika na hizi nafasi
lakini sisi tunaumia na kuwashabikia, tupige kelele bila kujaru vyama vyetu itawezekana tu,
Kwa nchi zetu za africa wanawake bado wanadharaulika,mi naona ni jambo jema tu wanawake kupewa hivi viti maalum,ili na wao watoe mchango kwenye jamii, ila sasa malengo yanatumika vibaya sijui mchumba wa fulani, mama mkwe, marafiki.
Siku moja nilikuwa nasoma moja ya hotuba ya hayati Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwakumbusha Wanajeshi wetu majukumu.Akatoa mfano wa nchi ya marekani wakati wa kudai usawa kati ya wamarekani weusi na weupe. Ikafikia sehemu akatoa mfano wa kesi zilizokuwa zinaendeshwa mahakamani baada ya weusi kufanyiwa faulo mbalimbali. Unajua Mahakimu walikuwa wanaamuaje? Wanamwita mweupe(mf George) wanamuliza "Bw. George kwa nini umemtemea mate huyu Ghachocha(mweusi)? Hujui kama kwa misingi ya katiba yetu yeye ni sawa na wewe? Haya nendeni,usimtemee tene mate huyu;mko sawa" Unajua nini kinafuata? Usishangae kuona hatua tano kutoka mahakamani ametemewa mate tena na kesi ikawa vilevile!
Labda ntawakera baadhi yenu lakini nakiri siyo lengo langu na naomba nisamehewe. Mpaka hapa mimi nimejifunza kuwa USAWA HAUOMBWI. Usawa huu mnaoutaka wenzetu haupatikani kwa kupitia migongo ya wanaume wanaotuhumiwa kuwanyanyasa.Badala yake mkitaka usawa wenye heshima onyesheni kweli kwamba mnaweza! Msipewe bure! Mkiona wametangaza nafasi na nyie kachukueni fomu. Pigeni kampeni sambamba na wanaume.Mkishinda mtakuwa mmeweza. Mkipewa nafasi tu hapo siyo tu mtakuwa hamwezi bado ila pia mtakuwa mmejidhalilisha zaidi kwa kusubiri kumegewa,Na kwa hiyo mtakuwa hamjui mnafanya nini! Unajua ni kipi kibaya kuliko vyote hapo? Ni hiki kipengele cha kulipa fadhila kwa waliokumegeeni. Mtaendelea KUDHALILIKA TU.(Igeni kwa Hilary Clinton;wale wanaweza!)
Siyo Huko mjengoni tu,kote;mshuleni maofisini mitaani n.k. Mkisikia kuna nafasi 200 za sekondari wafundisheni binti zenu na wadogo zenu kuzipigania hizo 100. Na mkitaka kuonyesha mnaweza "kama wanaume" kama mnavyodai msikubali kushushiwa alama kwa kigezo cha kuwa wanawake.Mkikubali mwisho wa siku itakuwa kweli kuwa mlipeleka wasichana 100 wasio na sifa kwa vigezo ila walioachiwa tu na haohao wanaume ili tu mridhike mko sawa.Haya ni matusi na yataendelea hivyo mpaka muelewe tatizo liko wapi.Msitake kuwezeshwa kabisa!Vinginevyo huo usawa hautakuwa na heshima!Hii kaulimbiu ya kitoto ya "WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA"ifutwe kwani inawafanya dhalili zaidi.Kwamba bila huruma na fadhila za wanaume hamchomoki hapo.Mpaka muwezeshwe!USAWA HAUOMBWI.
Mkiona kuna kikosi cha wanajeshi kinajiandaa kwenda kwenye operationi ulizeni kuna wanawake wangapi wanakwenda? wako kwenye vitengo gani? Msikubali spicial treatment wala favours! Chukueni the same standard,no more no less.Hapa watawaheshimu.Lakini kabla ya 'kukagua majeshi' kakagueni mafunzo ili mhakikishe wanajifunza sawasawa na wanaume,No favours no special treatment. Ndugu zangu safari ya kudai usawa ina miiko.Kama mnanielewa hii ndiyo njia sahihi!
Kwa hiyo kwa mtizamo wangu hivi viti maalum Havina maana.Vimelenga kubebe kundi fulani la marafiki ambao hawajapata nafasi rasmi serikalini.Ila kwa kuogopa upinzani usiseme na wao wakaruhusiwa! Hivi ni kweli kuna mtu anaweza kuniambia inakuwaje kuna MBUNGE wa VITI MAALUM VIJANA.Mbunge ambaye sisi vijana anotuwakilisha hatujamchagua wala hatujashirikishwa uteuzi wake? Huu Ni upuuzi.
