Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Hakuna anayesikiliza hoja zako wewe Pascal Mayalla . Ikumbukwewe kwamba wewe ndiye uliyemuuza Erick Kabendera kwa JPM . Wewe ni lofa mwenye njaa.
 
Paschal uko sahihi.
Yaani dereva anaendesha gari ghafla kichaa anavamia usukani na kuanza kuelekeza gari porini! hiyo inageuka takataka inatupwa nje!mkimuacha mnakufa wote!

Kule Zenji Rais wao wanamwita Mtalii wa kuja!! Wanaompinga ni millions bila ubabe nchi itamshinda!!
 

Please kasome katiba ya Zanzibar nafasi ya Makamu wa kwanza wa rais ni ceremonial tu, haina Majukumu.
 
Hapa Tanzania hakuna Upinzani Bali ni uharakatitu. Siasa za Upinzani sio uadui wala kumchafua mwenzako ili wewe Ufanikiwe kisiasa.

Mimi niseme kweli kwamba Mzee Maalim Alikua King wa siasa Tanzania. MTU mkweli na Mwuungana kabisa katika siasa za Ushindani wa kisera na kistaarabu, hawa wengine ni wahunitu.
 
Mayala umesoma tena sheria lakini huna akili ya huru kwani lipi baya hapo alilosema, kweni hujui kwa sisi bara tunawatawala wazanzibari huwezi kuwa na muungano wa aina hii baina ya nchi yenye watu 50000000 na nchi yenye watu 1000000 huku ni kumezwa moja kwa moja na hiyo hutuba ya makamo mwenyekiti wa ACT anaitowa kwa wanachama wake, na huyo unaemwambia amfukuze kazi Hana uwezo huo avumilie tu.
 

Ubabe wa nini Kama unakubalika?. Hussein Mwinyi aliwekwa tu pale.
 

Hata Tanzania hatuna serikali Bali iloyopo ni kundi la mafisadi wanaonufaika wao wenyewe.
 
Kama maalim seif alikuwa mstaarabu na hamkumuhishimu basi nyinyi ambao mlimtesa kwa muda mrefu na kumdhihaki mlikuwa washenzi sasa baada ya kufa ndio mnamuona mzuri kwa sababu alivumilia ushenzi na mateso yenu juu yake sisi tunaridhika kabisa kwa jinsi othman anavyofanya kazi zake ndani ya chama na ndani ya serikali.
 
Nakubaliana kabisa.

Anti Muungano agents wang'olewe at any cost.

Huyo Othman akayaongee anayo ongea akiwa nje ya serikali.

Jitu linakula heka ya Muunano halafu linaunanga, ni ushamba usiovumilika.

Mwaka 2022 unataka watu wote tufikiri pamoja? Yani unataka fikra za mwaka 1964 ziishi milele?. Halafu hakuna anti muungano Bali watu wanatoa mawazo mbadala kwa ajili ya kuimarisha muungano.
 
Kwanza katiba inasemaje kuhusu Makamu wa Rais .... je Rais ana huo uwezo? Maana inawezekana akawa na uwezo wa kumteua lakini akawa hana uwezo wa kumuondoa ..... unless atumie ubabe wa CCM kama walivyofanya kwa Ndugai.
 
Diplonasia ikichukua mkondo wake anaweza kufanyakazi bila kumtoa kwani vita unayoijua haileti madhila makubwa
 
Hii nchi uchawa.unalipa
 
Halafu akadhulumiwa haki zake mara.kadhaa
 
Ndo mana alipata kura moja kupitia wajumbe, sasa cjui hio Red card ya siasa uliopewa ww ulifanya kosa gani, Achana na siasa za Znz ,huku tumepitia matukio yote ya kimafia,mfano mapinduzi (1961),Muungano (1964),uchaguzi wa vita na mauaji (2001),uchaguzi wa amani na utulivu,.Je nyie hko bara mmpetia Haya. Pilipili iko shamba yakuwashia nini?
 
Nakubaliana kabisa.

Anti Muungano agents wang'olewe at any cost.

Huyo Othman akayaongee anayo ongea akiwa nje ya serikali.

Jitu linakula heka ya Muunano halafu linaunanga, ni ushamba usiovumilika.
Tatizo kubwa ni kwamba Hussein haijui Zanzibar wala hazijui shida za Zanzibar , alipachikwa tu ili alinde maslahi ya ccm
 
mzee wa kuchongea-kuchongea. ndio unachokimudu hiki, kuchongea wanaume wenzio. hatujasahau ya kabendera.

haya tumeshatuma jina lako na CV yako kwa mama, kesho utapangiwa wilaya ukawe DC.
 
Maoni mbadala ndio yanaendeleza nchi, kumfuta kazi maana yake ni kujidumaza kiakili na matokeo yake ni kudumaza maendeleo ya nchi.
Mkuu denooJ, kwanza naheshimu mawazo yako na
kweli kuwa na mawazo mbadala kwenye jambo lolote ni jambo zuri kwasababu litatoa options, ila mnapoamua kuingia kwenye ndoa, na mkawekeana kanuni ya uwajibikaji wa pamoja na mkakubalia ni ndoa ya mke mmoja mume mmoja, haiwekani mwanandoa mmoja akaanza mahusiano ya nje ya ndoa, huku ni kutaka kuvunja ndoa! huku akimsema vibaya mwenza wake!. Haiwezekani kiongozi ndani ya GNU akazumza hivyo!.
Chama kuwa kwenye serikali ya mseto sio kama mwanamke aliyechumbiwa na mwanaume, still hao walioko kwenye mseto wanatakiwa kuwa huru kimawazo.
Yes kila mtu yuko huru kimawazo unaweza kuwaza lolote lakini sio kusema lolote. Huwezi kusema jambo ambalo litahatarisha ndoa!.
Ninahisi huyo Othman anaweza kushughulikiwa na viongozi wa chama chake, kwasababu wenzie wote sasa ni walamba asali.
No hawezi kushungulikiwa na chama chake kwasababu huyu ndie mgombea wao wa urais 2025
Wakati mwingine huwa najiuliza hivi mkiwa mnahubiri demokrasia huwa mnakuwa mmelewa au? kwasababu najua nyie ni madikteta, na wewe ni mfano mmojawapo wa madikteta tulionao, unapenda vya kukufurahisha machoni pako pekee.
Hapana, mimi sio Dikiteta na kwa wanaonifahamu kwa karibu, mimi ndie Mwandishi pekee niliye mkabili JPM kuhusu udikiteta.

Licha ya mimi kuwa ni kada mtiifu na mwaminifu wa CCM, lakini kwenye hili la democrasia ninatanguliza maslahi ya Taifa.
Mfano ni huu Rais Magufuli, somo la managing diversity kwa Serikali yako linahitajika
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…