USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Kuna mmoja wa viti maalumu namuona hapa amejipara kama anaenda kwenye kitchen party, mbaya zaid anasinzia hapa nadhani baada ya lunch yake leo aliteremshia na shots kadhaa za whisky.

ndio kilichompeleka bungeni ati we hujui?
 
mkuu mada yako inamashiko sana! viti maalumu wasiwepo kabisa wanakula kodi zetu bure! mihuwa najiuliza kila jimbo lina mtu wakuwakilisha aliyechaguliwa na wanainchi hata kama aliiba kula sasa mnaongezea nawaviti maalumu anamwakililsha nani?mbona mdee aliweza tena alikuwa anapambana na wanaume? hata katibu wabunge kuna gazeti fulani nilisoma aliwahi kusema vitimaalumu nimzigo kwawalipa kodi! mbaya zaidi unakuta viti maalumu anapewa uwaziri!
 
Kuna mtu aliwahi kukwambia kazi yako ni kutuletea walichosema wenzio na yaliyojiri ndani ya CDM.
Naona alikuwa sahihi kabisa, umejiaibisha mwenyewe sasa tunajua uwelewa wako ulivo chini sana.

TZ hatuna tatizo na kumchagua mgombea yeyote wa kike, ndani ya vyama walete idadi kubwa ya wagombea wa kike na watu watawachagua tu kama wana uwezo. Haya mambo ya kupewa ni mzigo kwa taifa na ukichunguza hawa wabunge watakuwa wapo kwa maslahi ya wanaowachagua [wenyeviti na makatibu wa vyama (la mapenzi sijui!)]. Hawana lolote la maana kusema wanawakilisha wanawake

Kwa Kweli Dada Regia Hapa Umepotoka Kidogo!! Hili suala ni serious na linagusa Masilahi ya Watu!! Mmojawapo walioguswa ni wewe Pia!! Ila kwa Kuchangia katika suala Kama hili unahitajika kuwa na Busara Kidogo!! Mambo ya personal kama Kuooana They are Too Personal si Ya Kuingiza kwenye Katiba!! Ila kusema Ukweli wabunge Hawa wa bure ni Mzigo Mkubwa Kwa walipakodi!! Ni bora ukaliangalia Katika Mtazamo Huo!!!
 
Hallow Bill....this is definitely true..we need to get rid of this...kuna wabunge wa viti maalum wanamaliza miaka mitano ..hawajapata kufunua midomo...Yao...inanuka tu...Kama Kutakuwa na haja ya kuwa na wabunge wawili wanawake kila mkoa wapigiwe kura kwenye uchaguzi mkuu...

Process yakuwapata hao wawili ndiyo itakuwa tatizo maana hapo ndiyo nguvu ya madaraka na pesa ya hao hao wanaume ndiyo itakayo determine nani awepo kupigiwa kura. Hilo lakupigiwa kura siku ya uchaguzi ni lamuhimu sana ila process ya kuwapata nani wakupigiwa kura inahitaji consesus ya kitaifa zaidi kuliko kichama. Kuna njia nyingi sana za kuja na representation ya kitaifa kwa wanawake kama dhamira itakuwa kuwakilisha wanawake lakini kama ni polygamism ili ku strengthen nguvu za hao hao wanaume mabaazazi basi itakuwa kama inavyotokea kwa mambo ya katiba sasa hivi. Na huu wa sasa ni mfumo dume kwa asilimia 100.

Gender is not about sex (fe/male) only is about the disadvantaged; yaani kutokana na income, age, education, location i.e rural vs urban and many other independ variables lakini katika yote sex inakuwa confounding factor so katika hili tunatakiwa ku-adjust the equation tu yakuhakikisha katika hilo wanawake ndiyo most disadavantaged when you bring the two sex in these categories of independent variables.

Ukiangalia katika hilo group lote lililopo huko bungeni ni % ngapi wana represent women-rural; Lowly educated; low in income kwa mfano...Je kwa age ni wangapi labda wana represent akina mama wazee wasiokuwa na pension kijijini; vijana wa watoto wasio na kipato kikubwa etc etc..Utaona wengi (% kubwa, najua wengine watakuja na jina moja ku-justify their evil acts) ni watoto wa vigogo ndiyo wawakilishi wa vijana; wake za viongozi na wafanya biashara kuwakilisha miradi na position za male-linked relatives na wachache saaanaaa ndiyo true representative wa disadvantaged group.