Ni kweli kuna wanaosaidiasaidia lakini kwani hata wasiosaidia kwani wanawajibika kwa nani hawa? Ulisikia wana ofisi au bosi zaidi ya waliowateua? Labda tupate mfano; Mbunge wa viti maalum Mh.Mch.Dr. Lwakatare tangu ameingia bungeni hiyo awamu ya nne kuna aliyewahi kumsikia akichangia hoja yoyote? Pamoja na u sifuri huo mbona bado karudi na kiti chake Maalum?
Hii ni hasara kwa taifa.Mishahara nauli na posho jumlisha usafiri na mengineyo! Lakini si ni kweli pia kuwa hii nchi haina viongozi mwenye kuijali? Huu ni mfano tosha. JAMANI TUBADILISHE HII KATIBA KWANZA HALAFU TUANZE KUKAMATANA UCHAWI MCHANA. Hasara hizi si za msingi Kabisa na zinauma kuzitafakari.!!!!
Nilikuwa Sijajua kama wapo 102 Duh! Ukiwatizama kuacha wenye ulemavu wengi ni nyumba ndogo na wakwe za wenye nguvu ndani ya vyama.
''Wajiuzulu haraka Sana'' hawana tofauti na wahujumu uchumi Ndio wanaozomea sana bungeni.
Ati wanasema hushirikiana na wabunge majimboni mh!!
Ati Wabunge wasipokuwepo wao hukava nafasi!! oi..
Basi kama ndio hivyo kipato kiwe sawa!? kwa kukaimu tofauti na katiba isemavyo blah!
Wizi mtupu!
Watizame wapime harafu wafanye Uamuzi...W.Mukama
Dr kashilia ameongea lakin napingana nae katika mtindo alioshaur kuwa katika majimbo kumi manne wagombee wanawake kwa kwel hiyo sikubalian naye kwasababu wananchi wanataka mwakirish bora atakae watumimikia kwahiyo tusilazimishe kuwawekea wanawake hata kama ni wabovu eti kwasababu tunataka kukidhi haja ya wanawake wanne katika kila majimbo kumi, kinachotakiwa kama wanaweza na wao waingie majimbon wagombee kama wenzao akina Halima Mdee, Anna Kilango na wangineo. Kwahiyo cha muhimu mimi naona kwel viti maalum vifutwe kwasababu moja kubwa kwamba wanatumiwa kwa ajil ya maslah ya watu na maslah ya chama na si kwa maslahi ya wananchi au kwa Taifa. Kitu kingine nakubaliana pia na Dr Kashilila katika swala la wakuu wa mikoa na wilaya inabidi waondolewe kwasababu :-
kama tuna mkurugenzi mtendaj wa wilaya mkuku wa wilaya ni wa kazi gan kama hayupo pale kwa maslahi ya Chama? Na kama tuna katibu wa mkoa Mkuu wa wilaya wa nini? Mwisho nakubaliana kuwa viti maalum vifutwe na wakuu wa mikoa na wilaya wasiwepo na hili suala liangaliwe vizuri katika katiba mpya kama tutaipata. Ni hayo tu kwa Leo. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Sijuhi Kashirira naye ataitwa mchochezi,tusubiri
kimsingi wanaongeza umasikini kwa kufaidi rasilimali zetu,napendekeza tutafuta ratio kwa kila mkoa labda tuweke tu kwamba pale chama kinaposimamisha wagombea wake ama kimajimbo ama kimkoa basi iwe razima kila chama kitenge asilimia kadhaa ya wagombea wake eg.20% wawe ni akina mama
na wao waende wakasimame majukwaani waombe kura watakaochaguliwa waende na watakaoshindwa kwenye kura basi ilimradi vyama vitakuwa vimewasaidia kwamba walipewa nafasi lakini kupitia sanduku wananchi hawajamchagua fulani
nadhani hii itasaidia kuwabeba kichama lakini na wao watakuwa wameonesha wamepigana na wananchi wamewaridhia ...hii vipi wanajamii
tatizo wanawake wamejilegeza mno, badala ya kupambana kama wanavyodai 50 kwa 50 sasa wanakuwa wanategemea jeck za wanaume, na mbaya wanaume wasiomuogopa Mungu ukijipendekeza kuwa karibu yake lazima akuchakachue kwa kukuahidi viti maalum. wanawake andamaneni kupinga kupewa viti maalumu. Mnadharilishwa kwa hilo
siku moja nilikuwa nasoma moja ya hotuba ya hayati mwalimu nyerere alipokuwa akiwakumbusha wanajeshi wetu majukumu.akatoa mfano wa nchi ya marekani wakati wa kudai usawa kati ya wamarekani weusi na weupe. Ikafikia sehemu akatoa mfano wa kesi zilizokuwa zinaendeshwa mahakamani baada ya weusi kufanyiwa faulo mbalimbali. Unajua mahakimu walikuwa wanaamuaje? Wanamwita mweupe(mf george) wanamuliza "bw. George kwa nini umemtemea mate huyu ghachocha(mweusi)? Hujui kama kwa misingi ya katiba yetu yeye ni sawa na wewe? Haya nendeni,usimtemee tene mate huyu;mko sawa" unajua nini kinafuata? Usishangae kuona hatua tano kutoka mahakamani ametemewa mate tena na kesi ikawa vilevile!
Labda ntawakera baadhi yenu lakini nakiri siyo lengo langu na naomba nisamehewe. Mpaka hapa mimi nimejifunza kuwa usawa hauombwi. Usawa huu mnaoutaka wenzetu haupatikani kwa kupitia migongo ya wanaume wanaotuhumiwa kuwanyanyasa.badala yake mkitaka usawa wenye heshima onyesheni kweli kwamba mnaweza! Msipewe bure! Mkiona wametangaza nafasi na nyie kachukueni fomu. Pigeni kampeni sambamba na wanaume.mkishinda mtakuwa mmeweza. Mkipewa nafasi tu hapo siyo tu mtakuwa hamwezi bado ila pia mtakuwa mmejidhalilisha zaidi kwa kusubiri kumegewa,na kwa hiyo mtakuwa hamjui mnafanya nini! Unajua ni kipi kibaya kuliko vyote hapo? Ni hiki kipengele cha kulipa fadhila kwa waliokumegeeni. Mtaendelea kudhalilika tu.(igeni kwa hilary clinton;wale wanaweza!)
siyo huko mjengoni tu,kote;mshuleni maofisini mitaani n.k. Mkisikia kuna nafasi 200 za sekondari wafundisheni binti zenu na wadogo zenu kuzipigania hizo 100. Na mkitaka kuonyesha mnaweza "kama wanaume" kama mnavyodai msikubali kushushiwa alama kwa kigezo cha kuwa wanawake.mkikubali mwisho wa siku itakuwa kweli kuwa mlipeleka wasichana 100 wasio na sifa kwa vigezo ila walioachiwa tu na haohao wanaume ili tu mridhike mko sawa.haya ni matusi na yataendelea hivyo mpaka muelewe tatizo liko wapi.msitake kuwezeshwa kabisa!vinginevyo huo usawa hautakuwa na heshima!hii kaulimbiu ya kitoto ya "wanawake wakiwezeshwa wanaweza"ifutwe kwani inawafanya dhalili zaidi.kwamba bila huruma na fadhila za wanaume hamchomoki hapo.mpaka muwezeshwe!usawa hauombwi.
Mkiona kuna kikosi cha wanajeshi kinajiandaa kwenda kwenye operationi ulizeni kuna wanawake wangapi wanakwenda? Wako kwenye vitengo gani? Msikubali spicial treatment wala favours! Chukueni the same standard,no more no less.hapa watawaheshimu.lakini kabla ya 'kukagua majeshi' kakagueni mafunzo ili mhakikishe wanajifunza sawasawa na wanaume,no favours no special treatment. ndugu zangu safari ya kudai usawa ina miiko.kama mnanielewa hii ndiyo njia sahihi!
Kwa hiyo kwa mtizamo wangu hivi viti maalum havina maana.vimelenga kubebe kundi fulani la marafiki ambao hawajapata nafasi rasmi serikalini.ila kwa kuogopa upinzani usiseme na wao wakaruhusiwa! Hivi ni kweli kuna mtu anaweza kuniambia inakuwaje kuna mbunge wa viti maalum vijana.mbunge ambaye sisi vijana anotuwakilisha hatujamchagua wala hatujashirikishwa uteuzi wake? Huu ni upuuzi.
Ni kweli kuna wanaosaidiasaidia lakini kwani hata wasiosaidia kwani wanawajibika kwa nani hawa? Ulisikia wana ofisi au bosi zaidi ya waliowateua? Labda tupate mfano; mbunge wa viti maalum mh.mch.dr. Lwakatare tangu ameingia bungeni hiyo awamu ya nne kuna aliyewahi kumsikia akichangia hoja yoyote? Pamoja na u sifuri huo mbona bado karudi na kiti chake maalum?
Hii ni hasara kwa taifa.mishahara nauli na posho jumlisha usafiri na mengineyo! Lakini si ni kweli pia kuwa hii nchi haina viongozi mwenye kuijali? Huu ni mfano tosha. Jamani tubadilishe hii katiba kwanza halafu tuanze kukamatana uchawi mchana. Hasara hizi si za msingi kabisa na zinauma kuzitafakari.!!!!
Labda hao wanawake wakianza, baadaye hata Tanzania nzima tutaandamana kwa kudhalishwa na misaada toka nchi za nje ama na kuibomoa CCM iliyotujengea (wake kwa waume) tabia ya kupenda utegemezi.