Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Ushauri wa Bure: Diamond saidia baba yako

Cha ajabu zaidi siku huyu mzee akifa, Diamond atatumia gharama kubwa sana kumuaga kifahari. Hicho kibanda anachohishi kitafanyiwa service ndani ya siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haki huendana na wajibu!
Mzee anadai matumzo kwa Dai ,
Je yeye mzee aliwajibikaje katika kumtunza Dai?
Hata ktk hali yaani kumjulia hali alipoumwa kwa mfano alienda kumhudumia?
Au alikuwa na mazoea ya kutafuta kujua mwanae anaendeleaje?
Mbona tangu mdogo hakutafuta vyombo vya habari kuzungimzia mwanae?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUCHUKUA MAAMUZI YA KUMCHUKIA MZAZI MMOJAWAPO NDIYO KUINGILIA KWENYEWE HUKO KWA UGOMVI WA WAZAZI WAKE.

LAITI ANGEKUWA NI MWENYE HEKIMA, ASINGETHUBUTU KUMCHUKIA BABA YAKE MZAZI KAMWE SABABU KUPITIA HUYO BABA YAKE MZAZI NDIYOMAANA KAZALIWA DUNIANI.

KWANI MAMA YAKE DIAMOND ALIJITUNGIA UJAUZITO PEKE YAKE BILA KUJAMIIANA?

MZAZI NI MZAZI TU HAIJALISHI ALIKUTELEKEZA, ALIKUWA MCHAWI, JAMBAZI AU TABIA MBAYA YA AINA GANI MAANA MUNGU NDIYE MLIPIZA KISASI PEKEE.

NA KWA TAARIFA YAKO FIMBO/ADHABU/MALIPO YA MUNGU HUWA NI MACHUNGU SANA KULIKO YA BINADAMU.

SO DIAMOND NI MTU TU KIMWILI LAKINI KWA KITENDO CHA KUMTENGA BABA YAKE, HANA CHEMBE CHEMBE ZA UTU WALA UBINADAMU HATA 0.1%

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo anayofanya Diamond ni kujitia mikosi tu kwenye maisha yake...
 
Sio kweli mkuu, hizo media zinazomuhoji si ndio nafasi ya kujieleza
Mzee alisema ana mengi ya kumweleza mtoto, DIAMOND anakatazwa na mama YAKE,, hivi mtoto anakataliwa mimba? Mchanga? Au ukubwani?Huyo DIAMOND MSHAMBA TU,,huwezi kumdhalilisha BABA YAKO KIASI HICHO ,,,na pengine hajuwi hata ile siku MIMBA YAKE INAINGIA,,baba YAKE alitumia NGUVU KIASI gn kulazimisha PENZI KWA MAMA YAKE,, BABA NI BABA hata awe CHIZI..wewe unaona ni sawa? Mzazi kutembeza viatu barabarani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajuaje kama na mimi nimelelewa na mama na bado nikamtafuta baba nikiwa mtu mzima. Nimesema na ninarudia tena dini yangu inasema samehe saba mara sabini

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza ukamtafuta baba yako sawa na hata Diamond nae amemtafuta baba yake na anafahamu anapokaa..changamoto iliyopo hata kwa mzee wake mwenyewe Diamond ni kitu kinaitwa "MATARAJIO" yaani baba anatarajia support kubwaaaaaa na jamii pia inapenda Diamond atoe support kubwaaaaaaa kulingana na aina ya kipato anachopata (nadhani dogo ana provide service kwa mzee wake na kama kweli umelelewa na upande mmoja utakuwa na ushuhuda mzuri sana kwamba mtu anapolelewa na upande mmoja alafu akabaki kule ambapo kuna dhiki kuu mara nyingi huwa anapoteza feelings kabisa kwa upande mwngine wa mzazi ambao ulikuwa una angalau hivyo hata akimtafuta baba yake akamfahamu bado hatokuwa close nae kivile tofauti na yule aliekuwa nae kwenye dhiki na faraja lakini haina maana kwamba anamchukia.

Changamoto tu kuna wasemaji wengi wa familia ya Diamond wakati ukweli wa maisha yao wanaujua wenyewe na mwisho wa siku watu wafuatilie maisha yao maana wengi tu humu wanaishi nyumba nzuri za kisasa lakini wazazi wao wanaishi maisha ya kawaida na ndipo hapo chanzo cha walimwengu kumwona kama dogo hamsaidii baba yake wakati kinachotokea ni kuwa hawapo karibu kivileee na hii inatokana na familia zenyewe ukute dogo akienda kwa mdingi those days hapati mapokezi mazuri.

Nimepitia hii hali na mie yaani upande mmoja wa mzazi sio unawachukia na support ninatoa lakini ule ukaribu unakuwa haupo kivile sema kwa wengi wanaopitia kwenye hii hali sio mastar ndio maana inaonekana kawaida. Ndio maana hata unapoona ndugu yako ametofautiana na mke wake kiasi kwamba wakatengana na watoto wakakaa upande mmoja tunatakiwa tujitahidi sana wale watoto kuwafanya wajue ukoo hata kutumia ubaba mdogo ama umama mdogo kuwa unawatembelea yaani hata kama dingi ama maza kauzu lakini watoto wataona pamoja na kwamba mzee au mama hatufagilii lakini ndugu zake wako karibu na sie. Support kwa mtoto akiwa mdogo sio fedha hata kumhusisha kwenye shughuli za kifamilia kama sherehe etc unamualika yaani akikua hata kama upeleki matunzo atakuwa karibu na mzazi

Nadhani baba ndio anatakiwa amtafute mtoto na si mtoto anatakiwa amtafute mtoto (tunaita kumkomboa kitu mtoto wakati akiwa mdogo) maana dogo pamoja na dada yake Queen Dareen zamani wakiwa wasanii wachanga walishasema walikuwa wanakwenda kwa baba yao ila bibi yao mzaa baba kama alikuwa anawanyanyapaa
 
Mzee Abdul hapewi nafasi ya kujieleza,,,ila DIAMOND hadi yupo sec alikuwa ANAKWENDA kwa mzee wake,,,,TATIZO mama zetu wana SUMU Kali sn,,especially mtoto akiwa na mafanikio,,,ukikuta mama mwenye CHOYO basi UJUWE baba huna CHAKO..

Sent using Jamii Forums mobile app
Vp napo kwa Queen Doreen napo, manake naye alifikia hatua mpaka ya kumtukana matusi makubwa (mpaka wakawa wanaya mute) kupitia Shilawadu au bado unahisi napo hajapewa nafasi ya kujitetea? Mpaka Queen akatamka mzee si baba yake.

Au Mondi leo hii angekuwa na life bovu unahisi angemtafuta na kumlilia kama amliliavyo leo hii.

Hivi ww mwenyewe hujiulizi mtu mmoja amefanya kosa lile lile kwa watoto wawili aliozaa na wanawake wawili tofauti kwa mda tofauti, huoni huyu mzee ana matatizo na ni kama life style yake ya ujana kuzaa na kutelekeza majukumu yake.

Mimi mwenyewe nakubali kibinaadam na kwa imani yangu huyu mzee anastahili kusamehewa tatizo approach yake yakutumia vyombo vya habari ndio ina muharibia na kumchoresha.

Ukienda page ya tatu comment no 42 ya mjadala huu utaona ushauri nilio utoa na endapo mzee akifuata ushauri huo nina uhakika watayamaliza lkn hivi vyombo vya habari, havitamsaidia kupatana na mwanae zaidi ya kumchoresha.
 
Back
Top Bottom