Sipendi kutaja majina lakini acha kwahili niwe mkweli wa ninayo yafikiria kama raia (Personal views)...

Hivi Mh. Anna Abdallah kwa mfano anawakilisha kundi lawakina mama gani disadvantaged? Hajawahi kuwa na shida ya ajira wala pension, hajawahi kosa house girl nyumbani kwake wala pesa ya kununua dawa ya malaria kwaajili ya mtoto wake; amekuwa kiongozi tangu mm sijazaliwa so alihitaji afirmative measures gani ili aingie bungeni? Huyu tayari alikuwa na nafasi nzuri yaku-represent women at various capacities alizowahi kuwa nazo. Huyu ni mmoja kati ya wengi huko katika CCM

Ama Lucy Owenya kwa mfano anawakilisha vijana gani hao wakitanzania waliokuwa disadvantage; anajua wapi maswala yao? Alishawahi omba ajira akajua maana ya kukosa huku ukiwa tegemeo pekee kule kijijini kwenu, alishawahi kukosa scholarship kwamfano kwa wakati mwafaka ukapata wakati umeolewa huku umeacha watoto wako wachanga wengine kwakukosa malezi ya mama kufa eti kwasababu mama imebidi akasome ili kulinda ajira if for example ni mwalimu chuo kiku? Huyu tayari ana nafasi ya ku-represent vijana wenzake kwa nafasi familia yake iliyo mpatia. Baba kuwa mwakilishi Bungeni tena kwa ideology inayo fanana na yake na pia katika biashara zake. Angeweza saidia vijana wengi sana kuwa enterprenuers na kuwasaidia kuanzisha miradi mingi sana hapo hapo anako represent sasa hivi maana baba hapo politically ana opportunity hiyo angeweza kumpatia hiyo audiance bila kutumia public funds or office kwa manufaa binafsi bali manufaa ya vijana wakitanzania. Na huyu ni mmoja kati ya wengi (CDM).

Hawa siyo kwamba niwabaya no and absolutely nooo! Ni kwasababu tu mazingira waliyokulia hayawapi uhalali wa kuwa true representative ya hiyo disadvantaged group ndiyo maana hizo group hazipati unafuu wowote wa kimaslahi kwa upande wa enacted policies za nchi.

Hao nilio watumia kama mfano wanisamehe wala wasi personerlize for thats how I see them in my eyes na thats what I can say before them if I am to be asked in their presence.
 
- Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya, Tanzania TUTAONDOKANA NA Wabunge wa Bure na Viti maalum, I am sick na Bunge kujaa vimada wa Viongozi wa vyama vyetu vya siasa vyote kuanzia CCM mpaka Upinzani, ENOUGH! Wabunge wote wawe wa Majimbo tu
Only Mwanasheria Mkuu ndiye aruhusiwe kuingia Bungeni na Cabinet bila kugombea jimbo!

- Taifa letu linapoteza Shillingi Billioni 90 kila miaka mitano on hawa Wabunge wa bure, that is insane kwa taifa masikini kama letu.

Much Respect People!

William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!

For the FIRST TIME EVER, i give my hand of appreciation to you William, tuliona hilo mapema, hata b4 2010 election, hawa Vihiyo are biggest loss to government & kula kodi za wananchi maskini bure, kazi kujipodoa podoa tu bungeni of which Parliament is a most respected place, wapo kama hawapo, hawafai, ni mzigo, kero, fuata upepo, parasites, hasara, HIVI HADI LEO MUULIZE YEYOTE NCHI HII HAWA WABUNGE VIHIYO KAZI NA MALENGO YAO NA WANAWAWAKISHA NANI, no answer, HATUWATAKI TENA, hata RAIS analiona hili, labda maskini anaona aibu kusema publicly bcoz aliukuta mfumo huo, NOW ENOUGH IS ENOUGH, wanyonyaji wa wazi hawa, KATIBA MPYA IWATUPILIE MBALI, i am tired of these, wanaudhi kweli, i am done....!!!
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.

Mmmhh...!!! Njoooni muone huyu ndiye @ atleast among wabunge wa bure nilikuwa nakupa some credit, now i withdraw, i didn't expect this hasa kwako now no respect Regina, kumbe unatetema ur own maslahi, huangalii taifa,
This is not substandard is out of standard, si hoja ni kiroja,
Hapa nitakupiga misumari ya uhakika, omba msamaha, hawa wabunge vihiyo plus u inclusive are all parasites, kupe wote, ukweli unauma Regina, now ownwards i degraded u to 5% kuhusu utaifa wa nchi hii, huna uzalendo, UNA UBAVU KWELI WA KUTETEA VITI MAALUM KISA WW UPO, inaniuma sana, hufai kabisa Regina, VITI VYA BURE HATUVITAKI, ww ukiwemo unakula kodi za wananchi bure, niambie KAZI YAKO NI NINI UKIAMKA ASUBUHI KAMA MBUNGE HEWA, unamwakilisha nani,?wapi,? ofisi yako iko wapi? Semaaaa, ww ni mbunge hewa, period...!!!
 
Ni wanawake wachache sana wana caourage ya kusema ulichokisema. Niko karibu sana na baadhi ya wanaharakati wa haki za wanawake, na huwa wananishtua na kufedhehesha wanapotetea viti vya wanawake. Hawaelewi kabisa nadharia ya kulemazwa na "uharibifu chanya" kama aliouongelea mtumwa Frederick Douglass alipokataa kata kata msaada wa kuokolewa na mtu yule yule anaemzamisha ili ajifunze kusimama wima mwenyewe:

Hili suala la kuwa viti maalum vinadhalilisha wanawake lipo wazi na dhahiri kabisa na iwapo wanaharakati/watetezi wa haki za wanawake hawaelewi hilo kwa dhati kabisa basi kutakuwa na matatizo makubwa zaidi kuliko tunavyodhani.

Utalalamika vipi juu ya mfumo dume kisha ukautaka huo huo mfumo dume ukuondolee matatizo yako? Kauli mbiu ya 'Mwanamke ukimuwezesha anaweza' ni zaidi ya dharau kwa wanawake wote. Huyu anaetakiwa 'kumuwezesha' mwanamke ni nani? Mwanamme? Na kama mwanamke asipowezeshwa jee? Asifanye kwa vile hawezi, asubiri mpaka awezeshwe?

Kauli mbiu hiyo pamoja na uwepo wa viti maalum kwa wanawake vinamfunza nini msichana mdogo anaekuwa? Awe tegemezi kwa mwanamme?

Nashindwa pia kuelewa vipi mwanamke anatetea wanawake wengine ata endorse mfumo usiokuwa hata na "value for money". Kuna worth gani ya kutumia bilioni 90 "kuwawezesha" wanawake 100 tu?
 
sipendi kupewa upendeleo fulani kwa kuwa tu eti mimi ni mwananmke!!! hili linadumaza sana wanawake kifkra na kuona kwamba 'aah whatever the case I am a woman and I will be favored'

sijawahi kuunga mkono viti maalum na sitaunga mkono huu upuuzi kwa kuwa mpaka hapa sijashawishika kuona manufaa yake...
 
Zaidi ya kudumaza fikra za wanawake lakini pia ina undermine juhudi za wanawake walioweza wenyewe bila ya utegemezi kwa wanaume. Imekuwa sasa mwanamke akisimama ameweza mwenyewe watu wanaanza kujiuliza "ni kimada wa nani". Vinatudharaulisha mwanzo mwisho

Vifutwe mara moja
 
na hata hao walipo kwenye viti maalum si ndivyo wanvyochukuliwa? mara kadhaa tunasoma humu humu kuwa mbunge yule na yule na yule (wa viti maalaum) ni chakula cha fulani na fulani na fulani. (kwamba hatujiwezi asilani pasipo'fanywa' au fanyiwa jambo fulani)

huu upendeleo badala y akutujenga sasa naona unatuharibia jumla!
 
No problem nahisi ni jinsi wanavyopatikan na si lazima wawe wakinamama
 
Instead ya ku chagua vimada wangewapa
upendeleo
walemavu
ili wapate mahali pa
kuwasilishia matatizo
yanayowakabili
hawa wanaopewa bure
hivi viti ni kupaka wanja kuvyaa vikuku
na kupigana vikumbo
mjengoni
 
Katiba Mpya pia izuie Wabunge kuoana Kama ilivyotokea kwa Wazazi wako na Ubunge uwe na Kikomo kama Urais sio mpaka mtu anazeekea Bungeni kama Mzee Malecela.

Hawiji, ammh kaya yikuva nahau ha! Pungushi lilakali muhaja wangu, kuva mundu mkomi, paudeta udeti chikomikomi, kotokuvavika tatimundu na mamundu, daiwi nyanyi haa. Nenga muhaja waku.
 
