Habari waheshimiwa,
Najua mada hii inaweza kupokelewa kwa namna tofauti na baadhi yetu. Naomba radhi mapema. Ieleweke kuwa sijaandika kwa ajili ya kumdhalilisha yeyote, wala si kwa nia mbaya. Ni katika kuweka sawa pale ambapo naona kuna ulaghai wa wazi.
Kipindi cha nyuma niliwahi kuandika kuhusu dhana potofu kuwa viti maalum ni kwa ajili ya kuleta uwiano na vina maslahi gani kwa Taifa. Leo tena nimeona ni vema niongelee hili. Kimsingi ni kuwa hata baada ya kupita muda bado sijashawishika hata kidogo kuikubali dhana hii. Nitatoa sababu chache.
1. Kama viti hivyo ni kwa sababu busara za viongozi ziliamua kuwa kuna makundi maalum (mf. vijana) ambayo yanapaswa kuwakilishwa ni jambo zuri. Lakini kama kuna heri ndani ya hili wazo ni kwa nini wasiiweke hii nafasi iwe rasmi,vijana wagombee, sisi vijana tujichagulie wawakilishi wetu? Ni nani atanishawishi kuwa hao walioteuliwa ndiyo wawakilishi wetu? Kwani vijana wako hawapo? Hapa siwaelewi haraka!!!
2.Kama swala la msingi ni kuweka uwiano wa makundi ya wanawake kwa wanaume napo siyo mbaya. Lakini kama ni hivyo kwa nini nafasi hizo zisirasimishwe halafu tuwaache wanawake wajichagulie muwakilishi wao? Ni nani ataona nakosea kama nitakuwa na wasiwasi (not necessarily me) na jinsi wateule hawa wanavyopatikana?
Nani atanilaumu nikisema hii ilipitishwa ili kupata nafasi ya kuwapa ulaji tu wale wenzao ambao walikuwa pamoja kwenye harakati nyingine na wamekosa nafasi rasmi za kwapa ili kulipa fadhila? Ni nani anaweza kunishawishi kwa sauti, hadharani kuwa kuna utaratibu rasmi wa kuwateua hawa wateule? Na ni nani leo atalaumu kwa dhati kabisa, toka moyoni akisikia watu wanlalamika kuwa nafasi hizi wanawapa mahawara, wachumba, na ndugu zao?
Kama hili ni katika harakati ya kuweka usawa wa jinsia si neno pia. Lakini ninapata mashaka pale ambapo naona mazingira ya upatikanaji wa hawa Wabunge wateule yana utata. Mazingira haya yenye utata hayatapelekea Wanawake kutojikomboa tu ila yataendelea kuwadhalilisha na kuwafanya watumwa wa fikra na hoja za wengine ( waliowateua) Vinginevyo sioni jinsi mbunge teule anavyoweza kusimama na "kutounga mkono hoja 100%" ikiwa wale wa kuchaguliwa wenyewe wameamua kulinda shibe zao badala ya kuwawakilisha wananchi. Hiyo haitaleta usawa wowote! USAWA SAHIHI HUJA KWA MISINGI SAHIHI!
Siku moja nilikuwa nasoma moja ya hotuba ya hayati Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwakumbusha Wanajeshi wetu majukumu.Akatoa mfano wa nchi ya marekani wakati wa kudai usawa kati ya wamarekani weusi na weupe. Ikafikia sehemu akatoa mfano wa kesi zilizokuwa zinaendeshwa mahakamani baada ya weusi kufanyiwa faulo mbalimbali. Unajua Mahakimu walikuwa wanaamuaje?
Wanamwita mweupe(mf George) wanamuliza "Bw. George kwa nini umemtemea mate huyu Ghachocha(mweusi)? Hujui kama kwa misingi ya katiba yetu yeye ni sawa na wewe? Haya nendeni,usimtemee tene mate huyu;mko sawa" Unajua nini kinafuata? Usishangae kuona hatua tano kutoka mahakamani ametemewa mate tena na kesi ikawa vilevile!
Labda ntawakera baadhi yenu lakini nakiri siyo lengo langu na naomba nisamehewe. Mpaka hapa mimi nimejifunza kuwa USAWA HAUOMBWI. Usawa huu mnaoutaka wenzetu haupatikani kwa kupitia migongo ya wanaume wanaotuhumiwa kuwanyanyasa.Badala yake mkitaka usawa wenye heshima onyesheni kweli kwamba mnaweza! Msipewe bure! Mkiona wametangaza nafasi na nyie kachukueni fomu.
