Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza timu yetu ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Uganda. Hakika ushindi wa leo, umefufua matumaini ya kufuzu AFCON kwa mara nyingine tena.
Nije sasa kwa mchezaji Feisal Salum (Fei Toto). Kwanza nampongeza kuitwa kwenye timu ya Taifa, huku akiwa hata hajulikani alipo kwa takribani miezi 3 sasa, kwa kweli anatakiwa ajione kama mtu aliyepewa heshima kubwa ambayo hata hakustahili!
Maana kuna wenzake wengi tu wameachwa huku wakiwa wamefanya vizuri kwenye vilabu vyao, tofauti na yeye ambaye mpaka sasa klabu yake ya Yanga inamtambua kama mchezaji mtoro!
Ushauri wangu kwake nikiwa kama mdau wa michezo, mara tu baada ya hiyo mechi ya marudio kumalizika; namshauri aitishe mkutano na vyombo vya habari. Halafu ajitokeze hadharani kuomba radhi kwa klabu yake ya Yanga, wanachama, mashabiki, na wadau wote wa mpira wa miguu kwa sintofahamu iliyojotokeza, ili maisha yaendelee.
Kama msamaha ukipokelewa, arudi kwenye kikosi, na kucheza kwa bidii mpaka mkataba wake utakapokwisha hapo mwakani na kama ataona kuna umuhimu wa kuongeza, ataongeza, kama ataona anahijitaji changamoto mpya, basi ataondoka kwa heshima kama free agent.
Angalizo; Iwapo hiyo mechi ya marudio itapita, halafu dogo atapotelea tena mafichoni, basi nitamuona kama ni kijana ambaye siyo muungwana, mkaidi, na asiye na busara, na nitashangaa sana kama TFF watamuita kwa mara nyingine tena mchezaji asiye na timu, asiyejitambua, na aliyekosa nidhamu kama Fei Toto.
Huyu mtoto anatakiwa kutambua ya kwamba, maisha yake kwa sasa yanategemea mpira. Hivyo kama mpira kwa upande wake ni kazi, basi anatakiwa pia auheshimu, na aweke pembeni mahaba yake na timu nyingine.
Ajifunze kwa maelfu ya wafanyakazi nchini na duniani kwa ujumla, ambao wanafanya kazi mbalimbali kwa moyo huku baadhi yao wakiwa hawana hata mahaba na hizo kazi. Maana kinacho angaliwa ni ule mshahara ambao mfanyakazi akiupata, anautumia kwenye mahitaji yake ya kila siku na wala siyo mahaba na hiyo kazi.