mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Majeshi yetu ya Ulinzi na usalama ni vyombo nyeti mno katika mustakabali wa usalama wa nchi yetu (Kisiasa,Kiuchumi na Kijamii). Maeneo ya kambi za Jeshi ni maeneo adhimu na yanapaswa kutochangamana na maeneo ya kiraia kwa namna moja au nyingine.
Miaka michache iliopita tulipata janga la mabomu kulipuka ktk kambi kadhaa za jeshi na kusababisha maafa na utaabishaji mkubwa.Nadhani yatupasa kujifunza na kuepuka ukaribu na maeneo ya kiraia au kuchangamanisha maeneo haya na mambo ya biashara kwa ujumla.
Kwasasa kumekuwa na wimbi kubwa la wafanyabiashara kuwekeza maduka, yards,ofisi,kumbi, showrooms n.k. Inawezekana kabisa nia na lengo ni zuri (Kwa mujibu wa tathmini) kabisa ila kwa unyenyekevu mkubwa nadhani yatupasa kutazama kwa mapana athali zake kiusalama sasa na baadae.