PreGE2025 Ushauri wa bure kwa CCM: Tunaelewa Mmechanganyikiwa na Chadema, Ila tumieni fedha zenu kwa akili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Ni ukweli usiopingika kuwa CCM sasa wanaiogopa CHADEMA kuliko hata namna wanavyomwogopa Mungu.

Ukweli huu unatokana na ukweli kuwa, ni dhahili kuwa Watanzania wote sasa hivi wameona na wameelewa kuwa Chama cha Kweli cha Siasa ambacho kipo kwa ajili ya kuwapigania kweli ili kuwapatia maisha bora na maendeleo ya kweli ni Chadema.

Support kubwa wanayozidi kuipata Chadema kila siku kutoka kwa Watanzania kwa kutosaini Kanuni za Uchaguzi pamoja na kutaka Mabadiliko ya Katiba na Sheria za Uchaguzi ili kuwe na Uchaguzi Huru na wa Haki kusema kweli inawatesa sana CCM. Inawanyima usingizi hakika.

Sasaivi ukipita mitaani, ukipita kwenye vijiwe vya kahawa, vijiwe cha wacheza pool table, mitandanoni kuanzia twitter, Facebook, Instagram, Tiktok na kwingineko kote unaona namna Watanzania wanavyotoa maoni bila kupepesa macho kuunga mkono misimamo ya Chadema. Hili linawafanya CCM wawehuke sana.

Kinachonisikitisha ni kwamba, CCM baada ya kuogopeshwa na Chadema na kuchanganyikiwa, wanazidi kutumia hela za watanzania kufanya mambo ya ajabu badala ya kuziridisha hizo fedha Serikalini zikaboreshe barabara mbaya zinazowaathiri Watanzania kila siku.

Kinachonisikitisha ni suala kwamba badala ya CCM kujikita kutumia fedha za Watanzania kwa maendeleo yao ikowemo kuboresha madarasa yaliyochakaa wanayosoma watoto wa kitanzania masikini pamoja na mfumo wa elimu wanatumia fedha hizo kuwahonga mapandikizi waliyonayo huko Chadema kujaribu kuleta mtafaruko Chadema ili kuwakatisha tamaa Watanzania.

Makundi ya G55, Covid 19, Vyombo vya habari kuandika propaganda mfu dhidi ya Chadema na hawa wajinga waliofungua Kesi Mahakama Kuu eti kudai shughuli za Chadema zisitishwe kwa sababu chama kimeitenga Zanzibar ni ushahidi wa uhakika namna CCM wamechanganyikiwa na wanatumia fedha za Watanzania kwa shughuli za kipumbavu za kutengeneza mapandikizi Chadema ili yawanusuru Chama chao kutokana na kukataliwa na Watanzania kwa kiwango cha kutisha.

Nawashauri tu CCM. Watanzania wameona Chama Pekee cha Siasa kinachowapigania kweli ili wawe na maendeleo ya Uhakika ni Chadema, hivyo lolote mtakalofanya dhidi ya CHADEMA hamtafanikiwa.

Poleni sana CCM.
 
CHADEMA si Chama serious tena, hakiinyimi usingizi CCM na vile hakitashiriki uchaguzi mkuu, kutokana na ujinga wa Messiah wenu Tundu AL. Mzee Mbowe angewafikisha mbali kidogo, lakini ndyo hivyo mmemkataa, chama kimeanza cannibalism ya kujimaliza wenyewe, G55 etc
 
Poleni sana. Kubalini tu Watanzania wamewakataa
 
Hakika CCM wamechanganyikiwa

Ulipata urais wa kurithi

2025 unaenda kwenye uchaguzi bila chama kikuu cha upinzani, hani hakuna ushindani, hii ni ai u kubwa sana kwa Samia na historia yake itakua mbaya sana

Muda bado upo warekebishe hili swala, tunajua kwenye urais kwa mfumo tulionao ni ngumu sana mpinzani kutaganzwa hata ameshinda

Ila huku kwenye udiwani na wabunge kinawashinda nini kuweka fair, wapinzani wakipata wabunge 100 CCM mnatakufa?
 
Kama ndani ya chadema kuna mamluki wanaotumiwa na ccm na mnawajua na bado hamjachukua hatua zozote dhid yao, bado mnajiita chama makini?
HAYO MAMLUKI MLIWATAMBUA LINI?
KWA NINI NA NYIE MSIWEKE MAMLUKI NDANI YA CCM ILI WAWAVURUGE? SI MNAJIITA MNA AKILI NYINGI?
yaani hata jumba bovu la cdm mnawaangushia ccm? ama kweli cdm mmefeli ijapo na ccm nao wamefeli huko waliko!
si mnajigamba kuwa nyie ni wa demokrasia, nenden mahakaman msitupgie kelele kwenye keyboard hapa..

YAANI VYAMA VYA KISIASA TANZANIA NI UMAKU TUPU.

SIASA ZA MAKELELE ZILISHAPITWA NA WAKATI.
 
Alikimbia uchaguzi ni nani?

Si mlisema nyie ni Nguvu ya Umma?

Umma si una nguvu?

Kutoka nguvu ya Umma mpaka nguvu ya soda

Chiba atawapoteza punguani nyie
 
Kwa nini upoteze muda kuhangaika na Mamluki wakati wananchi wameshamjua ni mamluki na wameamua kumpuuza?

Wewe umeona kuna sehemu wananchi hata wanawaunga mkono zaidi ya kuwatukana na kuwalaani?
 
Kwa nini upoteze muda kuhangaika na Mamluki wakati wananchi wameshamjua ni mamluki na wameamua kumpuuza?

Wewe umeona kuna sehemu wananchi hata wanawaunga mkono zaidi ya kuwatukana na kuwalaani?
Nguvu ya Umma

Haha jamaa kachukuliwa kama kiroba cha mavi mbele ya Umma wenu feki

Watanzania sio maboya ndg
 
Unaumwa kiseyeye wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…