Ushauri wa bure kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso, acha kulialia! Chukua mawili matatu kutoka katika nondo hizi

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Mie hapa New York pana kaubaridi (nyuzi joto kama 6 hivi si haba) na nimekula pilau ya Xmas ambayo kapika shemeji /wifi yenu alifundishwa na mama mkwe wake kupika pilau ya maana. Wakati huohuo nimeweka ile muziki ya Bongo Classics nakula muziki taratibu kushusha msosi.

Lakini hapohapo nafikiria maisha ya wale watanzania ambao hawana maji safi na salama hii yasikitisha sana khasa ukimwambia mzungu eti Tanzania yenye miaka 64 ya huru ina shida ya maji!! Hapohapo wamwambia kwamba yapo maeneo yana maji kama kawaida (diverted water) na hawana shida kabisa).

Juzi nimemuona waziri wa maji Jumaa Aweso akihojiwa na Salim Kikeke na akashindwa kujibu suali lihusulo tatizo la maji kushindikana kutatuliwa ndani ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika. Lakini cha kushangaza pia ni kwamba waziri Uweso yupo kwenye wizara hiyo miaka mingi tangu ateuliwe mara ya kwanza na bado atakuwepo hapo kwa miaka mingine mitano (kama serikali yake bado itakuwepo kabla ya 2030).

Lakini pia nikafikiria nijaribu na mie kujiweka kwenye nafasi ya uwaziri wa maji je nitaweka mikakati ipi ya kuhakikisha kero ya maji yaondolewa Tanzania. Kwanza nirekebishe wale watu ambao hupenda kutumia neno Kero badala ya Shida ya Maji. Tatizo lililopo ni kwamba maji hayapatikani na hiyo imegeuka kuwa ni shida ya maji. Kero ni vile vilio na kelele za mahitaji ya maji hayo kutoka kwa wananchi. Hivyo waziri na serikali ijirekebishe moja kwa moja kutotumia neno Kero kwani neno hili lamaanisha kwamba serikali yaona kelele za wananchi ni Kero na kwamba ni pale tu itakapoamua ni lini itatue tatizo la maji itafanya hivyo.

Suala la maji si hisani kama serikali inavyofikiria kwamba yatoa huduma ya maji kwa wananchi wake kama hisani bali ni jukumu lake pamoja na barabara, umeme, hospitali, zahanati na elimu. Haya ni majukumu ya serikali yoyote ile ambayo imepewa ridhaa na wananchi iwangoze. Tatizo hapa kwa sasa tuna serikali ambayo haijapewa ridhaa (Mandate) na wananchi ikae madarakani, ingekuwa hivyo basi raisi angeapishwa rasmi mbele ya wananchi wote wa Tanganyika na akaungwa mkono na wananchi wote na kila mtu akawa na furaha kwamba tumepata raisi ambae akubalika na wananchi wote.

Sasa tuje kwenye tatizo la maji ambalo ndo msingi wa mada hii.

Ningeweza kuzungumzia tatizo la maji kwa nchi nzima lakini kwa leo tuangalie matatizo ya maji kwa mji wa Dar-es-Salaam kwa ujumla.

Matatizo ni kama yafuatavyo:

1. Upungufu na mgao wa maji.

2. Uwiano uso sawa wa upatikanaji wa maji.

3. Miundombinu ilochakaa na kuharibika bila kufanyiwa "Upgrade".

4. Kasi ya ukuaji wa idadi ya watu ambayo yazidi mifumo ya usambazaji maji.

5. Ukuaji wa sekta iso rasmi ya soko la maji.

Mji wa Dar-es-salaam hauna maji ya kutosha kwa wananchi jambo lilopelekea maji iwe ni shida kubwa kiasi cha maji hayo kuuzwa kwenye matenki na mapipa ya ukubwa mbalimbali. Lakini twasahau pia kwamba suala kama hili la maji ni lazima serikali iwashirikishe wadau kadha wa kadha, wananchi , kutengeneza stratejia na pia kutengeneza kanuni au framework ambayo ni lazima itumike na nchi nzima katika usambaza maji nchi nzima kiusawa, kiufanisi na kiuhimilivu.

Kiasi gani cha maji kilichopo ni suali la kwanza kabisa kabla ya yote kufahamu kwamba na hii ni kabla ya kuanza kusambaza maji, je kuna mito mingapi, maziwa, mifereji, vituo vya kusafisha maji na hifadhi ya maji (reservoirs). Hili la hifadhi ya maji ndilo muhimu zaidi kwani hizi hifadhi zatakiwa ziwe katika maeneo ambayo watu watapata maji safi na salama na ya uhakika.

Pili, ni kutambua ni kiasi kipi cha maji chatumika kwenye kilimo, viwandani, mahotelini na kwenye migahawa na majumbani. Ukigundua kuwa ni wapi maji yatumika sana au yamwagika basi utaweka njia sahihi ya kuvuna maji hayo ili yale yalo safi yaweze kurudi kwenye mfumo uliopo na yale yasotakiwa yaende kama maji taka. Pia sehemu hizi zikifungwa mita sahihi na zenye kuweza kutoa data za uhakika za matumizi sahihi ya maji, hiyo pia itasaidia kuweka kubaini wapi penye kasoro na pahitaji marekebisho.

Tatu, ni kubaini wapi kuna uhaba na wapi kuna uwingi na ziada ya maji. Hii yaendana na kuweka mita zitazosoma matumizi ya maji hayo na pia itawezesha kujengwa kwa njia maalum za kuweza kukinga maji hayo ili yaelekezwe katika hifadhi zilizopo.

Sasa katika mambo hayo matatu hapo juu bado siamini kama ni kweli hakuna taarifa zozote zilochapishwa na wataalam wa maji zinohusu hayo mambo au ndo wameandika na wizara imepuuza. Hiyo pia yanikumbusha yule mwananchi ambae alikuwa ni wa darasa la saba ambae alimuambia hayati JPM kwamba alipotoa ushauri wake kwa wizara ya maji akaishia kuulizwa CV yake ni ushauri wake ukapuuzwa, kwanini sie waafrika twazidi kuwa wapumbavu kiasi hiki miaka 64 baada ya huru twapigizana kelele kuhusu kero ya maji?

Wenzetu UAE na Kuwait ingawa wapo jangwani lakini wananchi wake wapata maji safi na salama na hii yatokana na viongozi wao kuwa na vitu viwili muhimu wanapofikiri, ubunifu na maono. Bila hivi vitu viwili watanganyika hatutafika kokote na kama serikali yenyewe haina nia ya kufikiria ubunifu na kuwa na maono, tusema tuwe na Maji Strategy 2040 nchi nzima, basi tumekwisha.

