Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

Ushauri: Umri unaenda sina ninachomiliki

" Imenigusa sana nilipojaribu kuvaa viatu vyako katika fikira zangu"

Wengi wetu tulitegemea elimu zetu ndizo zitakazotukwamua lakini kwa baadhi imekuwa kinyume.

Sasa ni wakati wa kujifunza kwa bidii kutoka kwa wasio na elimu kama zetu na wamefanikiwa kwa kujishusha.
Wakati huo huo uendelee kushukuru kwa Baraka na Neema nyingi ambazo Mwenyezi Mungu amekujalia ambapo kubwa zaidi ni PUMZI na UHAI uliojaliwa hadi Leo hii.
Kuna wenzako ambao walifanikiwa kielimu, vyeo na nafasi katika umri mdogo zaidi yako ila Leo hawapo tena duniani na hawakuondoka na chochote walichomiliki, pia wapo waliofanikiwa kupata mafanikio katika umri wa miaka 50 na hadi Leo bado wanaishi.

Endelea kumshukuru Mungu na ukiomba huku ukijishughulisha kwa bidii na IPO siku utafanikiwa ni mambo ya wakati tu utafika wakati wako utatoka
Hapo umenena kiongozi.. [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
Mmiliki wa alibaba mpaka anafikisha miaka 28 alikuwa hakuna anachomiliki hakukata tamaa ,hilo tatizo sio kwako tu vijana wengi especially tulio soma cha msingi tusichague cha kufanya tujichanganye kwote kwote. Usikate tamaa hatujui mungu katupangia nn kesho .

Song:Naiona kesho by Martha mwaipaja
 
Kazi uliziacha kijijini ukakimbilia madigrii rudi upesi huko ukaungane na wenzako ulime kabla nguvu hazijakuishia.kosa ni la mama yako aliyeolewa na masikini kisha ukazaliwa.njoo tulime.
 
Hakuna mambo ya eti kusoma nilipoteza muda,,,,,,,chora mstari anza upya sasa. Tatizo letu ni ubinafsi.
 
Kama nimekuelewa, mzazi mwenzio ana kipato kizuri. Tafuta wazo zuri la biashara ya kiwango anachoweza ku-finance, halafu mshirikishe
Ni wazo zuri kama ana mahusiano mazuri na mzazi mwenzie anaweza kumuinua akafika mbali hata hiyo ajira asiione ni kitu
 
dah pole sana mkuu... hapo ni kujiongeza tu kukaa karibu na wasiosoma wanaofanya ujasiriamali.. utajofunza mengi sana ya mtaji mdogo na jinsi ya kukuza mtaji.. ukiwa karibu na wamachinga, mama ntilie, na wengineo vijiweni....

kuna vingi tu unaweza fanya kwa mtaji wa laki moja sisi wasomi hatuvijui.. ila wasiosoma wanavijua
Hata wenye Kazi tunafanya shughuli za ziada baada ya saa za kazi tena Kwa mitaji midogo, mno yote nikukwepa madeni madogo yasiyoyalazima. Tatizo vijana wengi wasomi wanaogopa kufanya shughuli flani flani eti wataonekaje ili hali wamesoma!!!!! Na wanataka kuanza na mitaji mikubwa...kumbuka mtaji wa kwanza ni mawazo yako, hivyo unaweza pewa hata mill 2 na usizifanyie kitu...utulivu wa akili ni muhimu mno
 
Mkuu najua maumivu unayoyapitia kwasasa, pamoja na kukabiliana na changamoto zote zilizopo kwenye elimu ila ulijitahidi kupambana hadi ukafanikiwa kwakuwa uliamini elimu ndio itakuwa msaada kwenye maisha yako.. mambo yamekwenda kinyume pole sanaa,,,
Kitu unachopaswa kufanya kwasasa ni kuendelea kupambana na kuishinda sauti inayokushawishi kukata tamaa, endelea kupambana kwa namna yoyote ile hata kama wanakudharau mtaani na pengine rafiki zako uliowaacha mtaani wakiishia Std 7 wana maisha mazuri zaidi yako ila USIKATE TAMAA ENDELEA KUPAMBANA.
Badili namna ya kufikiri na weka elimu pembeni piga kazi kwa namna yoyote ile, hizo kazi ndogo ndogo unazofanya tafuta namna ya kuzifanya ziwe kubwa na zikidhi mahitaji.

If you want to change, you have to be tired and sick of being tired and sick.
 
Salaam wanajamvi,

Jamani naomba mnipe ushauri kutoka kwenu hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha.

Kwanza naweza sema hapa Tanzania kusoma sana ndo kuukaribisha umasikini tu.

Kijana mimi wa kitanzania mwenye elimu ya Bachelor degree na Postgraduate Diploma hadi sasa nagonga 30 years sina cha maana ninachomiliki katika maisha yangu.

Sijui kwa sababu nimetumia muda mwingi kusoma, au hii familia niliyozaliwa ya umasikini ndo chanzo hata sijui.

Nilisoma kwa mkopo wa serikali na postgraduate nikafadhiliwa kwa kujua kwamba nikimaliza nitaingia kwenye system kupitia ualimu wa masomo ya arts imekua ndivyo sivyo.

Umri unaenda sina mtaji sina ndugu wa kuniwezesha kwa chochote kazi zimekua ngumu so nategemea kudra za Mwenyezi Mungu labda nitafanikiwa.

Najishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato lakini hakikidhi mahitaji napata hela ya kula, kulipa kodi miezi 2 2 au 1.

Nina mtoto anaishi kwa mama yake, najisikia vibaya kumwona mwanangu anakua lakini hadi sasa baba yake similiki chochote kitakachomsaidia, mama yake ndo anauwezo kwa sasa wa kumjengea mazingira bora coz kipato chake kinatosha kabisa.

Sina ninachomiliki jamani, naombeni ushauri njia bora ya kuishi, namna ya kufanya ili nami niweze kutoka katika dimbwi hili la umaskini, nakiri kwamba nimesoma na kwa sasa sina ndoto tena ya kutaka kuajiriwa nina ndoto ya kujiajiri lakini sijui wapi napata mtaji, labda itokee nipate ajira ya uhakika ya kupata salary bila usumbufu hapo nitajipanga kudunduliza hela nipate japo mtaji.

Umasikini mbaya sana. Na elimu ya Tanzania inachochea umasikini.

Nipeni ushauri jamani ili mwaka 2018 niwe mtu mpya nijue nini nifanye nami nimiliki japo biashara hata ya kuuza juice, banana power hata shujaa vodka.

Ushauri tafadhali, sihitaji maneno ya kejeli nina frustration zangu.

NAWASILISHA
jichanganye kila kona ukitulia sehemu mmoja utabaki kulaumu
 
We siyo graduated ni graditude huwezi kuwa zoba kwa kiasi hicho nikimuona MTU ana degree halafu analalamika ajira natamani nimtemee mate huna Tina kwa taiga hili kabisa .si ajabu umeacha mashamba kijijini nawe IPO mjini unabanana na washua wakati umeacha Mali ,Mimi na degree ya HRM nibahatika kufanya field wilaya flani hadi Leo nafanya shughuri zangu kwenye wilaya hiyo na sina mpango wa kuajiliwa kabisa .
 
Mkuuu unanifanya niamn kuwa kusoma ndo chanzo cha umaskn katka nchi yetu
 
Back
Top Bottom