Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Halafu akimfuta, na hao ACT wakajitenga na hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa, huoni hivyo Visiwa vitarudi tena kwenye ule mkwamo wao wa kisiasa wa miaka nenda?

Mimi naona Serikali ya Tanganyika ingeheshimu maamuzi ya Wazanzibari. Kama wanataka kujitoa kwenye huu Muungano, watoke. Haya mambo ya kuwalazimisha kuwa sehemu ya Muungano, yamepitwa na wakati.
Well said Kamanda sema Pascal anajifanya mjuaji
 
Wanabodi,

Politics is a game like any other games, that people plays, it has its rules and regulations, ukikiuka unaweka pembeni. Yaani mchezo wa siasa pia ni mchezo kama mchezo mwingine wowote, una sheria zake, taratibu na kanuni, ukikiuka, unapewa kadi nyekundu unawekwa pembeni.

P

Huu ni ushauri wako, unayo haki kikatiba kama aliyonayo Othman Masoud na hujaambiwa hata unyamaze. Wacha atumie haki yake ya kikatiba. Anachozungumza ndio ukweli. Hili wewe hulioni kwa sababu ni MLAMBA ASALI.
 
Ni ngumu kufanya kazi na mtu ambaye hamuelewani kwenye mambo muhimu (key fundamental issues).
 
Huyo H.mwinyi pengine ndio kamtuma aanzishe ili wamuunge mkono
 
Siasa za bongo ni utopolo na mleta uzi naye ni kituko tu.
Afutwe kazi kwa kutoa maoni binafsi?
 
Nakubaliana kabisa.

Anti Muungano agents wang'olewe at any cost.

Huyo Othman akayaongee anayo ongea akiwa nje ya serikali.

Jitu linakula heka ya Muunano halafu linaunanga, ni ushamba usiovumilika.
Hebu fanya utulie kidogo. Unaonekana umepaniki ghafla! Huwezi kumlazimisha mtu kuongea vile unavyotaka wewe. Kila mtu ana mdomo wake.

Acha watu waongee bhana.
 
Kaka Paskali, unataka maoni yako ya kumfukuza Bwana Othman yafanyiwe kazi...!! Lakini unataka maoni ya Othman yamfukuzishe kazi..!! Hutendi haki..

Hivi kwanini mtu akitoa maoni yanayokinzana na watawala anatakiwa afanyiwe jambo baya?

Mnataka taifa la NDIYO MZEE? Kwanini hoja zake zisijibiwe kwa hoja zenye nguvu zaidi?

Akikujibu nijuze.
NB-Paskali alikulia kwenye za serikali,Baba yake mzazi alikua ni RSO huko kanda ya ziwa,mama yake pia akiwa mtu wa idara. Niishie hapo
 
Nakubaliana kabisa.

Anti Muungano agents wang'olewe at any cost.

Huyo Othman akayaongee anayo ongea akiwa nje ya serikali.

Jitu linakula heka ya Muunano halafu linaunanga, ni ushamba usiovumilika.
Nchi hii anatakiwa kila MTU awe chawa !! Hii ni kwa usalama wake !! Au ?!
 
Wanabodi,

Politics is a game like any other games, that people plays, it has its rules and regulations, ukikiuka unaweka pembeni. Yaani mchezo wa siasa pia ni mchezo kama mchezo mwingine wowote, una sheria zake, taratibu na kanuni, ukikiuka, unapewa kadi nyekundu unawekwa pembeni.

P
Kwahiyo umamfunga mdimo P 🤔
 
Tangu akiwa AG wa Znz ,Othuman unajukikana msimamo wake binafsi ni upi aligombana na kina shein na kikwete mwisho wakamfuta kazi kwa dhihaka na aibu... lakini bado hakubadilika... Nilishtuka sana siku Kamati kuu ilivyosema Maalim alimpendekeza kuwa mrithi wake,nikajua moto utawaka tu mbeleni
 
Wanabodi,

Politics is a game like any other games, that people plays, it has its rules and regulations, ukikiuka unaweka pembeni. Yaani mchezo wa siasa pia ni mchezo kama mchezo mwingine wowote, una sheria zake, taratibu na kanuni, ukikiuka, unapewa kadi nyekundu unawekwa pembeni.

