MBUNGE KUWAKANGA VITI MAALUMU SOON, HII NI JANA ALIPOKUWA KWENYE MJADALA WA KATIBA MPYA
Mbunge wa Ziwani (CUF) na hoja binafsi
Katikati ya mjadala huo Mbunge wa Jimbo la Ziwani, Mohamed Zuberi Ngwali (CUF), alisema umefika wakati wa kujadili fedha za umma na hata nafasi ya wabunge wa viti maalumu, ambao hawana kazi kubwa kuliko wabunge wa majimbo.
Alisema katika kuhakikisha anasimamia fedha za umma yupo mbioni kuwasilisha hoja binafsi bungeni, kwani wabunge hao hawafanyi kazi kubwa zaidi ya kununua hereni za dhahabu na magauni wawapo bungeni.
Nitawasilisha hoja binafsi ili kuhoji nafasi na kazi za wabunge wa Viti Maalumu bungeni
sisi tupo wawakilishi wa majimbo tuliochanguliwa wao wana kazi gani? alisema na kuhoji mbunge huyo.