USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

USHAURI: Tubadili mfumo wa viti maalum, vifutwe!

Sio viti maalum kwa sasa ni vitanda maalum.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Sijawahi kuheshimu viti maalum na wala sitakuja kuviheshimu kwani havina maslahi kwa nchi zaidi ya maslahi kwa vyama vinavyoteua.
Vifutwe!
 
Je kina mama wataweza kupita na kushinda wengi wanaogopa hawana moyo kama kina mdee,makinda,kilango

sasa mbona wakipewa huo uvitu maalumu wanatupigia kelele kwamba tupo sawa? Wengine wanachochea wake zetu watunyime unyumba?
 
wabunge hawa hawana mchango wowote,zaidi ya kuwapendezesha walio wateua na vyama vyao. Dhana ya kuwa empower wanawake katika ngazi za kiuongozi ni udhalilishaji wa kijinsia. Hawa huunga mkono kila kitu.hata yenye tija kwa taifa likiletwa na wapinzani wao hupinga na kuzomea.

Hata spika wa bunge hili aliwah kusema wasibweteke na kupewa u viti maalumu,wajiandae kwenda majimboni kugombea.
Kwa katiba mpya hawa wasiwepo kabisa wakayapiganie majimboni kupata ubunge kwa kuchaguliwa.
 
Sina hakika kama ni chanzo cha matatizo yote.

Lakini ni chanzo cha mengi.

Hata Mkulu wa sasa alitokea hukohuko.
 
Kwanza kabisa niwe wazi tu katika hili kuwa kitu tulichokikosea katika taifa letu ni kuwa na wabunge wa viti maalumu.hawa wabunge wamekua wa kwanza katika kutetea upumbavu ilimrad tu waonekane na wenyewe wamo.Mfano mzur ni hawa wabunge wa CHAMA CHA MAJANGA wanatia aibu bungeni,unakuta anatetea na kusema serikali ni sikivu wakati watanzania tunaona serikali ni KIZIWI.

CHAMA CHA MAJANGA kinawatumia sana hawa kujipigia kampen na wanasahau kuwa bungeni si sehemu ya kupeleka wapiga makofi tu bila kuwakilisha wananchi.Katika elimu pia WANASIFIKA KWA KUUNGAUNGA ILIMRADI TU WAWE NA SIFA YA KUPIGA DOMO KWA KISWAHILI KIRAHISI WAWE NA SIFA YA KUONGEA.WANALIPWA FEDHA NYINGI ZA WALIPA KODI ILA HAWANA MCHANGO WOWOTE.

PENDEKEZO
WABUNGE WOTE WAPIGIWE KURA NA WANANCHI NA MAMBO YA UVITI MAALUMU YASIWEPO ILI IKIFIKA MUDA WA KUJUA MBIVU NA MBICHI WANANCHI TUFANYE KAZI YETU.

ANGALIZO KWA CCM
HAKUNA CHAMA KILICHOTAWALA MILELE KAMA KIPO KINYUME CHA HAKI NA USAWA NA MIFANO IPO WAZI NA INAJULIKANA.MNACHOFANYA LEO KITAWA COST KESHO.

ANGALIZO KWA WABUNGE
USIFIKIRI KUTETEA CHAMA CHAKO ANGALI UNAUJUA UKWELI NA KUUPINGA KUTAKUSAIDIA KATIKA TAIFA LETU LENYE WATU WEREVU NA WALIOSOMA KWA MDA HUU.NAWE PIA NAKUHAKIKISHIA UNACHOFANYA LEO KESHO KITAKU COST NA WATANZANIA HATUTAKUA NA HURUMA KUMHUKUMU MWALIFU.

*TANZANIA MPYA INAKUJA*
 
hili linatakiwa liwepo kwenye katiba tena wakigwa ban itapunguza na ngono zembe pale mjengoni!!!!
 
Ni dhahiri kuwa hakuna umuhimu wa kuwa na uwakilishi wa viti maalumu coz wanafanya kazi ya kulinda nafasi zao na si kwa maslahi ya Taifa.
 
Hawa wabunge wetu wa viti maluum, wangapi kama halima mdee?
1) Vigezo
2) Nani anawachagua
3) Kazi yao muhimu ni nini haswa
4) Bado tunawahitaji? Na kama ndio je mfumo wa kuwachagua ubadilike?
5) Beside halima mdee kuwa mfano bora wa kuigwa nani mwingine viti maalum anaweza kuwa kama halima mdee
6) Je, umri pia uzingatiwe?

Wadau naomba msaada?

----- Maoni ya wadau-----

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza kuwa nafasi za Wabunge wa Viti Maalum wanaoteuliwa zipo kwa mujibu wa Sheria na zimeainishwa katika Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani amesema kuwa Ibara ya 78 (1) na (4) ya Katiba inaeleza utaratibu mzima wa kuwapata Wabunge wanawake wa Viti maalum.

Amesema kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya Kura zote halali za wabunge kitapata Wabunge wa Viti Maalum kulingana na Kura kilizopata

Amefafanua kuwa Chama kinachopata asilimia 5 ya Kura zote halali za Wabunge katika Uchaguzi Mkuu kinatakiwa kuwasilisha orodha ya majina ya wanachama kinaowapendekeza kuwa wagombea wa Viti Maalum katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Aidha, ameeleza kuwa endapo inatokea nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na sababu mbalimbali, Spika wa Bunge humtaarifu Mwenyekiti wa Tume juu ya uwepo wa nafasi hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343

Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume hukiandikia barua chama husika kukitaarifu juu ya uwepo wa nafasi wazi ya viti maalum ili kiweze kuwasilisha pendekezo la jina katika orodha kiliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015, ikiambatanishwa na Fomu namba 8 D ya kuomba jina lililopendekezwa liteuliwe na Tume katika nafasi ya Ubunge kulingana na vigezo vilivyoainishwa.
 
Last edited by a moderator:
Kila chama kina utaratibu wake wa kuwapata kutoka na idadi watakayopewa kutokana na kura za ubunge nchini.

CCM wanatumia UWT wanachaguana wenyewe kwa wenyewe na kunakuwa na nafasi kadhaa za vijana wa kike, walemavu, NGO etc. Uchaguzi unafanywa na akinamama wenyewe kwa demokrasi bila kuingiliwa.

Kwa chadema huwa vigogo wa chama wanaweka vigezo wanavyoona vinafaa na kuteua wabunge. Wengi wa vigogo hao ni wanaume na hata mwaka 2010 aliyeweka vigezo vya kuchagua wanawake Dr. Kitila Mkumbo. Wanawake wa chadema wamelalamika sana juu ya huu utaratibu wa kuwekewa vigezo na wanaume, lakini uongozi wa chama umefumba masikio.
 
Habari waheshimiwa,
Najua mada hii inaweza kupokelewa kwa namna tofauti na baadhi yetu. Naomba radhi mapema. Ieleweke kuwa sijaandika kwa ajili ya kumdhalilisha yeyote, wala si kwa nia mbaya. Ni katika kuweka sawa pale ambapo naona kuna ulaghai wa wazi.

Kipindi cha nyuma niliwahi kuandika kuhusu dhana potofu kuwa viti maalum ni kwa ajili ya kuleta uwiano na vina maslahi gani kwa Taifa. Leo tena nimeona ni vema niongelee hili. Kimsingi ni kuwa hata baada ya kupita muda bado sijashawishika hata kidogo kuikubali dhana hii. Nitatoa sababu chache.

1. Kama viti hivyo ni kwa sababu busara za viongozi ziliamua kuwa kuna makundi maalum (mf. vijana) ambayo yanapaswa kuwakilishwa ni jambo zuri. Lakini kama kuna heri ndani ya hili wazo ni kwa nini wasiiweke hii nafasi iwe rasmi,vijana wagombee, sisi vijana tujichagulie wawakilishi wetu? Ni nani atanishawishi kuwa hao walioteuliwa ndiyo wawakilishi wetu? Kwani vijana wako hawapo? Hapa siwaelewi haraka!!!