Serikali ya Zanzibar, ni serikali ya mseto, inaendeshwa na vyama viwili, CCM na ACT, ila watu wa ACT ndani ya GNU wanapaswa kutekeleza sera za CCM.

Serikali ya GNU japo ni serikali ya mseto, lakini inaongozwa na Ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo ACT ndani ya GNU ama wanatakiwa kuhubiri ilani ya uchaguzi ya CCM, na sera za CCM ama wanyamaze kimya, halafu wale ACT wengine nje ya GNU ndio wanaweza kuendelea kupiga siasa za ilani ya ACT!.

Ndani ya Serikali, kuna kitu kinaitwa a collective responsibilities, ukiishakuwa ndani ya serikali, huwezi kusema jambo lolote ambalo ni kinyume cha sera na ilani inayotawala ukabaki salama.

Maalim Seif alipokuwa ndani ya GNU, alinyamaza, hivyo Masoud Othman Masoud ama naye anyamaze, ama atoke nje ndio akaendelee kuhubiri kuuvunja huu muungano wetu adhimu!

Mtu aliyemo ndani ya serikali, hawezi kuyasema maneno kama haya

Kwa maoni yangu, huyu mtu anatakiwa awekwe pembeni, apate muda wa kutosha ajishughulishe na siasa, kwasababu ACT ndani ya GNU wanatakiwa kutekeleza Ilani na sera za CCM!

Ushauri kama huu kumhusu mtu huyu huyu niliwahi kuutoa kule nyuma na ukatekelezwa, Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Hili la kila uchao mtu huyu kuuchokoa muungano hakuanza leo, na hakuna ubaya wowote kuuzungumzia muungano kwa jambo lolote alimradi hilo linalozungumzwa ni liwe la ukweli kuna siku aliongopa kuhusu sovereignity Kuhusu Muungano, Makamo wa Kwanza wa Zanzibar, Adai ni Zanzibar Pekee iliyopoteza Sovereignty, Je Yuko Sahihi?

Hata Mama Samia akiwa VP aliwahi kushauri watu waachwe wa vent kuhusu muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

Kama kuwa huru kuujadili muungano, ni awe huru nje ya GNU and not inside GNU!.

P
Unasukumwa na roho mbaya na kujipendekeza, hakuna jingine.
 
Kaka Pascal wewe ni mtu mzima acha kuingilia ndoa za watu🤣🤣.
What is ACT?
Is a branch of a Revolutionary Party that artificially deals with the GNU!!
Hicho chama Wazanzibar waliingizwa mkenge lakini ukweli juu ya kuanzishwa kwake na chanzo cha fedha,Zitto Kabwe anajua Siri yake🤣🤣🤣
 
Duh !! Kumbeee !! ( ya akina Bwakila ) !!
 
Hakuna muungano, kuna uvamizi. Nyerere alivamia Zanzibar kama Putin alivyovamia Ukraine na mpaka leo majeshi yake yamebaki.
 
Kwani kuwa makamu wa kwanza wa Rais Zenji, inaondoa uanachama wa mtu kutoka chama cha upinzani iwe CUF, ACT nk?
Hapana, haiondoi uanachama, ila viongozi wa ACT walio ndani ya GNU, wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo the best thing to do ni kunyamaza, na ndicho alichofanya Maalim Seif. Huwezi kuwa ndani ya GNU yenye ilani ya CCM inayoamini kwenye kuimarisha muungano halafu wewe unamwaga sumu ya kuvunja muungano!.
P
 
Back
Top Bottom