Tukiangalia katika nchi kunakuwepo mifumo mikubwa mitatu ya usambazaji maji ambayo yahusisha madaraja matatu, yaani kuna mitambo mikubwa ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, njia za usambazaji na hifadhi, mabomba makubwa ambayo yasambaza maji kutoa sehemu zenye maji ya ziada na kuyapeleka sehemu zenye uhitaji, na kwa miji ya Pwani kama Dar-es-Salaam au Bagamoyo kuna mitambo ya kuzalisha maji safi na salama yanotokana na maji ya baharini.

Kama watanganyika huru tangia mwaka 1964 kweli tumeshindwa kujenga mitambo ya kusafisha maji ya chumvi (desalination Plants) kuwa maji safi na salalam ili kutumiwa majumbani? Wizara ya maji ingeweza kabisa kujenga mitambo hii katika pwani ya mji wa Dar-Es-Salaam na mji wa Bagamoyo na hata Kigamboni. Hivyo watu wa Bagamoyo, Dar-es-Salaam na Kigamboni wangetumia maji yanotokana na mitambo hiyo. Kazi ya kujenga mitambo hii wangepea wakandarasi ambao watokea kwenye nchi zilojenga mifumo hii ikiwemo Israeli, UAE na Kuwait. Pia katika chuo cha maji ingewekwa kozi maalum kwa wanafunzi ambao wangejifunza namna ya kujenga vituo na mitambo hii ya Desalination.

Pia ipo mitandao ya maji katika kila mkoa yaani kwa mji wa Dar-es-Salaam DAWASA inakuwa na mitambo yake ambayo ni lazima ibadilishwe ili iwe ya kisasa na iweze kuendana na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu. Mabomba yapo na pia matenki yapo ya kuhifadhia maji. Shida iliyopo ni kutokuwepo mifumo ya kisasa ya kusoma matumizi ya maji hayo. Ni lazima pawepo mitambo ya kusoma matumizi ya maji ya ubora wake pia ili kweza kubaini mchakato wowote wa kuvuruga vyanzo na hifadhi za maji hayo. Hii pia yaendana na dhana kwamba maji mengi yameelekezwa katika baadhi ya sehemu zenye makazi ya watu fulani tu kwa upendeleo badala ya kuwa katika stratejia ya maji nchini.

Vituo vidogo vya usambazaji maji navyo ni tatizo kubwa kwani kwani mafundi maji huamua ni wakati gani waruhusu maji yatoke na ni wakati upi wazuie maji hayo na siku zote wana spana mkononi tiyari kupokea fedha za kuuza maji. Vituo hivi vidogo vya usambazaji maji ni lazima viwe na ulinzi wa masaa 24, viwe na mitambo ya kubaini wapi maji yavuja na wapi maji yamezuiwa, kuwepo na mita za kisasa na pia kuwepo na bomba moja kubwa kwa ajili ya kusaidia wananchi ambao watahitaji maji nyakati za kiangazi au uhaba mkubwa unotokana na matatizo kutokea Ruvu Juu au Ruvu Chini.

Ni kweli kwamba kiangazi na ongezeko la watu ni baadhi ya changamoto zilizopo lakini bado serikali ni lazima iweke stratejia ya Maji kwa mkoa wa Dar-es-Salaam.

Zipi ni stratejia za kuhakikisha mji wa Dar-es-Salaam hauna shida ya maji kufikia 2030?

1. Kutengeneza ramani ionyeshayo usambazaji wa maji katika mji wa Dar-es-Salaam unoanzia kwenye mitambo ya Ruvu Juu au Ruvu Chini.
Ramani hii itasaidia kuonyesha sehemu zenye maji ya kutosha, wapi kuna uhaba na pia namna ya kusambaza maji zaidi kwenda kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi. Njia hii itaenda sambamba na kubaini sehemu zenye maji chini ya ardhi na kwamba endapo mtu agundua sehemu aliyopo amechimba na pana maji ni lazima aifahamishe wizara ya maji ili sehemu hiyo iwe ni nyaraka ya serikali kwa ajili ya kuelekeza maji hayo kwenda kwneye hifadhi.

2. Kujenga mitambo ya kusafisha maji ya chumvi kuwa maji safi na salama kwa matumizi ya majumbani, mahotelini na kwenye migahawa.

Kama nilivyosema hapo juu nchi za UAE na Kuwait au Israeli wana utaalam huu, hivyo ni jambo zuri tuwazungumze ili watusaidie watatuona tuna akili na twajitambua na msaada utatoka kama umeme. Na hii isiwe Dar-es-Salaam pekee bali katika mikoa yote ya Pwani kwetu Tanga na Mtwara. Sambamba na hili, pia kujengwe hifadhi za kistratejia (strategic reservoirs) ambazo zitakusanya maji nyakati za mvua. Sambamba na hili pia kuingizwa kozi maalum kwa ajili ya kufundisha wanafunzi wa chuo cha maji njia mpya za kuboresha usambazaji na usimamizi wa wa maji mijini.

4. Kuimarisha mitambo iliyopo.

DAWASA yatakiwa kuimarisha mitambo yake ya usambazaji maji (upgrading) kwa kuwekeza katika njia bora na za kisasa, kuwekeza katika mitambo mipya na kisasa ya kuchakata maji taka, kuweka mita za kisasa (smart metering) ili kuzuia na kudhibiti wizi wa maji na uunganishaji kiholela, kuwekeza kwenye teknolojia ya kubaini kuvuja kwa maji (Water Leaks) na pia kuwekeza kwenye mitambo ya kuchakata maji kupata yale yatayotuika kwenye viwanda na shughuli za kilimo.

5. Kusaidia kupatikana maji katika sehemu zenye matatizo ya miinuko au vijijini.

Hii ni pamoja na kutoa elimu na kuziwezesha shule, vituo vya afya na majumbani kutega na kuhifadhi maji katika hifadhi maalum nyakati za mvua, vijiji na tarafa kuwa na sehemu maalum ya kuteka maji wa ajili ya kijiji, kuweka mitambo ya kuchimba maji (boreholes) inotumia umeme wa jua ambayo itamilikiwa na DAWASA na ambayo ni rahisi kuiendesha, na haina gharama sana.

6. Kuunda timu za mafundi kufanya kazi masaa 24.

Timu hizi za mafundi maji zitakuwa na jukumu la k uhakikisha kunafanyika matengenezo yoyote yanohitajika masaa 24 (repair and maintenance), kutambua matobo na kuvuja kwa maji khasa kutoka kwenye mabomba makubwa, na ni lazima DAWASA iwe na namba ya simu (maalum hotline) kwa wananchi kutoa taarifa ya kuvuja kwa maji na pia DAWASA hiyohiyo iwe na namba ya WhatsApp ambayo wananchi pia wataitumia kutuma taariza za vitenfo vyovyote vya hujuma kwa njia za maji na wizi pia.

