Ushauri: Viongozi wa dini wazuie Quran na Biblia kutumika mahakamani kwa mashahidi kula viapo

Ushauri: Viongozi wa dini wazuie Quran na Biblia kutumika mahakamani kwa mashahidi kula viapo

Felix

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2014
Posts
876
Reaction score
764
Wakuu, nimekuwa nikifuatilia mashahidi wengi mahakamani Wanakula kihapo kwa hivi vitabu, na kudai watasema ukweli mtupu. Na kumalizia Mungu awasaidie. Lakin mwishowe kwenye ushahidi wanasema uongo live live. Kitendo hicho mm naona nikuvinajisi vitabu vitakatifu.

Kwa mfano tu mzuri, hivi Shahidi wa juzi kesi ya Mbowe, shahidi no 5, mwanasheria wa Tigo, hv kweli kabisaa amekana hamjui mbowe Wala hajawai kumsikia kama ni kiongoz wa chama. Mtanzania tena mwanasheria. Uongo wa live kabisaaa. Mungu atawapiga vibaya watu Kama hao.

Sasa basi kama ilivyo Sheria ya nchi kutotumia bendera ya taifa hovyo hovyo, nashauri viongozi wa dini watoe tamko mtu akienda kula kihapo asitumie vitabu hivi. Kitendo cha kuhapa mbele za Mungu uku ukijua anaenda kusema uongo, ni sawa na kwenda mskitini/ kanisani huku mfukoni unabox la condom, ukimaliza ibada unaenda kusheratika. Mbaya sana.
 
Kama wanaongopa huku wakiwa wameapa kwa kutumia vitabu vya dini wanazo ziamini basi hukumu hiyo aachiwe Mungu.
 
Wazo lako sio baya.

Nina mawazo tofauti kidogo, kwa kuwa hao Viongozi wa Dini hawana kipimo cha kupima huo uwongo, basi Mungu atamalizana nao wanaotumia vitabu vyake kwa mzaha.
 
Hao watumishi wa Mungu hawana hati miliki ya dini wala vitabu. Lakini pia unawezaje kumsemea mtu, kama ni kweli hamfahamu?
 
Kwanini mahakama ziwaapishe watu wanaokinzana huku wakijua lazima kuna upanda utaongopa.

Ni mjadala tu sio kuwa ninalaumu mahakama yoyote nchi yotote.
 
Back
Top Bottom