2.Kama swala la msingi ni kuweka uwiano wa makundi ya wanawake kwa wanaume napo siyo mbaya. Lakini kama ni hivyo kwa nini nafasi hizo zisirasimishwe halafu tuwaache wanawake wajichagulie muwakilishi wao? Ni nani ataona nakosea kama nitakuwa na wasiwasi (not necessarily me) na jinsi wateule hawa wanavyopatikana?

Nani atanilaumu nikisema hii ilipitishwa ili kupata nafasi ya kuwapa ulaji tu wale wenzao ambao walikuwa pamoja kwenye harakati nyingine na wamekosa nafasi rasmi za kwapa ili kulipa fadhila? Ni nani anaweza kunishawishi kwa sauti, hadharani kuwa kuna utaratibu rasmi wa kuwateua hawa wateule? Na ni nani leo atalaumu kwa dhati kabisa, toka moyoni akisikia watu wanlalamika kuwa nafasi hizi wanawapa mahawara, wachumba, na ndugu zao?

Kama hili ni katika harakati ya kuweka usawa wa jinsia si neno pia. Lakini ninapata mashaka pale ambapo naona mazingira ya upatikanaji wa hawa Wabunge wateule yana utata. Mazingira haya yenye utata hayatapelekea Wanawake kutojikomboa tu ila yataendelea kuwadhalilisha na kuwafanya watumwa wa fikra na hoja za wengine ( waliowateua) Vinginevyo sioni jinsi mbunge teule anavyoweza kusimama na "kutounga mkono hoja 100%" ikiwa wale wa kuchaguliwa wenyewe wameamua kulinda shibe zao badala ya kuwawakilisha wananchi. Hiyo haitaleta usawa wowote! USAWA SAHIHI HUJA KWA MISINGI SAHIHI!

Siku moja nilikuwa nasoma moja ya hotuba ya hayati Mwalimu Nyerere alipokuwa akiwakumbusha Wanajeshi wetu majukumu.Akatoa mfano wa nchi ya marekani wakati wa kudai usawa kati ya wamarekani weusi na weupe. Ikafikia sehemu akatoa mfano wa kesi zilizokuwa zinaendeshwa mahakamani baada ya weusi kufanyiwa faulo mbalimbali. Unajua Mahakimu walikuwa wanaamuaje?

Wanamwita mweupe(mf George) wanamuliza "Bw. George kwa nini umemtemea mate huyu Ghachocha(mweusi)? Hujui kama kwa misingi ya katiba yetu yeye ni sawa na wewe? Haya nendeni,usimtemee tene mate huyu;mko sawa" Unajua nini kinafuata? Usishangae kuona hatua tano kutoka mahakamani ametemewa mate tena na kesi ikawa vilevile!

Labda ntawakera baadhi yenu lakini nakiri siyo lengo langu na naomba nisamehewe. Mpaka hapa mimi nimejifunza kuwa
USAWA HAUOMBWI. Usawa huu mnaoutaka wenzetu haupatikani kwa kupitia migongo ya wanaume wanaotuhumiwa kuwanyanyasa.Badala yake mkitaka usawa wenye heshima onyesheni kweli kwamba mnaweza! Msipewe bure! Mkiona wametangaza nafasi na nyie kachukueni fomu.

Pigeni kampeni sambamba na wanaume.Mkishinda mtakuwa mmeweza. Mkipewa nafasi tu hapo siyo tu mtakuwa hamwezi bado ila pia mtakuwa mmejidhalilisha zaidi kwa kusubiri kumegewa,Na kwa hiyo mtakuwa hamjui mnafanya nini! Unajua ni kipi kibaya kuliko vyote hapo? Ni hiki kipengele cha kulipa fadhila kwa waliokumegeeni. Mtaendelea KUDHALILIKA TU.(Igeni kwa Hilary Clinton;wale wanaweza!).