7. Kuunda mfumo wa kuondoa soko lisilo rasmi la maji.

Soko lisilo rasmi la maji limekuwa ni tatizo kubwa kwani ujasusi waweza kubaini kuwa maji mengi yanouzwa mabarabarani huenda yatokea katika vyanzo vya maji ambayo ni mali ya DAWASA. Hivyo ili kukabiliana na tatizo hili ambalo lasababisha ukosefu wa mapato yaani (Non Revenue Water) ni kufunga mita za kisasa katika majengo yote marefu, majengo ya makazi (flats/ estates) majengo ya kiofisi, viwandani na maghalani na ipitishwe sheria kwamba ni kosa la jinai kuigusa mita ya DAWASA na kwamba mtu yoyote ataechakachua mita hizi atafikishwa mahakamani.

8. Utawala, Taasisi na Taarifa au Data.

DAWASA lazima iwekewe malengo yaani "targets" kwamba ndani ya miaka miwili kwa mfano, kuwe kumejengwa "desalination Plants" na ziwe up and running. Kupunguza NRW na pia kuhakikisha kila mwaka kuna muunganisho mpya wa maji. Hii itaenda sambamba na waziri wa maji kuhakikisha chombo kinosimamia DAWASA au regulator chatoa taarifa ya ufanisi wa DAWASA kila baada ya miezi mitatu. Pia kuhakikisha kunakuwepo mipango maalum ya ufanisi na udhibiti wa vifaa na mali ya DAWASA pamoja na huduma bora kwa wateja.

9. Kufunguka kwa kutoa Data na kuwashirikisha wananchi.

Pamoja na kwamba wizara ya maji ina tovuti lakini bado taarifa sahihi hazionekani katika tovuti hiyo. Ni lazima katika tovuti hiyo kuwepo na ubao (dashboard) ambayo yaelezea kila kanda na usambazaji maji, uhaba unotarajiwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mpya ya njia za maji. Pia kuwepo na sehemu ya maoni au feedback kutoka kwa wananchi ambao watakuwa huru kutuma ujumbe mfupi, katika mtandao wa WhatsApp na pia kuweka vituo maalum (wards) kwa kila ofisa wa maji wa wilaya kuzungumza na wananchi ili waeleze shida zao na zionekane hatua zilochukuliwa kukabiliana na shida hizo.

10. Kuunda mashirikiano na sekta binafsi, na taasisi zisizo za serikali. Hizi zitaisaidia wizara kuwa na wigo mpana wa msaada ambapo kwenye masuala kama namna ya kupata mitambo ya kuchuja maji ya mvua (desalination plants), namna ya kuuondoa tatizo kama la NRW na pia kusaidiwa kupata mita za kisasa (smart metering).

Mwisho, Tanganyika ina miaka 64 ya Uhuru ni miaka ya mtu mzima aliestaafu na yuko kijijini Korogwe. Waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha maji yapatikana nchi nzima una wajibu wa kufanya hivyo, hakikisha maji yapatikana nchi nzima kwa kuanza na mji wa Dar-es-Salaam na ifike wakati nchi nzima maji iwe ni historia.

Nimekupa nondo hizi chukua unoziona zafaa zifanyie kazi.

Bado zipo nyingi lakini hizi zakufaa wa sasa.
 
Ukiwa nchi za watu ndo utajua Tanzania bado sana
Nipo nchi mojawapo ya southern asia huku toka nije ni takribani miezi minne ila sijawahi kuona maji yakatike bombani wala umeme hata siku moja.kwa kweli tuna kazi sana ya kufanya vyanzo tunavyo sijui tatizo linakuwa ni nini?
 
Ukiwa nchi za watu ndo utajua kwa kweli tuna kazi sana ya kufanya vyanzo tunavyo sijui tatizo linakuwa ni nini?
Nepotism.. ajira kujuana unaajiri watoto wa dada zako na shemeji zako na watu km hao unategemea kutakua na ufanisi kwenye utendaji? Aweso ilibidi apigwe chini apewe mwingine mwenye uwezo zaidi... hivi hakuna wanaoweza kufanya zaidi yake? Kwanini wasipewe waendeleze alipoishia?
 
Bila kuwa na katiba MPYA ya wananchi itakayowadhibiti wanasiasa mchwa wa CCM wanaotafuna kwa kufuru za kodi wananchi hatutoboi.
 
Attachments

  • VID-20251226-WA0005.mp4
    10.4 MB
We si Una pingu za jela wewe?umeiba simu wapi leo kupost utumbo huo.
 
Mie hapa New York pana kaubaridi (nyuzi joto kama 6 hivi si haba) na nimekula pilau ya Xmas ambayo kapika shemeji /wifi yenu alifundishwa na mama mkwe wake kupika pilau ya maana. Wakati huohuo nimeweka ile muziki ya Bongo Classics nakula muziki taratibu kushusha msosi.

Lakini hapohapo nafikiria maisha ya wale watanzania ambao hawana maji safi na salama hii yasikitisha sana khasa ukimwambia mzungu eti Tanzania yenye miaka 64 ya huru ina shida ya maji!! Hapohapo wamwambia kwamba yapo maeneo yana maji kama kawaida (diverted water) na hawana shida kabisa).

Juzi nimemuona waziri wa maji Jumaa Aweso akihojiwa na Salim Kikeke na akashindwa kujibu suali lihusulo tatizo la maji kushindikana kutatuliwa ndani ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika. Lakini cha kushangaza pia ni kwamba waziri Uweso yupo kwenye wizara hiyo miaka mingi tangu ateuliwe mara ya kwanza na bado atakuwepo hapo kwa miaka mingine mitano (kama serikali yake bado itakuwepo kabla ya 2030).

Lakini pia nikafikiria nijaribu na mie kujiweka kwenye nafasi ya uwaziri wa maji je nitaweka mikakati ipi ya kuhakikisha kero ya maji yaondolewa Tanzania. Kwanza nirekebishe wale watu ambao hupenda kutumia neno Kero badala ya Shida ya Maji. Tatizo lililipo ni kwamba maji hayapatikani na hiyo imegeuka kuwa ni shida ya maji. Kero ni vile vilio na kelele za mahitaji ya maji hayo kutoka kwa wananchi. Hivyo waziri na serikali ijirekebishe moja kwa moja kutotumia neno Kero kwani neno hili lamaanisha kwamba serikali yaona kelele za wananchi ni Kero na kwamba itakapoamua ni lini itatue tatizo la maji itafanya hivyo.

Suala la maji si hisani kama serikali inavyofikiria kwamba yatoa huduma ya maji kwa wananchi wake kama hisani bali ni jukumu lake pamoja na barabara, umeme, hospitali, zahanati na elimu. Haya ni majukumu ya serikali yoyote ile ambayo imepewa ridhaa na wananchi iwangoze. Tatizo hapa kwa sasa tuna serikali ambayo haijapewa ridhaa (Mandate) na wananchi ikae madarakani, ingekuwa hivyo basi raisi angeapishwa rasmi mbele ya wananchi wote wa Tanganyika na akaungwa mkono na wananchi wote na kila mtu akawa na furaha kwamba tumepata raisi ambae akubalika na wananchi wote.

