Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Acheni Akili mfu ninyi vibwetele kwani hakuna Watanzania wanao ishi Marekani Uingereza Ujerumani na kwingineko wameoa, kuolewa na wanafanya kazi na biashara zao? Kwani hizo nchi zote tumeungana nazo kuwa Tanganyika?
 
Nakubaliana kabisa.

Anti Muungano agents wang'olewe at any cost.

Huyo Othman akayaongee anayo ongea akiwa nje ya serikali.

Jitu linakula heka ya Muunano halafu linaunanga, ni ushamba usiovumilika.
Muungano gani, ukoloni huo mnazani wazanzibar wote ni mazwazwa?
 
Naunga mkono hoja, OMO ni mnafiki kwanza shavu zake zimejaa kuonesha karidhika ila kuna kitu anataka zaidi. Badala ya kuongelea issue za maendeleo yeye anataka kulete fujo.
Mtu anaesema lililopo moyoni mwake consistently huwezi kamwe kumuita mnafiki.
 
Mbona zipo nchi nyingi tu duniani zinaendeshwa na serikali za mseto ? Kwani huwa wanafanyaje katika kutoa maoni yao Hao waliomo kwenye huo mseto ??!!
Huwa kwanza kabisa wanajadiliana na kukubaliana mambo ya msingi. Ilitakiwa ACT na CCM waelewane mapema kabisa kuhusu muungano kabla ya kuunda serikali ya pamoja. Othman has missed the fundamental point of coalitions.

Hii ya Zenj ilikuwa ya maslahi binafsi ya mtu mmoja na kundi lake. Sasa bahati mbaya kavamia asiye na compromise kama mtangulizi wake. Naamini yuko out of step hata na mwenye chama.
 
Kwanza, kama kawaida ya wanaCCM huelewi uhusiano mzito wa siasa na harakati. Upinzani hauwezi kuwa na impact bila dozi ya harakati. Na ukisikia upinzani usidhani ni CHADEMA au ACT pekee. Hata ndani ya CCM. Ile sarakasi iliyopigwa bungeni hivi majuzi kudai pesa ya mradi wa barabara haikuwa ya mchiriku.

Pili, hiyo uliyompa Maalim Seif sio sifa ni dharau. Unamsifu kiongozi wa upinzani kwa ku-compromise? Unataka vyama pinzani vya kuabudu watawala kama ilivyo Urusi au Rwanda? That’s a completely twisted mindset. Tukuza CCM unavyopenda lakini weka maandishi yenye mantiki na kufikirisha watu wenye akili hapa JF.
 
Paskali bwana, kama unaona Othman kakosea basi ishia hapo hapo. Mambo ya kupendekeza atenguliwe siyo jukumu lako.
 
Lakini huu mseto haupo kama fadhila Bali ni takwa la kikatiba katika katiba ya Zanzibar ! Sasa swali la kujiuliza je vitu ulivyovieleza havikuainishwa katika hiyo katiba !! Au ndio contradictions zenyewe hizo ?!!
 
Dogo wewe huelewi bado mtoto..kua uyaone mwanawane..hujui maana ya kujenga chuki na uhasama kama huu watu wanaotaka kujenga.. kakojoe ulale jomba
Nani ataanza kujenga chuki?,Watanganyika au Wazanzibari..

Chuki zilijengwa baina ya Wahutu na Watutsi na zimetulia,Chuki alijenga Hitler baina ya Wayahudi Wazungu na zimetulia

Hatu hizo chuki zitakazojengwa Baina Watanganyika na Wazanzibari zitatulia tu..

Zanzibar lazima iwe na mamlaka yake,ili iendeleze utamaduni,mila,dini na ustaarabu wake

Mnataka kulazimisha Muungano kwa vitisho sasa,kumbukeni kabla ya Mungano kulikuwepo na Zanzibar,na itaendekea kuwepo..
 
Viongoizi waadilifu? wakati ccm hakuna kiongozi mwadilifu.

Muadilifu anakemea matendo maovu na sio kuficha maovu. Ni nani ccm anaekemea maovu yanayotendeka juu ya raia?

Mnakemea yakiwasibu nyinyi tu huko lumunba.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi,
Mwanasheria huyu Mkuu wa Zanzibar, hebu msikilize hapa!.

Kamati ya Maridhiano Six:MWANASHERIA OTHMAN MASOUD AUCHAMBUA MUUNGANO NA KATIBA MPYA
Paskali
OMO ndie mgombea urais wa Zanzibar 2025 kupitia tiketi ya ACT, kwa hoja kama hizi, hiki kikiwa ndicho Zanzibar wakitakacho, nimeshauri na naendelea kushauri kuundwa tume ya maridhiano Zanzibar kabla ya uchaguzi ili huyu jamaa akishinda atangazwe, lakini isipoundwa, ikatokea huyu jamaa ndie kashinda, itabidi tufunike tena kombe kama 2015 maana JMT haiwezi kukubali watu ma radical kama huyu kukabidhiwa nchi, akikabidhiwa leo, kesho yake tuu atauvunja huu wetu adhimu na adimu!
Ushauri wangu ni huu
Mwenzenu mimi nina jicho la tatu, 2015 nilishauri Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein hawakusikia, kilichokuja kutokea ni hiki Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

Sasa kwa 2025 nimeelezwa HII kitu!
P
 
Mambo ya wazanzibar waachieni wenyewe wazanzibar watanganyika hamtaki kuona Zanzibar iliyo salama mnafurahia migogoro Ili muendelee kututawala
Pascal wewe si mzanzibar Kwa mujibu ya katiba yetu shughulikiia yanakuhusu yetu tuwachie wenyewe
 
Mambo ya wazanzibar waachieni wenyewe wazanzibar watanganyika hamtaki kuona Zanzibar iliyo salama mnafurahia migogoro Ili muendelee kututawala
Pascal wewe si mzanzibar Kwa mujibu ya katiba yetu shughulikiia yanakuhusu yetu tuwachie wenyewe
Mkuu dega , mimi ni mtanzania mzalendo muumini wa nchi moja ya JMT ambapo Zanzibar ni sehemu yetu, hivyo Zanzibar inanihusu sana, tena kama uko Zanzibar, tarehe 28 January hii njoo Zanzibar Serena, nikutambulishe shemeji yako, mfahamiane uheshimiane kwa kuoleana!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…