Ushauri wa ununuaji gari ya kuanzia maisha

Hiyo pesa haitoshi hata kula kwa mwezi moja.
Gari ndogo kama ist , passo, starlet mafuta kwa siku si chini ya 20k i.e. lita 7
Bora ununue tvs au boxer
Kwan akiwa na gari lazima aliendeshe Kila siku?, Umejuaje kama mafuta Si chini ya elfu 20? Acha kukatisha tamaa watu bhana
 
Kama bajeti yako ya kununua gari Ni Mil. 6, basi jitahidi katika kutafuta kwako gari ulinunue kwa Mil 5.

Hiyo Milioni 1 tafuta fundi mzuri akufanyie service ya maana.
 
Ukimiliki gari utashangaa unakosa pesa ya chakula, pesa ya kununua nguo lakini somehow pesa ya mafuta hautakosa. Na gari itakuwa inatembelewa hivyo hivyo kwa kuunga unga
 
Kwani shida nini hapo, unampeleka tu chap anakupa mpunga noti moja unageuka unaendelea na ratiba zako.
 
Chukua IST kama utapata, tenga pesa ya service ya engine, gear box na miguu hakikisha vipo vema. Kisha rekebisha matatizo ya umeme yote. Halafu anza kuiendesha kwa ustaarabu utadumu nayo. IST nyingi zinauzwa kati ya milioni 7 hadi 12 kwa used za Tanzania ambazo zinakuwa vizuri tu na zinahitaji service ya at least 30%.

But ukitaka mpya una option ya kuagiza na mawakala hawa wajapan kama una cash kuanzia 15 milion. Na kama hauna uwezo wa hiyo cash yote ila unaweza kulipa kidogo kidogo then nitakuwekea mawasiliano hapa ya mdau ambaye kwa IST ya kuagiza japan utachagua zilizopo Yard yao (ni nzuri sana mimi nimeshafika hapo yard na kujiridhisha sio wapigaji hata wewe nakushauri uende ukajionee) au wakuagizie utayochagua wewe mtandaoni iletwe.

Utalipia milioni 7 kwanza then utapewa IST yako uanze kuitumia wakati kadi watabakia nayo wao huku ukiwa unalipia kidogo kidogo na kama ukipata pesa ya mkupuo unaweza futa deni mara moja ili usiteseke na riba zao.

Nakuwekea hapa mawasiliano umtafute kijana akupe muongozo zaidi kulingana na mapato yako.

+255749681935 kampuni inaita TERA.
 
Ushauri mzuri sana.
 
Rush ni mzuri na sio beighali
Wewe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hebu shika adabu yako kwanza kabla haujaendelea halafu futa hii reply yako hapa kabla ya wauza magari hawajaiona.

Wewe unaongelea Rush gari au pikipiki? [emoji23][emoji23][emoji23]

Rush unaijua vizuri wewe?

Kale kagari kanaenda bei juu ya Rav 4, kanashinda bei na gari kubwa ambazo sio za kulinganishwa nazo ila ndipo bei yake ipo huko. Ebo.
 
Mwaka unakaribia kuisha, vipi mleta uzi ulifanikiwa kununua lile garii?
 
Milioni 10 [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] dah kummke. Nielekeze ulipo nikuletee wateja zaidi ya kumi watakupa milioni kumi kumi hizo ili uwaletee Rush zao na nitakufanyia mpango kila mteja akupe milioni 1 ya shukurani kwa kuwapa deal nzuri.


Eti milioni 10,hiyo milioni 10 IST itaishia bandarini hapo hautaitoa hadi umalizie deni lililosalia.
 
Mkuu mimi naona ungejichanga had 10 milion ,ununue IST ya uhakika zaidi, sijawah miliki ila kwa uzoefu wa weng nasikia mafuta ya 50000 unaznguka nayo hata mwez , na hata yakiisha ukiipitisha sheli tu geji ya mafuta inasomaaa hyoo
Story za miaka ya nyuma ya 2020 usizilete mwaka 2024 kwasababu lita 1 mwaka 2020 sio sawa na lita moja mwaka huu 2024.

Kuna utofauti so sasa hivi hausemi mafuta ya 50,000 sema ya 70,000 ndio utakuwa sahihi.
 
Mm ninae tvs pikpik nimeipak ndan Sina hata 100 ya kuweka wese
Npo tu ndan naangalia Tv Kam fala fulan hiv na libukta lang na ndan sijavaa hata chup

Chombo ya moto ni balaa mafuta yenywe ya kupima Kwa kijiko
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo unaipata kwa Toyota vitz cc990
Hizo ndizo zinakamua wese kushinda IST uliza wanaizimiliki. Usione kagari kama CC990 ukahisi katakusevu mafuta utaingia chaka.

Engine zinakuwa hazina nguvu kwahiyo ukiwa unapita kwenye miinuko mirefu, ukiwasha AC wakati unaendesha, ukiweka mzigo au kubeba watu wengi huku AC inafanya kazi then unapita kipande cha miinuko ndipo utaelewa.

Namna kale kagari katakuwa kana lalamika kuelemewa na mzigo ndipo kanakunywa mafuta kushinda IST.

So gari nzuri kwa hizi baby walker chukua kuanzia CC1200 hadi 1400 hizo ni nzuri kwenye kumaintain mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…