John haukumbuli baba yako alipotoka kuwa balozi alipewa huo ubunge? na baagaye kuteuliwa Mbunge? hakuwa na jimbo muda mrefu

Alikuwa na huo ubunge wa kupewa....
 
- Ni matumaini yangu makubwa sana kwamba kwenye katiba mpya, Tanzania TUTAONDOKANA NA Wabunge wa Bure na Viti maalum, I am sick na Bunge kujaa vimada wa Viongozi wa vyama vyetu vya siasa vyote kuanzia CCM mpaka Upinzani, ENOUGH! Wabunge wote wawe wa Majimbo tu Only Mwanasheria Mkuu ndiye aruhusiwe kuingia Bungeni na Cabinet bila kugombea jimbo!

- Taifa letu linapoteza Shillingi Billioni 90 kila miaka mitano on hawa Wabunge wa bure, that is insane kwa taifa masikini kama letu.

Much Respect People!

William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!

Mkuu wabunge wa vitu maalumu wawepo kwa wale ambao hawana chama chochote kama mimi. Ukiangalia ni idadi kubwa sana ya Watanzania si wanachama wa vyama. Hivyo kutokuwasikiliza au kupata maoni na kuwatetea itakuwa hawatendewi haki. Kwa mfano uchaguzi uliopita wapiga kura wote kama sikosei walikuwa milioni 6 ambao kisheria wanajulikana ni wa vyama vyote, wakati huo huo jumla ya watanzania wote ni milioni 40. Ndio kusema watu hawa milioni 36 ambao sio wanachama hawawakilishwi na mbunge yeyote na kwa kweli hakuna demokrasia
 
Bi. Regia Mtema,
Unasikitisha sana, mbunge mzima kuja hapa na kutoa kauli za ajabu kabisa. W.J. Malecela ni raia mwananchi ambaye katoa hoja yake wewe MBUNGE mzima unakuja na majibu kama hayo? hufahamu kwamba kauli kama hii inaweza kuja haribu hata Uwakilishi wako..

Jaribu kuwasoma raia wananchi wako, uelewe nini hasa kinachowasumbua kisha nawe njoo na hoja ama umuhimu unaoona kuwepo kwa viti maalum lakini dada yangu hayo uloyatoa sii majibu kabisa ila matusi makubwa sana kwa wazee ambao wengi wetu hapa kijiweni tunawaheshimu acha mbali kabisa wadhifa walokuwa nao.

Kwa mfano:- Leo hii asilimia 70 ya nguvu kazi (kama sii zaidi) ni Wanawake lakini pato lao kwa ujumla toka wahudumu wa nyumbani hadi maofisa ni chini ya asilimia 30 ya pato la wanaume, wanawake pia wanahodhi chini ya asilimia 20 ya ardhi yetu na kadhalika. Wanawake ndio mama wa taifa na familia hivyo kuwezeshwa kwake sio swala la kujaza wawakilishi bungeni bali kuwakilisha taasisi na jumuiya za wanawake..(huu ni mfano tu sina takwimu..) Sasa unatakiwa kuchaguliwa mwanamke kuwakilisha wanawake kwa hoja kama hii bungeni..

Inasikitisha sana kuona hata UWT kimekuwa umoja wa wanasiasa wakike CCM, yaani kimebadilika kuwa chombo cha kisiasa badala ya kuwa chombo cha kusimamia haki za wanawake wote nchini. Leo hii Mwenyekiti wa Jumuiya hii - Sophia Simba is a politician wakati zamani huyu mama alitakiwa kuwa msimamizi wa shughuli na michango ya wanawake ktk ujenzi wa Taifa letu...UWT ilikuwa JUMUIYA ya Wanawake nchini na sio tawi la chama.

Sasa pengine approach ya watu haikuwa nzuri toka mwanzo na ndio maana ukafyatua vuvuzela..Nakuomba sana utujuze,kwa nini unaona umuhimu wa kuwepo viti maalum. Kumbuka Bunge letu sio chuo cha kujifunza wala mahala pa kupeana semina isipokuwa ni ukumbi wa wawakilishi wa wananchi toka majimbo tofauti n.k. Wewe pale bungeni unawakilisha kundi gani?
 
Ana wakilisha interest za chama.

Kwa sababu kwanza wananchi wa Kilombero walimkataa jimboni. Pili, hata wanawake wanaounga mkono CHADEMA hawakumchagua, aliteuliwa 'kisayansi'.
 
Back
Top Bottom