Sasa tuje kwenye tatizo la maji ambalo ndo msingi wa mada hii.

Ningeweza kuzungumzia tatizo la maji kwa nchi nzima lakini kwa leo tuangalie matatizo ya maji kwa mji wa Dar-es-Salaam kwa ujumla.

Matatizo ni kama yafuatavyo:

1. Upungufu na mgao wa maji.

2. Uwiano uso sawa wa upatikanaji wa maji.

3. Miundombinu ilochakaa na kuharibika bila kufanyiwa "Upgrade".

4. Kasi ya ukuaji wa idadi ya watu ambayo yazidi mifumo ya usambazaji maji.

5. Ukuaji wa sekta iso rasmi ya soko la maji.

Mji wa Dar-es-salaam hauna maji ya kutosha kwa wananchi jambo lilopelekea maji iwe ni shida kubwa kiasi cha maji hayo kuuzwa kwenye matenki na mapipa ya ukubwa mbalimbali. Lakini twasahau pia kwamba suala kama hili la maji ni lazima serikali iwashirikishe wadau kadha wa kadha, wananchi , kutengeneza stratejia na pia kutengeneza kanuni au framework ambayo ni lazima itumike na nchi nzima katika usambaza maji nchi nzima kiusawa, kiufanisi na kiuhimilivu.

Kiasi gani cha maji kilichopo ni suali la kwanza kabisa kabla ya yote kufahamu kwamba na hii ni kabla ya kuanza kusambaza maji, je kuna mito mingapi, maziwa, mifereji, vituo vya kusafisha maji na hifadhi ya maji (reservoirs). Hili la hifadhi ya maji ndilo muhimu zaidi kwani hizi hifadhi zatakiwa ziwe katika maeneo ambayo watu watapata maji safi na salama na ya uhakika.

Pili, ni kutambua ni kipi cha maji chatumika kwenye kilimo, viwandani, mahotelini na kwenye migahawa na majumbani. Ukigundua kuwa ni wapi maji yatumika sana au yamwagika basi utaweka njia sahihi ya kuvuna maji hayo ili yale yalo safi yaweze kurudi kwenye mfumo uliopo na yale yasotakiwa yaende kama maji taka. Pia sehemu hizi zikifungwa mita sahihi na zenye kuweza kutoa data za uhakika za matumizi sahihi ya maji, hiyo pia itasaidia kuweka kubaini wapi penye kasoro na pahitaji marekebisho.

Tatu, ni kubaini wapi kuna uhaba na wapi kuna uwingi na ziada ya maji. Hii yaendana na kuweka mita zitazosoma matumizi ya maji hayo na pia itawezesha kujengwa kwa njia maalum za kuweza kukinga maji hayo ili yaelekezwe katika hifadhi zilizopo.

Sasa katika mambo hayo matatu hapo juu bado siamini kama ni kweli hakuna taarifa zozote zilichapishwa na wataalam wa maji zinohusu hayo mambo au ndo wameandika na wizara imepuuza. Hiyo pia yanikumbusha yule mwananchi ambae alikuwa ni wa darasa la saba ambae alimuambia hayati JPM kwamba alipotoa ushauri wake kwa wizara ya maji akaishia kuulizwa CV yake ni ushauri wake ukapuuzwa, kwanini sie waafrika twazidi kuwa wapumbavu kiasi hiki miaka 64 baada ya huru twapigizana kelele kuhusu kero ya maji?

Wenzetu UAE na Kuwait ingawa wapo jangwani lakini wananchi wake wapata maji safi na salama na hii yatokana na viongozi wao kuw ana vitu muhimu wanapofikiri, ubunifu na maono. Bila hivi vitu viwili watanganyika hatutafika kokote na kama serikali yenyewe haina nia ya kufikiria ubunifu na kuwa na maono, tusema tuwe na Maji Strategy 2040 nchi nzima, basi tumekwisha.

Tukiangalia katika nchi kunakuwepo mifumo mikubwa mitatu ya usambazaji maji ambayo yahusisha madaraja matatu, yaani kuna mitambo mikubwa ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, njia za usambazaji na hifadhi, mabomba makubwa ambayo yasambaza maji kutoa sehemu zenye maji ya ziada na kuyapeleka sehemu zenye uhitaji, na kwa miji ya pwani kama Dar-es-Salaam au Bagamoyo kuna mitambo ya kuzalisha maji safi na salama yanotokana na maji ya baharini.

Kama watanganyika huru tangia mwaka 1964 kweli tumeshindwa kujenga mitambo ya kusafisha maji ya chumvi (desalination Plants) kuwa maji safi na salalam ili kutumiwa majumbani? Wizara ya maji ingeweza kabisa kujenga mitambo hii katika pwani ya mji wa Dar-Es-Salaam na mji wa Bagamoyo na hata Kigamboni. Hivyo watu wa Bagamoyo, Dar-es=Salaam na Kigamboni wangetumia maji yanotokana na mitambo hiyo. Kazi ya kujenga mitambo hii wangepea wakandarasi ambao watokea kwenye nchi zilizojenga mifumo hii ikiwemo Israeli, UAE na Kuwait. Pia katika chuo cha maji ingawekwa kozi maalum kwa wanafunzi ambao wangejifunza namna ya kujenga vituo na mitambo hii ya Desalination.

Pia ipo mitandao ya maji katika kila mkoa yaani kwa mji wa Dar-es-Salaam DAWASA inakuwa na mitambo yake ambayo ni lazima ibadilishwe ili iwe ya kisasa na iweze kuendana na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu. Mabomba yapo na pia matenki yapo ya kuhifadhia maji. Shida iliyopo ni kutokuwepo mifumo ya kisasa ya kusoma matumizi ya maji hayo. Ni lazima pawepo mitambo ya kusoma matumizi ya maji ya ubora wake pia ili kweza kubaini mchakato wowote wa kuvuruga vyanzo na hifadhi za maji hayo. Hii pia yaendana na dhana kwamba maji mengi yameelekezwa katika baadhi ya sehemu zenye makazi ya watu fulani tu kwa upendeleo badala ya kuwa katika stratejia ya maji nchini.

Vituo vidogo vya usambazaji maji navyo ni tatizo kubwa kwani kwani mafundi maji huamua ni wakati gani waruhusu maji yatoke na ni wakati upi wazuie maji hayo na siku zote wana spana mkononi tiyari kupokea fedha za kuuza maji. Vuto hivi vidogo vya usambazaji maji ni lazima viwe na ulinzi wa masaa 24, viwe na mitambo ya kubaini wapi maji yavuja na wapi maji yamezuiwa, kuwepo na mita za kisasa na pia kuwepo na bomba moja kubw akwa ajili ya kusaidia wananchi ambao watahitaji maji nyakati za kiangazi au uhaba mkubwa unotokana na matatiz kutokea Ruvu Juu au Ruvu Chini.

