Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Huna haja ya kuja mpaka Dar mkuu. Unachotakiwa kufanya ni kufungua website ya kampuni husika kama ni befoward ama sbt kisha chagua gari unayoitaka na kuimudu. Then utachagua pia port of delivery then watakupa kost zote mpaka inapofika bandarini. Yaani CIF.

Kisha utachgua clearing agent wako ambaye atakuchaji dola mia mpaka mia mbili inategemea na clearing agent ambaye pia ataingia mtandao WA ascyuda wa TRA ili kupata actual tax mpaka inasjiliwa. utatakiwa ufanye deposit ya CIF wakati huohuo ukimuachilia agent wako akifuatilia documentation we endelea kumeki tayari kwa ajili ya tax ambayo rafli itakua inakaribiana na kiasi cha CIF.

Usijali pesa zako zi salama kwani una uwezo wa kuclaim mapungufu yoyote yatakayotokea ukisaidiana na clearing agent wako. Mwisho hayo makampuni sio kwamba ni wamiliki wa hayo magari la hasha hao ni madalali tu wa magari yanayouzwa kwa goodwill. Kwa ufafanuzi zaidi waweza nicheki pm.
 
Nataka kuagiza gari kupitia befoward au SBT au Trust sasa naogopa kuibiwa kwenye mitando, na niko mikoani ambako siwezi kufika dar kirahisi nitaagiza vp na nitajuaje kama pesa zangu zi salama sijaibiwa? Swali la pili, gharama ninazoziona kwenye tra calcultor +cif ndo basi nalipata gari langu au kuna nyongeza ya makato? msaada plz urgently!
1. Jinsi ya kuagiza.
Fungua mtandao (Be forward kwa mfano), chagua gari ulilopenda, hakikisha unapata total price (CIF) halafu jaza taarifa zako kwenye fomu halafu click "inquiry". Baada ya hapo watakujibu kupitia email na mazungumzo yenu ikiwemo kupunguziana bei yatafanyika kwa email. Baada ya hapo watakutumia invoice na kukupa maelekezo jinsi ya kulipia bank.

2. Jinsi ya kuangalia ushuru TRA
Fungua calculator ya TRA na ujaze taarifa za gari na bofya 'calculate'. Ikikupa gharama angalia palipoandikwa 'customer value (CIF), hiyo ndio bei elekezi ya TRA. Ile CIF ya gari ikiizidi hiyo ya TRA basi utalipa ushuru zaidi ya hiyo uliyopata baada ya kuingiza taarifa za gari.

3. Tafuta agent
Mkishakubaliana jinsi ya kulipa, utaenda bank na utajaza form maalumu na kutuma pesa. Baada ya siku kadhaa watakutumia documents za malipo ya gari ili uweze kuanza kushughulikia mambo ya ushuru. Utatafuta agent kwa ajili ya ku process hayo mambo.
 
Nilitumia Beforward, my friend alitumia SBT. Wote wazuri.
thanks sana but nashindwa kuelewa maana mfano gali ni cif usd 2000 nilielekeza ina kuwa ni 1.8 ni tra yaan inakuwa hiv kwa kuichange kwa tsh 2000*2000*1.8 = hapo 2000 hiyo ni usd 2000 *2000 kuchange dolar to tsh* 1.8 kama tra calculater
 
Sijakuelewa hapa.
 
Nakushauri utumie BEFORWARD mkuu. Wapo makini sana. Nina experience nao ya kuagiza gari mara mbili. Bei waliyoweka pale siyo fixed, wee komaa nao wakupe discount. Wakikupa bei ya mwisho, wewe watajie yako sasa ambayo itakuwa chini kidogo ya waliyokupa. Walinipaga discount toka 5100$ mpaka 4900 nikawaambie sina 4900, nina 4800 wakakataa. Baadae kidogo wakanitumia email waka kubali. Ilichukua siku 32 kupata gari.

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili kwenye website yao kwaku click inquiry kwenye gari unayotaka ambapo utajaza details zako na email. Watakutumia proforma invoice yenye bei. Utaanza kujibizana nao hadi mfikie muafaka ambapo watakupa proforma invoice nyingine ambayo utaiprint uende nayo bank kuganya malipo. Namba za akaunti, details za gari na za kwako zitaonesha hapo kwenye hiyo proforma.

