Ushauri wa bure kwa Askofu Gwajima: Ukivuliwa nguo, ukabaki utupu! Ustaarabu ni kuchutama!

Paskali, duniani chawa ni wengi, hata ukienda shule kwenye somo la OB = Organisatonal Behaviour kuna somo la chawa. Wewe ni chawa msimu usiyekua na aibu. Kwenye ethics kuna dilemma, inategemea sana na lengo. Truth V Loyalty, hapo kuna mgongano. Gwajima kachagua ukweli wewe umechagua Loyalty. Hapo ndiyo tofauti kubwa ilipo.

Ni kweli Gwajima anaweza kudhurika lakini kasema ukweli. That is consequential Conflict
 
Kwenye ishu iliyovuliwa nguo ni Serikali.
kwa hiyo wewe ndugu paschal unapenda jinsi watu wanavyotekwa na wengine kwenda kuuwawa kama mzee kibao wakati serikali ipo na inatumia fedha za umma kulinda watu wake.
ALICHOSEMA GWAJIMA NI KWELI SERIKALI NDIO IMEVULIWA NGUO WALA SIO GWAJIMA.

Ndugu wewe ni mtu mzee kabisa acha kutunga vistori vya uchawa unataka uwe sawa na kina mwijaku?
 
Umeandika Ujinga wa kiwango kikubwa sana. Umeandika kama shambega fulani hivi. Sikutukani wewe ni kaka yangu fani moja ila unatuangusha sana. Hili andiko lako wakisoma familia ya Kibao utapata laana wewe.
 
Mkuu Pascal Mayalla
Sijaona mahali amejibiwa na kuvuliwa nguo! DC wa Ikungi alijaribu, hakufanikiwa kumvua hata kofia
Kumvua nguo abaki utupu lazima ziwepo hoja za ku' debunk' hoja zake mstari hadi mwingine.Sijaziona!

Kama wewe namshauri asiliamshe dude, wanaotaka kumvua wanasubiri alete hoja waifanye 'mada'' na si hoja alizotoa!

JokaKuu
 
Tutakupa tuzo KALAMU YA MAMA..
na PPR sabasaba uhakika
Ahsante kada
 
Nilichoelewa Pasikali anamwelezea sululuu kuwa ni kichaa lkn kiujanjajanja kwakuwa jina analotumia P ni halisi.
Kwamba 'Gwamaji' achutame maana kichaa 'amisa' kamchukulia nguo nakukimbia nazo...
Kwahiyo "wochihandred" sio hazimo-hazimo umeona umwite kichaa kabisaaaa😭😭😭🤣
 
 

P,

Hatakuwa mgombea wa CCM tena hata wakisema sasa ni too late. Huwezi kusubiri mtu ana hoja tofauti ndiyo wamletee mambo ya ahadi kwanini hayajaswmwa mwaka jana! Hayataoata mvuto kwasasa ataenda na upepo wa gwajimalization
 
Kwa hiyo utekaji ni sehemu ya Sera au matarajio ya wananchi wa Kawe
 
Kwako ndugu Mayalla,

Hizi nazo unaziita busara? Unataka wanyonge na wajinga wasemewe na nani. Nani wa kuwatetea?
 
Aliamshe dude, Samia anapaswa kukabiliwa na kila mpenda haki.
 
Hacha ujinga, unatetea mamlaka ya uovu.
 

Kijazi
Asante kwa mawazo yako, inashangaza na inaumiza kwamba bado Watanzania wanaamini kuwa Mbunge anaweza kuleta mabadiliko makubwa jimboni kwake!! Hana kabisa uwezo huo, lakini miaka na miaka unaona wanatoa ahadi, huku tukijua mipango ya Serikali huwa imeaandaliwa, na Budget zake zimeiisha andaliwa.....anyway tuna safari ndefu sana!
 
Mbona kama umetukana mtu, Kwa hiyo Gwajima achutame nguo zake amekimbia nazo kichaa. Kichaa ni aliyemjibu na kumuacha askofu uchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…