Ni kweli kwamba kiangazi na ongezeko la watu ni baadhi ya changamoto zilizopo lakini bado serikali ni lazima iweke stratejia ya Maji kwa mkoa wa Dar-es-Salaam.

Zipi ni stratejia za kuhakikisha mji wa Dar-es-Salaam hauna shida ya maji kufikia 2030?

1. Kutengeneza ramani ionyeshayo usambazaji wa maji katika mji wa Dar-es-Salaam unoanzia kwenye mitambo ya Ruvu Juu au Ruvu Chini.
Ramani hii itasaidia kuomyesha sehemu zenye maji ya kutoha, wapi kuna uhaba na pia namna ya kusambaza maji zaidi kwenda kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi. Njia hii itaenda sambamba na kubaini sehemu zenye maji chini ya ardhi na kwamba endapo mtu agundua sehemu aliyopo amechimba na pana maji ni lazima aifahamishe wizara ya maji ili sehemu hiyo iwe ni nyaraka ya serikali kwa ajili ya kuelekeza maji hayo kwenda kwneye hifadhi.

2. Kujenga mitambo ya kusafisha maji ya chumvi kuwa maji safi na salama kwa matumizi ya majumbani, mahotelini na kwenye migahawa.

Kama nilivyosema hapo juu nchi za UAE na Kuwait au Israeli wana utaalam huu tuwazungumze ili watusaidie watatuona tuna akili na twajitambua na msaada utatoka kama umeme. Na hii isiwe Dar-es-Salaam pekee bali katika mikoa yote ya pwani kwetu Tanga na Mtwara. Sambamba na hili, pia kujengwe hifadhi za kistratejia (strategic reservoirs) ambazo zitakusanya maji nyakati za mvua. Sambamba na hili pia kuingizwa kozi maalum kwa ajili ya kufundisha wanafunzi wa chuo cha maji njia mpya za kuboresha usambazaji na usimamizi wa wa maji mijini.

4. Kuimarisha mitambo iliyopo.

DAWASA yatakiwa kuimarisha mitambo yake ya usambazaji maji (upgrading) kwa kuwekeza katika njia bora na za kisasa, kuwekeza katika mitambo mipya na kisasa ya kuchakata maji taka, kuweka mita za kisasa (smart metering) ili kuzuia na kudhibiti wizi wa maji na uunganishaji kiholela, kuwekeza kwenye teknolojia ya kubaini kuvuja kwa maji (Water Leaks) na pia kuwekeza kwenye mitambo ya kuchakata maji kupata yale yatayotuika kwenye viwanda na shughuli za kilimo.

5. Kusaidia kupatikana maji katika sehemu zenye matatizo ya miinuko au vijijini.

Hii ni pamoja na kutoa elimu na kuziwezesha shule, vituo vya afya na majumbani kutega na kuhifadhi maji katika hifadhi maalum nyakati za mvua, vijiji na tarafa kuwa na sehemu maalum ya kuteka maji wa ajili ya kijiji, kuweka mitambo ya kuchimba maji (boreholes) inotumia umeme wa jua ambayo itamilikiwa na DAWASA na ambayo ni rahisi kuiendesha, na haina gharama sana.

6. Kuunda timu za mafundi kufanya kazi masaa 24.

Timu hizi za mafundi maji zitakuwa na jukumu la k uhakikisha kunafanyika matengenezo yoyote yanohitajika masaa 24 (repair and maintenance), kutambua matobo na kuvuja kwa maji khasa kutoka kwenye mabomba makubwa, na ni lazima DAWASA iwe na namba ya simu (maalum hotline) kwa wananchi kutoa taarifa ya kuvuja kwa maji na pia DAWASA hiyohiyo iwe na namba ya WhatsApp ambayo wananchi pia wataitumia kutuma taariza za vitenfo vyovyote vya hujuma kwa njia za maji na wizi pia.

7. Kuunda mfumo wa kuondoa soko lisilo rasmi la maji.

Soko lisilo rasmi la maji limekuwa ni tatizo kwani ujasusi waweza kubaini kuwa maji mengi yanouzwa mabarabani huenda yatokea katika vyanzo vya maji ambayo ni mali ya DAWASA. Hivyo ili kukabiliana na tatizo hili ambalo lasababisha ukosefu wa mapato yaani (Non Revenue Water) ni kufunga mita za kisasa kaitika majengo yote marefu, majengo ya makazi (flats/ estates) majengo ya kiofisi, viwandani na maghalani na ipitishwe sheria kwamba ni kosa la jinai kuigusa mita ya DAWASA na kwamba mtu yoyote ataechakachua mita hizi atafikishwa mahakamani.

8. Utawala, Taasisi na Taarifa au Data.

DAWASA lazima iwekewe malengo yaani targets kwamba ndani ya miaka miwili kwa mfano kuwe kumejengwa "desalination Plants" na ziwe up and running. Kupunguza NRW na pia kuhakikisha kila mwaka kuna muunganisho mpya wa maji. Hii itaenda sambamba na waziri wa maji kuhakikisha chombo kinosimamia DAWASA au regulator chatoa taarifa ya ufanisi wa DAWASA kila baada ya miezi mitatu. Pia kuhakikisha kunakuwepo mipango maalum ya ufanisi na udhibiti wa vifaa na mali ya DAWASA pamoja na huduma bora kwa wateja.

9. Kufunguka kwa kutoa Data na kuwashirikisha wananchi.

Pamoja na kwamba wizara ya maji ina tovuti lakini bado taarifa sahihi hazionekani katika tovuti hiyo. Ni lazima katika tovuyi hiyo kuwepo na ubao (dashboard) ambayo yaelezea kila kanda na usambazaji maji, uhaba unotarajiwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mpya ya njia za maji. Pia kuwepo na sehemu ya maoni au feedback kutoka kwa wananchi ambao watakuwa huru kutuma ujumbe mfupi, katika mtandao wa WhatsApp na pia kuweka vituo maalum (wards) kwa kila ofisa wa maji wa wilaya kuzungumza na wananchi ili waeleze shida zao na zionekane hatua zilochukuliwa kukabiliana na shida hizo.

10. Kuunda mashirikiano na sekta binafsi, na taasisi zisizo za serikali. Hizi zitaidaisia wizara kuwa na wigo mpana wa msaada ambapo kwenye masuala kama namna ya kupata mitambo ya kuchuja maji ya mvua (desalination plants), namna ya kuuondoa tatizo kama la NRW na pia kusaidiwa kupata mita za kisasa (smart metering).

Mwisho, Tanganyika ina miaka 64 ya Uhuru ni miaka ya mtu mzima aliestaafu na yuko kijijini Korogwe. Waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha maji yapatikana nchi nzima una wajibu wa kufanya hivyo, hakikisha maji yapatikana nchi nzima kwa kuanza na mji wa Dar-es-Salaam na ifike wakati nchi nzima maji iwe ni historia.

Nimekupa nondo hizi chukua unoziona zafaa zifanyie kazi.

