Ushauri: Ununuaji wa magari

Ushauri: Ununuaji wa magari

Kwa personal experience yangu hao jamaa ni pasua kichwa. Niliagiza gari, baada ya kulipia imechukua miezi miwili kufika Dar.
 
Jamani nimepata gari nataka kuwapelekea wazazi wangu Tanzania, ni Toyota Carina ya 1997, petrol, manual, 1.8L.
Nimeinunua kwa $750 na shipping cost ni $1000 mpaka Dar. Tafadhali naombeni kama kuna mjuzi anayeweza kunipa gharama za utoaji wa gari hilo hapo bandarini kabla ya kulituma. Asanteni kwa msaada wenu.
 
Gari la mwaka 1997 mkuu ukifika huku bongo utapigwa uchakavu hadi ushangae! Pia mdau kama unataka kuwachukulia wazaz wako gari why uwachukulie mkweche? Ingekuwa ni wewe ungelichukua hilo la 1997? Kumbuka gari kuu kuu kwa mafundi kila siku, mara pump, mara gear haziingii. Why usiwachukulie hata Vitz ya mwaka 2004? Wanaendesha hadi wanasahau kuna cha fundi wala nini.

Huo ni mtazamo wangu tu lakini! Ila kwa hilo la 1997 kodi jiandae kupigwa 5m plus
 
Habari zenu wataalamu? Aisee natarajia kununua Gari aina ya Toyota Caldina ya mwaka 2003 na bei yake kwa mujibu wa Autorec Japan (CIF) ni USD 5,570.

Naomba msaada jinsi ya kukalculate kodi kwa gari hiyo ili nione kama naweza kuagiza ama la kulingana na mfuko wangu. Na pia kama ushauri utakuwepo kuhusu gari hiyo.
 
Ingia kwenye mtandao wa TRA upate RSP ya hiyo gari Caldina then ingiza kwenye calculator yao ikupe CIF Value according to TRA then ingia fanya calculation
 
Mkuu ingia kwenye website ya TRA kuna formula ya GARI YANGU itakupa kodi unayotakiwa kulipa,kwa haraka haraka kwa hiyo gari ulioagiza andaa kama 3M ama kodi tu,
 
Jinsi ya tra wanavyo calculate gharama za gari yako
1. Wanaangalia hyo gari wakati ikiwa mpya bei yake ilikuwa n kiasi gani times(zidisha) kwa 40%(depreciation calculation) mfano hyo opal ya mwaka 2001 ikiwa mpya gharama yake n $30000 then wanazidisha kwa 40%($40000*40%)=$16000

2. Then unachukua 0.25*$16000=$4000(c

3. Gari then imetengenezwa zaidi ya miaka 10 nyuma inachajiwa 20%(dumping fees) 20%*16000=$3200
then jumlisha hizo cost zote $16000+$4000+$3200=$23200

4. Then chukua 0.18 zidisha kwa hyo jumla ya gharama 0.18*23200=$4176
so $4176 ndo itakuwa chaji ya TRA, samahanini ka maelezo yamekuwa marefu ni sababu nimetumia kiswahili ili watu wote waelewe
 
Mazingira, Uzuri wa kununua through Tradecarview, unalindwa dhidi ya matapeli. Utatakiwa kulipia kidogo nadhani ni 5% ya value ya gari kwa huduma hii. Its worthy it maana hutapoteza pesa zako.
 
Haya chakarikeni mkizichoka hizo zote nawakaribisha kwenye ulimwengu wa Vogue.
 
achana nao hao,wana bei kuubwa sana
Habari zenu wataalamu? Aisee natarajia kununua Gari aina ya Toyota Caldina ya mwaka 2003 na bei yake kwa mujibu wa Autorec Japan (CIF) ni USD 5,570.

Naomba msaada jinsi ya kukalculate kodi kwa gari hiyo ili nione kama naweza kuagiza ama la kulingana na mfuko wangu. Na pia kama ushauri utakuwepo kuhusu gari hiyo.
 
Ni gari nzuri. Spares zipo Geniune.
Labda ushindwe kununua tu.
 
Nauza Suzuki ESCUDO - Tshs 10M

Details zake ni kama zilivyo hapa chini:-
Make: SUZUKI
Model: ESCUDO
Body Type: STATION WAGON
Colour: GREEN
Year of manufacture: 1992
Engine capacity: 1590 cc
Fuel: PETROL
Imported direct from Japan. Imetumiwa na mtu 1 tu. Muziki mkubwa, tairi mpya, regular service.
Only serious buyers contact me (dgc64@yahoo.com - 0784599507 or 0713599507)
Nimeamua kuuza kwa kuwa naenda masomoni kwa muda mrefu.
 
Libaba OPAL siyo mchezo, inachagua vituo vya mafuta (wewe utakuwa na undugu wa karibu na BP tu). kuhusu spare sijajua sana ila nilishawahi kusikia watu wanasema eti vifaa vyake ni aghali.

Subiri watu wengine wachangie pia. yangu ni hayo tu


Mkuu naomba nikujibu vizuri sana swali lako kwani mimi ni mtaalamu wa kodi na ndio tunafanya kazi za clearing and forwading, hata kama ukileta mzigo wowote bandarini lazima uwe na Agent wa kukutolea mzigo wako.

kwanza unatakiwa ujue bei ya gari based on CIF (cost, insurance and Freight)
ukishatumiwa tumiwa document tafuta agent wa clearing and forwarding akupe ushauri na gharama
gharama zifuatazo pia usisahau
shipping line charge km dola mia
wharfage charge kama shilingi laki tatu
agent fees kuanzia laki 2 mpka 3
registration fee 330,000
plate number 38,000
kuhusu kodi yake nitakupa jibu sasa hivi
kwa msaada zaidi nicheki sintauj@gmail.com
 
mkuu nimeona hiyo opa kwenye page ya be forward na nimecalculate rate za tra nimepata tsh. 3830800/= kwa bei hiyo unamiliki opa yako simply ukiagiza gari yenye ukubwa wa cc zaidi ya 1500 unatoa asilimia 10 ya cif, as exercise fee, 25% ya import fee na vat 18% angalia link hii mkuu kupata gari yako Used OPA TOYOTA for Sale | BF74798 | Japanese Used Cars Exporter BE FORWARD kila la heri
 
Wakuu naombeni msaada wa gharama za ushuru wa kuzitoa bandarini, gari toka Japan aina ya Nissan Xtrail na Noah, za kuanzia mwaka 2004. Karibuni sana
 
Wandugu,

Hivi Toyota Harrier ya 1998 ambayo CC 3000 Bei Japan inauzwa USD 3990

Hadi ikingia barabarani itakuwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom