Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Juzi juzi Kiongozi wa huko visiwani imebidi atolee maelezo/ ufafanuzi tuhuma za yule Mzee wa chama aliyepigwa kidogo auwawe.

Kama sio hizo kelele za huyo Mzee wananchi wangejuaje mambo ya kandarasi, viwanja na tuhuma zingine alizozisema?
 
Tatizo GNU yenyewe Ni mkataba wa kimaslahi binafsi. Ni mpango wa CCM kuendelea kuungata upinzani au fikra pinzani kwa style ya panya "kungata na kupuliza".

Gnu haijibu hoja na haja za wazanzibari, Ni mpango tu wa political giant-figures kupeana ulaji.


Mpinzani wa kweli hawezi kuamini katika mfumo huu wa GNU usio address true grievances za watu bali kugawana madaraka viongozi.
 
Ingalikuwa kipindi cha Mwalimu Nyerere huyu bwana angalipata tabu Sana kwa kosa kubwa la kuvunja muungano ulio jengwa kwa gharama kubwa!
 
Naunga mkono hoja, OMO ni mnafiki kwanza shavu zake zimejaa kuonesha karidhika ila kuna kitu anataka zaidi. Badala ya kuongelea issue za maendeleo yeye anataka kulete fujo.
 
Kwani kuwa makamu wa kwanza wa Rais Zenji, inaondoa uanachama wa mtu kutoka chama cha upinzani iwe CUF, ACT nk?

Walipokubali kuwaunganisha wapinzani walitakiwa kuwa na makubaliano kuhusu watakavotawala na hayo yalitakiwa kuwa na msingi ktk katiba na sheria zao iloruhusu kuwepo kwao. Kama kitu hicho hakipo, ni balaa nyngne. Unakuwa mpinzan unapotofautiana chama tawala. Kuingizwa madarakani haikumanisha umeacha upinzan na ikiwa katiba au sheria zao zinalazmisha hayo, ndo mapungufu yenyewe. Iltakiwe pawepo hicho kipengere ktachotatua masuala yenye utata ktk utawala wa nchi. Suala la collective responsibility ni pale tu mnapokua timu moja na ktokana na ktofautiana kimawazo concensus inapatkana kw kura. Lkn pia inajulkana kuwa sio kila wkt majority wako right ndo sbb ktk masuala makuu kuna knachoitwa minority opinion. Wajue kuwa wapinzani wapo kw sbb hawakuridhika na hizo sera za CCM. Hayo mambo ya collective responsibility ni huku kwetu, otherwise hiyo Ktb itawaletea mattzo, ipitiwe upya
 
Huu ni uchawa,mbna Ruto anampinga Kenyatta ktk baadhi ya mambo???hii nchi itachelewa sana kuendelea
 
Wale hawataki kujitenga, wanataka cha zaidi. Sisi Watanganyika, ajira za Muungano ndio hizo hizo za Tanganyika, Ardhi ya Muungano ndio hiyo hiyo ya Tanganyika. Wao wana ardhi ya Zanzibar na ardhi ya Tanganyika. Wao kuna ajira za Muungano na Ajira za Zanzibar. Sisi siasa za Muungano ndio hizo hizo za Tanganyika. Wao wana siasa(uongozi na manufaa yake yote) za Zanzibar na za Muungano.
 
Hv mwanamke kama hakutaki kwann ulazimishe penzi?????
 
Nakubaliana kabisa.

Anti Muungano agents wang'olewe at any cost.

Huyo Othman akayaongee anayo ongea akiwa nje ya serikali.

Jitu linakula heka ya Muunano halafu linaunanga, ni ushamba usiovumilika.
Mada ingekuwa Othman ajiuzulu au atakiwe kujiuzulu (kauli ya kumfukuza au kumfuta kazi haina staha and is not politically correct). Huwezi kuwa tofauti na msimamo mkubwa wa serikali katika suala zito kama la muungano halafu ukaendelea kuitumikia serikali hiyo hiyo.

Uhuru wa kuongea anao; hawezi kunyang’anywa. Lakini haikubaliki kuupinga muungano huu jinsi ulivyo ukiwa ndani ya ajira ya serikali ya CCM. Kwanza, mantiki ya kawaida kabisa inadai asingekubali nafasi hiyo ya kazi kabla ya kutoa sharti la marekebisho ya muungano kuwa ajenda muhimu ya SMZ.

Kibatala alipoulizwa kama akiteuliwa kuwa AG atakubali? Alijibu itabidi kwanza marekebisho makubwa yafanyike katika mfumo mzima wa eneo hilo ndipo akubali. Nje ya hapo ni out of question.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…