Bado zipo nyingi lakini hizi zakufaa wa sasa.
Safi sana sana sana mdau....

Shida ya huyu bw mdogo ni MAPENZI, wanawake wanampeleka peleka mpaka anasahau majukumu yake!

Shida iliyopo ni kutokuwepo mifumo ya kisasa ya kusoma matumizi ya maji hayo. Ni lazima pawepo mitambo ya kusoma matumizi ya maji
Sasa hivi kila nyumba au jengo Dar es Salaam linalopata huduma ya maji limefungwa mita ya kusoma matumizi ya maji.
Mamlaka inayosambaza maji wanakuja kusoma units zilizotumika na kusambaza bills kwa ujumbe wa simu.
Na maeneo yote yaliyofungwa hizo mita wamechukua GPS coordinates.
Hivyo kwa kutumia database yao wanajua maeneo gani yanatumika maji megi.
Tatizo matumizi ya hizo taarifa. Wanazitafsiri vipi kwenye mipango yao ya kuboresha huduma.
Ubunifu sifuri.
Usimamizi sifuri.
Na uwajibikaji sifuri.
Uzembe na ufisadi(rushwa, wizi au matumizi mabaya) nawapa 100%.
 
Nchi hii Kila mmoja anatengeneza tatizo kisha anatafuta suluhisho mwishoni...

Turejee nyuma kidogo, Kuna kipindi kulikuwa na malalamiko ya ukosekanaji wa umeme mara kwa mara na ndipo majenereta yakawa yanauzwa na ikanunuliwa mitambo mikuubwa... Mwisho wa siku tukaja kuona ishu iliyotokea kwenye mikataba ya RICHMOND na ndugu zake

Hivi wanao uza maji na magari au kwenye matenki wanayapata wapi haya' maji? Hili swali linatakiwa kujibiwa wanayapata wapi?

Nimebahatika kutembea nikaona Bonde la ruvu hivi lile bonde halina maji ya kutosha Ardhini? Na kama yapo Serikali Ina mpango gani...

Mbona Dodoma inalishwa na maji kutoka Ardhini? Kwanini si Dar?

Tunahitaji kitu kinaitwa UWAJIBIKAJI, UTU, UBINADAMU hivi ndivyo vinaweza kuiokoa nchi hii kutokana na changamoto zilizopo...

Kwenye uwajibikaji, viongozi watende wanayopaswa kuyafanya kwa mujibu wa viapo vyao, waache kujiandaa kwenye kununua magari ya kifahari na Mali ili kurahisishia familia zao

UBINADAMU na UTU ni pale tu' watakapo amua kuyabeba maumivu ya wengine yawe kama Yao...
Huko masaki kinondoni sijui kijitonyama mbezi beach wanachangamoto ya maji? Kama haya' maeneo hayana changamoto ya maji basi ni kuwa hawana utu wa kukubali kutumikia nchi Bali maisha yao kwanza
 
Solution ni katiba mpya itakayoruhusu watu sahihi kuwa kwenye nafasi sahihi za kiuongozi na kiutendaji. Watu wasio sahihi wasipate nafasi au wang'olewe haraka.
 
Mie hapa New York pana kaubaridi (nyuzi joto kama 6 hivi si haba) na nimekula pilau ya Xmas ambayo kapika shemeji /wifi yenu alifundishwa na mama mkwe wake kupika pilau ya maana. Wakati huohuo nimeweka ile muziki ya Bongo Classics nakula muziki taratibu kushusha msosi.

Lakini hapohapo nafikiria maisha ya wale watanzania ambao hawana maji safi na salama hii yasikitisha sana khasa ukimwambia mzungu eti Tanzania yenye miaka 64 ya huru ina shida ya maji!! Hapohapo wamwambia kwamba yapo maeneo yana maji kama kawaida (diverted water) na hawana shida kabisa).

Juzi nimemuona waziri wa maji Jumaa Aweso akihojiwa na Salim Kikeke na akashindwa kujibu suali lihusulo tatizo la maji kushindikana kutatuliwa ndani ya miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika. Lakini cha kushangaza pia ni kwamba waziri Uweso yupo kwenye wizara hiyo miaka mingi tangu ateuliwe mara ya kwanza na bado atakuwepo hapo kwa miaka mingine mitano (kama serikali yake bado itakuwepo kabla ya 2030).

Lakini pia nikafikiria nijaribu na mie kujiweka kwenye nafasi ya uwaziri wa maji je nitaweka mikakati ipi ya kuhakikisha kero ya maji yaondolewa Tanzania. Kwanza nirekebishe wale watu ambao hupenda kutumia neno Kero badala ya Shida ya Maji. Tatizo lililipo ni kwamba maji hayapatikani na hiyo imegeuka kuwa ni shida ya maji. Kero ni vile vilio na kelele za mahitaji ya maji hayo kutoka kwa wananchi. Hivyo waziri na serikali ijirekebishe moja kwa moja kutotumia neno Kero kwani neno hili lamaanisha kwamba serikali yaona kelele za wananchi ni Kero na kwamba itakapoamua ni lini itatue tatizo la maji itafanya hivyo.

Suala la maji si hisani kama serikali inavyofikiria kwamba yatoa huduma ya maji kwa wananchi wake kama hisani bali ni jukumu lake pamoja na barabara, umeme, hospitali, zahanati na elimu. Haya ni majukumu ya serikali yoyote ile ambayo imepewa ridhaa na wananchi iwangoze. Tatizo hapa kwa sasa tuna serikali ambayo haijapewa ridhaa (Mandate) na wananchi ikae madarakani, ingekuwa hivyo basi raisi angeapishwa rasmi mbele ya wananchi wote wa Tanganyika na akaungwa mkono na wananchi wote na kila mtu akawa na furaha kwamba tumepata raisi ambae akubalika na wananchi wote.

Sasa tuje kwenye tatizo la maji ambalo ndo msingi wa mada hii.

Ningeweza kuzungumzia tatizo la maji kwa nchi nzima lakini kwa leo tuangalie matatizo ya maji kwa mji wa Dar-es-Salaam kwa ujumla.

Matatizo ni kama yafuatavyo:

1. Upungufu na mgao wa maji.

2. Uwiano uso sawa wa upatikanaji wa maji.

3. Miundombinu ilochakaa na kuharibika bila kufanyiwa "Upgrade".

4. Kasi ya ukuaji wa idadi ya watu ambayo yazidi mifumo ya usambazaji maji.

5. Ukuaji wa sekta iso rasmi ya soko la maji.

Mji wa Dar-es-salaam hauna maji ya kutosha kwa wananchi jambo lilopelekea maji iwe ni shida kubwa kiasi cha maji hayo kuuzwa kwenye matenki na mapipa ya ukubwa mbalimbali. Lakini twasahau pia kwamba suala kama hili la maji ni lazima serikali iwashirikishe wadau kadha wa kadha, wananchi , kutengeneza stratejia na pia kutengeneza kanuni au framework ambayo ni lazima itumike na nchi nzima katika usambaza maji nchi nzima kiusawa, kiufanisi na kiuhimilivu.