Pigeni kampeni sambamba na wanaume.Mkishinda mtakuwa mmeweza. Mkipewa nafasi tu hapo siyo tu mtakuwa hamwezi bado ila pia mtakuwa mmejidhalilisha zaidi kwa kusubiri kumegewa,Na kwa hiyo mtakuwa hamjui mnafanya nini! Unajua ni kipi kibaya kuliko vyote hapo? Ni hiki kipengele cha kulipa fadhila kwa waliokumegeeni. Mtaendelea KUDHALILIKA TU.(Igeni kwa Hilary Clinton;wale wanaweza!).
Siyo Huko mjengoni tu,kote;mshuleni maofisini mitaani n.k. Mkisikia kuna nafasi 200 za sekondari wafundisheni binti zenu na wadogo zenu kuzipigania hizo 100. Na mkitaka kuonyesha mnaweza "kama wanaume" kama mnavyodai msikubali kushushiwa alama kwa kigezo cha kuwa wanawake.Mkikubali mwisho wa siku itakuwa kweli kuwa mlipeleka wasichana 100 wasio na sifa kwa vigezo ila walioachiwa tu na haohao wanaume ili tu mridhike mko sawa.Haya ni matusi na yataendelea hivyo mpaka muelewe tatizo liko wapi.Msitake kuwezeshwa kabisa!Vinginevyo huo usawa hautakuwa na heshima!Hii kaulimbiu ya kitoto ya "WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA"ifutwe kwani inawafanya dhalili zaidi.Kwamba bila huruma na fadhila za wanaume hamchomoki hapo.Mpaka muwezeshwe!USAWA HAUOMBWI.
Mkiona kuna kikosi cha wanajeshi kinajiandaa kwenda kwenye operationi ulizeni kuna wanawake wangapi wanakwenda? wako kwenye vitengo gani? Msikubali spicial treatment wala favours! Chukueni the same standard,no more no less.Hapa watawaheshimu.Lakini kabla ya 'kukagua majeshi' kakagueni mafunzo ili mhakikishe wanajifunza sawasawa na wanaume,No favours no special treatment. Ndugu zangu safari ya kudai usawa ina miiko.Kama mnanielewa hii ndiyo njia sahihi!
Kama nilivyosema awali, kwa mtizamo wangu hivi viti maalum havina maana.Vimelenga kubeba kundi fulani la marafiki ambao hawajapata nafasi rasmi serikalini.Ila kwa kuogopa upinzani usiseme na wao wakaruhusiwa! Hivi ni kweli kuna mtu anaweza kuniambia inakuwaje kuna MBUNGE wa VITI MAALUM VIJANA.Mbunge ambaye sisi vijana anaotuwakilisha hatujamchagua wala hatujashirikishwa uteuzi wake?
Au kuna mtu anajua imekuwaje Mbunge mteule James Mbatia ameteuliwa kuwa mbunge?( Brother James this is not personal please.) My logic is kama Mbatia kwa mfano tu, aligombea ubunge, wananchi aliokuwa anaomba ridhaa yao wakaona hatoshi, wakashindwa kumchagua, leo anateuliwa na rais akamwakilishe nani? Huyu alimteua (no offence) ametumia akili ipi? Huu Ni upuuzi!
Ni kweli kuna wanaosaidiasaidia lakini kwani hata wasiosaidia kwani wanawajibika kwa nani hawa? Ulisikia wana ofisi au bosi zaidi ya waliowateua? Labda tupate mfano; Mbunge wa viti maalum Mh.Mch.Dr. Lwakatare tangu ameingia bungeni hiyo awamu ya nne kuna aliyewahi kumsikia akichangia hoja yoyote ya msingi? Pamoja na u sifuri huo mbona bado karudi na kiti chake Maalum?
Hii ni hasara kwa taifa!.Mishahara nauli na posho jumlisha usafiri na mengineyo! Lakini si ni kweli pia kuwa hii nchi haina viongozi mwenye kuijali? Hasara hizi si za msingi Kabisa na zinauma kuzitafakari.!!!!