Siyo Huko mjengoni tu,kote;mshuleni maofisini mitaani n.k. Mkisikia kuna nafasi 200 za sekondari wafundisheni binti zenu na wadogo zenu kuzipigania hizo 100. Na mkitaka kuonyesha mnaweza "kama wanaume" kama mnavyodai msikubali kushushiwa alama kwa kigezo cha kuwa wanawake.Mkikubali mwisho wa siku itakuwa kweli kuwa mlipeleka wasichana 100 wasio na sifa kwa vigezo ila walioachiwa tu na haohao wanaume ili tu mridhike mko sawa.Haya ni matusi na yataendelea hivyo mpaka muelewe tatizo liko wapi.Msitake kuwezeshwa kabisa!Vinginevyo huo usawa hautakuwa na heshima!Hii kaulimbiu ya kitoto ya "WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA"ifutwe kwani inawafanya dhalili zaidi.Kwamba bila huruma na fadhila za wanaume hamchomoki hapo.Mpaka muwezeshwe!
USAWA HAUOMBWI.

Mkiona kuna kikosi cha wanajeshi kinajiandaa kwenda kwenye operationi ulizeni kuna wanawake wangapi wanakwenda? wako kwenye vitengo gani? Msikubali spicial treatment wala favours! Chukueni the same standard,no more no less.Hapa watawaheshimu.Lakini kabla ya 'kukagua majeshi' kakagueni mafunzo ili mhakikishe wanajifunza sawasawa na wanaume,No favours no special treatment. Ndugu zangu safari ya kudai usawa ina miiko.Kama mnanielewa hii ndiyo njia sahihi!

Kama nilivyosema awali, kwa mtizamo wangu hivi viti maalum havina maana.Vimelenga kubeba kundi fulani la marafiki ambao hawajapata nafasi rasmi serikalini.Ila kwa kuogopa upinzani usiseme na wao wakaruhusiwa! Hivi ni kweli kuna mtu anaweza kuniambia inakuwaje kuna MBUNGE wa VITI MAALUM VIJANA.Mbunge ambaye sisi vijana anaotuwakilisha hatujamchagua wala hatujashirikishwa uteuzi wake?

Au kuna mtu anajua imekuwaje Mbunge mteule James Mbatia ameteuliwa kuwa mbunge?( Brother James this is not personal please.) My logic is kama Mbatia kwa mfano tu, aligombea ubunge, wananchi aliokuwa anaomba ridhaa yao wakaona hatoshi, wakashindwa kumchagua, leo anateuliwa na rais akamwakilishe nani? Huyu alimteua (no offence) ametumia akili ipi? Huu Ni upuuzi!

Ni kweli kuna wanaosaidiasaidia lakini kwani hata wasiosaidia kwani wanawajibika kwa nani hawa? Ulisikia wana ofisi au bosi zaidi ya waliowateua? Labda tupate mfano; Mbunge wa viti maalum Mh.Mch.Dr. Lwakatare tangu ameingia bungeni hiyo awamu ya nne kuna aliyewahi kumsikia akichangia hoja yoyote ya msingi? Pamoja na u sifuri huo mbona bado karudi na kiti chake Maalum?

Hii ni hasara kwa taifa!.Mishahara nauli na posho jumlisha usafiri na mengineyo! Lakini si ni kweli pia kuwa hii nchi haina viongozi mwenye kuijali? Hasara hizi si za msingi Kabisa na zinauma kuzitafakari.!!!!
 
Hakuna tatizo la viti maalum kwani hata wabunge wa kuchaguliwa nao wanamapungufu sana tuu na hawana michango na wengi wao ni chanzo cha migogoro wakijivunia wapiga kura wao.
 
Hii ni namna mbadala ya kudumisha fikra "sahihi za mwenyekiti wa chama"
 
Kusipokuwa na wabunge wa viti maalum viongozi wa CHADEMA watapata wapi "vipoozeo?".
 
Naomba niulize swali: Nani anaweza kunitajia mbunge yeyote wa viti maalum mwenye kutoa hoja bungeni zaidi ya kuchangia na kujichubua? Nina zawadi ya pipi hapa na andazi.
 
Habari wana Jf!
Naomba kuelezwa/kuambiwa kazi za wabunge wa viti
maalum!!! Na kuna faida ya kuendelea kuwa nao??
 
Back
Top Bottom