Kiasi gani cha maji kilichopo ni suali la kwanza kabisa kabla ya yote kufahamu kwamba na hii ni kabla ya kuanza kusambaza maji, je kuna mito mingapi, maziwa, mifereji, vituo vya kusafisha maji na hifadhi ya maji (reservoirs). Hili la hifadhi ya maji ndilo muhimu zaidi kwani hizi hifadhi zatakiwa ziwe katika maeneo ambayo watu watapata maji safi na salama na ya uhakika.

Pili, ni kutambua ni kipi cha maji chatumika kwenye kilimo, viwandani, mahotelini na kwenye migahawa na majumbani. Ukigundua kuwa ni wapi maji yatumika sana au yamwagika basi utaweka njia sahihi ya kuvuna maji hayo ili yale yalo safi yaweze kurudi kwenye mfumo uliopo na yale yasotakiwa yaende kama maji taka. Pia sehemu hizi zikifungwa mita sahihi na zenye kuweza kutoa data za uhakika za matumizi sahihi ya maji, hiyo pia itasaidia kuweka kubaini wapi penye kasoro na pahitaji marekebisho.

Tatu, ni kubaini wapi kuna uhaba na wapi kuna uwingi na ziada ya maji. Hii yaendana na kuweka mita zitazosoma matumizi ya maji hayo na pia itawezesha kujengwa kwa njia maalum za kuweza kukinga maji hayo ili yaelekezwe katika hifadhi zilizopo.

Sasa katika mambo hayo matatu hapo juu bado siamini kama ni kweli hakuna taarifa zozote zilichapishwa na wataalam wa maji zinohusu hayo mambo au ndo wameandika na wizara imepuuza. Hiyo pia yanikumbusha yule mwananchi ambae alikuwa ni wa darasa la saba ambae alimuambia hayati JPM kwamba alipotoa ushauri wake kwa wizara ya maji akaishia kuulizwa CV yake ni ushauri wake ukapuuzwa, kwanini sie waafrika twazidi kuwa wapumbavu kiasi hiki miaka 64 baada ya huru twapigizana kelele kuhusu kero ya maji?

Wenzetu UAE na Kuwait ingawa wapo jangwani lakini wananchi wake wapata maji safi na salama na hii yatokana na viongozi wao kuw ana vitu muhimu wanapofikiri, ubunifu na maono. Bila hivi vitu viwili watanganyika hatutafika kokote na kama serikali yenyewe haina nia ya kufikiria ubunifu na kuwa na maono, tusema tuwe na Maji Strategy 2040 nchi nzima, basi tumekwisha.

Tukiangalia katika nchi kunakuwepo mifumo mikubwa mitatu ya usambazaji maji ambayo yahusisha madaraja matatu, yaani kuna mitambo mikubwa ya Ruvu Juu na Ruvu Chini, njia za usambazaji na hifadhi, mabomba makubwa ambayo yasambaza maji kutoa sehemu zenye maji ya ziada na kuyapeleka sehemu zenye uhitaji, na kwa miji ya pwani kama Dar-es-Salaam au Bagamoyo kuna mitambo ya kuzalisha maji safi na salama yanotokana na maji ya baharini.

Kama watanganyika huru tangia mwaka 1964 kweli tumeshindwa kujenga mitambo ya kusafisha maji ya chumvi (desalination Plants) kuwa maji safi na salalam ili kutumiwa majumbani? Wizara ya maji ingeweza kabisa kujenga mitambo hii katika pwani ya mji wa Dar-Es-Salaam na mji wa Bagamoyo na hata Kigamboni. Hivyo watu wa Bagamoyo, Dar-es=Salaam na Kigamboni wangetumia maji yanotokana na mitambo hiyo. Kazi ya kujenga mitambo hii wangepea wakandarasi ambao watokea kwenye nchi zilizojenga mifumo hii ikiwemo Israeli, UAE na Kuwait. Pia katika chuo cha maji ingawekwa kozi maalum kwa wanafunzi ambao wangejifunza namna ya kujenga vituo na mitambo hii ya Desalination.

Pia ipo mitandao ya maji katika kila mkoa yaani kwa mji wa Dar-es-Salaam DAWASA inakuwa na mitambo yake ambayo ni lazima ibadilishwe ili iwe ya kisasa na iweze kuendana na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu. Mabomba yapo na pia matenki yapo ya kuhifadhia maji. Shida iliyopo ni kutokuwepo mifumo ya kisasa ya kusoma matumizi ya maji hayo. Ni lazima pawepo mitambo ya kusoma matumizi ya maji ya ubora wake pia ili kweza kubaini mchakato wowote wa kuvuruga vyanzo na hifadhi za maji hayo. Hii pia yaendana na dhana kwamba maji mengi yameelekezwa katika baadhi ya sehemu zenye makazi ya watu fulani tu kwa upendeleo badala ya kuwa katika stratejia ya maji nchini.

Vituo vidogo vya usambazaji maji navyo ni tatizo kubwa kwani kwani mafundi maji huamua ni wakati gani waruhusu maji yatoke na ni wakati upi wazuie maji hayo na siku zote wana spana mkononi tiyari kupokea fedha za kuuza maji. Vuto hivi vidogo vya usambazaji maji ni lazima viwe na ulinzi wa masaa 24, viwe na mitambo ya kubaini wapi maji yavuja na wapi maji yamezuiwa, kuwepo na mita za kisasa na pia kuwepo na bomba moja kubw akwa ajili ya kusaidia wananchi ambao watahitaji maji nyakati za kiangazi au uhaba mkubwa unotokana na matatiz kutokea Ruvu Juu au Ruvu Chini.

Ni kweli kwamba kiangazi na ongezeko la watu ni baadhi ya changamoto zilizopo lakini bado serikali ni lazima iweke stratejia ya Maji kwa mkoa wa Dar-es-Salaam.

Zipi ni stratejia za kuhakikisha mji wa Dar-es-Salaam hauna shida ya maji kufikia 2030?

1. Kutengeneza ramani ionyeshayo usambazaji wa maji katika mji wa Dar-es-Salaam unoanzia kwenye mitambo ya Ruvu Juu au Ruvu Chini.
Ramani hii itasaidia kuomyesha sehemu zenye maji ya kutoha, wapi kuna uhaba na pia namna ya kusambaza maji zaidi kwenda kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi. Njia hii itaenda sambamba na kubaini sehemu zenye maji chini ya ardhi na kwamba endapo mtu agundua sehemu aliyopo amechimba na pana maji ni lazima aifahamishe wizara ya maji ili sehemu hiyo iwe ni nyaraka ya serikali kwa ajili ya kuelekeza maji hayo kwenda kwneye hifadhi.