Bank ukishafanya malipo watakupa Swift Application Form ambayo utawatumia kwa kui scan ili gari isiuzwe tena maana utatakiwa usubirie bank wakupe SWIFT/TT kama siku mbili au moja inategemea na bank gani. Bank wakishakupa swif utai scan na kuwatumia beforwar nao watasubiria malipo yakishawafikia watakutumia Final proforma invoice ambayo itaainisha kila kitu na hiyo ndiyo risit yako ya kununulia gari. Utampa agent wa clearing and forward aendelee na taratibu nyingine kwa malipo mtakayokubaliana.

NB: Email utakayoanzia nayo mazungumzo na beforward iwe hiyohiyo hadi mwisho na uwe unaandika kwa ku reply na ku quote previous email.

Pia hakikisha umeangalia gharama za ushuru wa hiyo gari kwenye website ya TRA kabla hujaagiza ili usijeshindwa kuikomboa. Kila la kheri mkuu
 
Nakushauri utumie BEFORWARD mkuu. Wapo makini sana. Nina experience nao ya kuagiza gari mara mbili. Bei waliyoweka pale siyo fixed, wee komaa nao wakupe discount. Wakikupa bei ya mwisho, wewe watajie yako sasa ambayo itakuwa chini kidogo ya waliyokupa. Walinipaga discount toka 5100$ mpaka 4900 nikawaambie sina 4900, nina 4800 wakakataa. Baadae kidogo wakanitumia email waka kubali. Ilichukua siku 32 kupata gari.
Ila wamenisikitisha baada ya kuja kugundua walichezea odometer. Baada ya muda ikaanza kuchanganyikiwa. Sasa inanionesha natembea hadi km 6000 ndani ya wiki 2. Kazini na kurudi ni 22km.
 
Ila wamenisikitisha baada ya kuja kugundua walichezea odometer. Baada ya muda ikaanza kuchanganyikiwa. Sasa inanionesha natembea hadi km 6000 ndani ya wiki 2. Kazini na kurudi ni 22km.
Pole mkuu. Watu wengi hudanganyika kwakuangalia ODO inayosoma km chache na kudhani hiyo gari haijatumika sana. Ukikuta gari ya miaka ya nyuma sana na odometer inasoma km chache sana achana nayo. Maana yawezekana wamei reverse au ilipataga ajali wakairekebisha na kuipaki bila kuitumia kwa miaka minhi au mara chache chache sana. Pia ukikuta gari ya nyuma sana ila ODO inasoma km nyingi ipotezee
 
Ilikuwa na 96 elfu km. Baada ya document kufika nikaona ilikuwa na owners wawili kabla. Na wote waliitumia kwa umbali wa km 90 hadi laki kila mmoja, lakini huku wanakupa distance ya owner mmoja ambayo nayo unakuta imechezewa. SBT huwa wanaandika kbs hata km ni laki 2.5.
 
Wajamani naombeni kujuzwa, hivi zile kodi zilizokuwepo kwenye mtandao ni za kweli? Mfano kama umekuta ni milion tatu kwa gari x ni kweli itakuwa hiyo? Au kuna mabadiliko
 
Baba Jazey, Kwenye hiyo calculator angalia mahali palipoandikwa 'custom value CIF (USD). Hakikisha CIF ya gari unalotaka haizidi hiyo CIF inayoonekana hapo, utalipia ushuru huo unaooneshwa baada ya calculation. Endapo CIF ya gari unalotaka itakuwa kubwa zaidi ya hiyo ya TRA, basi utalipa zaidi, na ni wao TRA ndio wanajua itazidi kiasi gani baada ya kupiga hesabu upya kutumia CIF yako kubwa.
 
Kwenye hiyo calculator angalia mahali palipoandikwa 'custom value CIF (USD). Hakikisha CIF ya gari unalotaka haizidi hiyo CIF inayoonekana hapo, utalipia ushuru huo unaooneshwa baada ya calculation. Endapo CIF ya gari unalotaka itakuwa kubwa zaidi ya hiyo ya TRA, basi utalipa zaidi, na ni wao TRA ndio wanajua itazidi kiasi gani baada ya kupiga hesabu upya kutumia CIF yako kubwa.
Nashukuru mkuu
 
Back
Top Bottom