2. Kujenga mitambo ya kusafisha maji ya chumvi kuwa maji safi na salama kwa matumizi ya majumbani, mahotelini na kwenye migahawa.

Kama nilivyosema hapo juu nchi za UAE na Kuwait au Israeli wana utaalam huu tuwazungumze ili watusaidie watatuona tuna akili na twajitambua na msaada utatoka kama umeme. Na hii isiwe Dar-es-Salaam pekee bali katika mikoa yote ya pwani kwetu Tanga na Mtwara. Sambamba na hili, pia kujengwe hifadhi za kistratejia (strategic reservoirs) ambazo zitakusanya maji nyakati za mvua. Sambamba na hili pia kuingizwa kozi maalum kwa ajili ya kufundisha wanafunzi wa chuo cha maji njia mpya za kuboresha usambazaji na usimamizi wa wa maji mijini.

4. Kuimarisha mitambo iliyopo.

DAWASA yatakiwa kuimarisha mitambo yake ya usambazaji maji (upgrading) kwa kuwekeza katika njia bora na za kisasa, kuwekeza katika mitambo mipya na kisasa ya kuchakata maji taka, kuweka mita za kisasa (smart metering) ili kuzuia na kudhibiti wizi wa maji na uunganishaji kiholela, kuwekeza kwenye teknolojia ya kubaini kuvuja kwa maji (Water Leaks) na pia kuwekeza kwenye mitambo ya kuchakata maji kupata yale yatayotuika kwenye viwanda na shughuli za kilimo.

5. Kusaidia kupatikana maji katika sehemu zenye matatizo ya miinuko au vijijini.

Hii ni pamoja na kutoa elimu na kuziwezesha shule, vituo vya afya na majumbani kutega na kuhifadhi maji katika hifadhi maalum nyakati za mvua, vijiji na tarafa kuwa na sehemu maalum ya kuteka maji wa ajili ya kijiji, kuweka mitambo ya kuchimba maji (boreholes) inotumia umeme wa jua ambayo itamilikiwa na DAWASA na ambayo ni rahisi kuiendesha, na haina gharama sana.

6. Kuunda timu za mafundi kufanya kazi masaa 24.

Timu hizi za mafundi maji zitakuwa na jukumu la k uhakikisha kunafanyika matengenezo yoyote yanohitajika masaa 24 (repair and maintenance), kutambua matobo na kuvuja kwa maji khasa kutoka kwenye mabomba makubwa, na ni lazima DAWASA iwe na namba ya simu (maalum hotline) kwa wananchi kutoa taarifa ya kuvuja kwa maji na pia DAWASA hiyohiyo iwe na namba ya WhatsApp ambayo wananchi pia wataitumia kutuma taariza za vitenfo vyovyote vya hujuma kwa njia za maji na wizi pia.

7. Kuunda mfumo wa kuondoa soko lisilo rasmi la maji.

Soko lisilo rasmi la maji limekuwa ni tatizo kwani ujasusi waweza kubaini kuwa maji mengi yanouzwa mabarabani huenda yatokea katika vyanzo vya maji ambayo ni mali ya DAWASA. Hivyo ili kukabiliana na tatizo hili ambalo lasababisha ukosefu wa mapato yaani (Non Revenue Water) ni kufunga mita za kisasa kaitika majengo yote marefu, majengo ya makazi (flats/ estates) majengo ya kiofisi, viwandani na maghalani na ipitishwe sheria kwamba ni kosa la jinai kuigusa mita ya DAWASA na kwamba mtu yoyote ataechakachua mita hizi atafikishwa mahakamani.

8. Utawala, Taasisi na Taarifa au Data.

DAWASA lazima iwekewe malengo yaani targets kwamba ndani ya miaka miwili kwa mfano kuwe kumejengwa "desalination Plants" na ziwe up and running. Kupunguza NRW na pia kuhakikisha kila mwaka kuna muunganisho mpya wa maji. Hii itaenda sambamba na waziri wa maji kuhakikisha chombo kinosimamia DAWASA au regulator chatoa taarifa ya ufanisi wa DAWASA kila baada ya miezi mitatu. Pia kuhakikisha kunakuwepo mipango maalum ya ufanisi na udhibiti wa vifaa na mali ya DAWASA pamoja na huduma bora kwa wateja.

9. Kufunguka kwa kutoa Data na kuwashirikisha wananchi.

Pamoja na kwamba wizara ya maji ina tovuti lakini bado taarifa sahihi hazionekani katika tovuti hiyo. Ni lazima katika tovuyi hiyo kuwepo na ubao (dashboard) ambayo yaelezea kila kanda na usambazaji maji, uhaba unotarajiwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mpya ya njia za maji. Pia kuwepo na sehemu ya maoni au feedback kutoka kwa wananchi ambao watakuwa huru kutuma ujumbe mfupi, katika mtandao wa WhatsApp na pia kuweka vituo maalum (wards) kwa kila ofisa wa maji wa wilaya kuzungumza na wananchi ili waeleze shida zao na zionekane hatua zilochukuliwa kukabiliana na shida hizo.

10. Kuunda mashirikiano na sekta binafsi, na taasisi zisizo za serikali. Hizi zitaidaisia wizara kuwa na wigo mpana wa msaada ambapo kwenye masuala kama namna ya kupata mitambo ya kuchuja maji ya mvua (desalination plants), namna ya kuuondoa tatizo kama la NRW na pia kusaidiwa kupata mita za kisasa (smart metering).

Mwisho, Tanganyika ina miaka 64 ya Uhuru ni miaka ya mtu mzima aliestaafu na yuko kijijini Korogwe. Waziri mwenye dhamana ya kuhakikisha maji yapatikana nchi nzima una wajibu wa kufanya hivyo, hakikisha maji yapatikana nchi nzima kwa kuanza na mji wa Dar-es-Salaam na ifike wakati nchi nzima maji iwe ni historia.

Nimekupa nondo hizi chukua unoziona zafaa zifanyie kazi.

Bado zipo nyingi lakini hizi zakufaa wa sasa.
Usihangaike kuandika mengi. Huyu ndie waziri wa maji tangu Uhuru, ni corrupt kuliko wote ktk hiyo wizara. Ndiye Waziri wa maji ambae nimeshuhudia mabomba ya maji yakitoa matope badala ya maji safi. Na hajaweza kutatua hiyo changamoto hadi leo. Sema amshukuru Samia, kapiga hela sana kwenye miradi feki ya maji.
 
Vita vya urais kuelekea 2030,washindani wa mtoto lazima washughulikiwe ipasavyo wapoteze mvuto!

Nakumbuka jamaa alikua jembe kweli kweli !lakini Leo anaonekana kituko coz bundi anacheza wizarani make apoteze mvuto then asiwepo kwenye equation ya challenge ijayo!

So unaona Mwigulu kapewa Ili apotee kabisa kimedani!!?

Nawaza!kama kawaida yangu Huwa na mawazo fulani!
 
Back
Top Bottom