Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Act wazalendo , Maalim Seif usikubali kushiriki serikali ya wamwaga damu , kuhahalisha walichokipanda , usikubali maana utakuwa umehalalisha uchaguzi haramu kuwa halali .
 
Una umri gani?

Unachokijua ni next to nothing!

Post-election violence za 2010 zilichinja watu 3000+ Ivory Coast kisa Gbagbo kung'ang'ania madaraka.

Na kwa taarifa yako mpaka sasa Gbagbo keshafutiwa mashitaka yote toka November 2019 anakula bata akisubiri rufaa yao,sasa sijui Gbagbo yupi kafungwa ICC.

Kama mambo yangekuwa rahisi hivyo basi ICC ingeshajaa wafungwa.

Mnapoteza muda wenu tu.
Labda nikuulize wewe una umri gani???

Wapi hapa Gbagbo alishtakiwa kuua watu 3000???

Kwenye makosa yake hapa kuna kuua watu 3000????
CC4AD28C-C12F-429A-9F83-4A8B2ADFEA87.jpeg
 
Kwanza kujibizana na Lord dening kuhusu ICC ni kupoteza muda.

Jamaa ni mweupe kabisa kuhusu hiyo mahakama.

Mimi kila siku huwa nampa mfano wa hapo Kenya tu kwamba Kenyata na Odinga walisababisha watu zaidi ya 1500 kupoteza maisha lakini kesi yao kule icc haikumaliza hata mwaka na Kenyaga na Odinga ndio wale pale ikulh wanakula mema ya nchi.
Wapi hapa makosa ya Gbagbo yalikuwa ni kuua watu 3000???
11D93338-C12A-4613-BEFA-DEC72C213F9D.jpeg
 
Umri umeshaenda muacheni awatumikie wazanzibar kwa mlango mwingine.
Kwani lengo lao si moja?..
Mzee nenda ukale maisha.
 
Kama rais wa Zanzibar Hana mamlaka kwenye nchi ya Tanzania muungano una matatizo.kwanini rais wa TANGANYIKA ana sauti Zanzibar Ila rais wa Zanzibar asiwe na sauti TANGANYIKA?
Ni Rais wa Zanzibar, wewe umesoma shule gani?
 
Kuna maisha baada ya kukataa hyo nafasi.utamsaidia?
Act wazalendo , Maalim Seif usikubali kushiriki serikali ya wamwaga damu , kuhahalisha walichokipanda , usikubali maana utakuwa umehalalisha uchaguzi haramu kuwa halali .
 
Hivi mshindani aliyemshinda Zitto Kabwe ameshaapishwa bungeni? Anaitwa Nani?
Ushauri Muflisi!

Mtoa hoja atambue kuwa Zanzibar na Rais Hussein mwinyi hana cha kupoteza iwapo ACT Wazalendo, haitataka kushirikiana na nayo kwenye serikali ya maridhiano ya kitaifa kwa mujibu wa katiba.

Yeye ataendelea kupiga kazi katika kutatua kero za wananchi, wakati wao wakibaki vijiweni kupiga umbea na majungu baina yao na kupeleka umbea kwa mabeberu wao, huku Maalim Seif akiendelea kunufaika na mafao ya pensheni yake, kutokana na wadhifa aliokuwa nao wa kuwa Waziri Kiongozi wa SMZ, na Makamo wa Kwanza wa Rais wa SMZ.

Wasipupmbazwe na hoja za Zitto, ambaye bila ya kutarajia, ndoto zake zimepeperushwa, na sasa anatapatapa! ataendeleaje na msala wa maisha bila ya kuwa na pahala madhubuti pa kujishikia!.
 
Kama ACT Wazalendo wakikubali basi itakuwa wameeka mbele matumbo yao na haina haja kuwa na viongozi wanaotaka madaraka kuliko haki za watu.
 
Labda nikuulize wewe una umri gani???

Wapi hapa Gbagbo alishtakiwa kuua watu 3000???

Kwenye makosa yake hapa kuna kuua watu 3000????
View attachment 1630827
Una matatizo ya akili bila shaka.

Kuna mahali umeona nimeandika hata mashitaka ya Gbagbo mimi?

Nimekuambia zile vurugu za baada ya uchaguzi zilichinja watu 3000+ Ivory Coast baada ya Gbagbo kung'ang'ania madaraka.

Kwa hiyo Gbagbo amefungwa ICC kama ulivyodai? Hujakielewa hata hiyo attachment uliyoweka mwenyewe?

Ni ujuha kutegemea vifo vitatu vipeleke mtu ICC.
 
Akikataa wamnyime mgao wake kama Makamu wa Rais Mstaafu

Akikataa maana yake anafurahia mpasuko wa Znz

Akikiataa maana yake ni Wakala wa mabeberu

Akikataa maana yake kavunja katiba
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sasa wewe unawaamini hao jamaa kwa lipi?

Mfano uliweka imani yako kwa Lisu mpaka ukafikia hatua ya kusema mbele ya Lisu hata tume huru haina haja kwa lipi?

Seif keshajichokea kiumri hana la kupoteza, atakubali hiyo nafasi ili ajimalizie uzee wake vizuri.

Kajitahidi sana wakati wake, kapigana sana, lakini nyie wafuasi wake mnaishia kumsapoti mitandaoni.

Na Lisu alientegemea kumpa backup ndio huyo kala kona.

Bora ajikalie kimya ale maisha.

Siwaamini bali nawakubali, sio niliweka imani kwa Lisu, bali nina imani naye mpaka sasa. Sijawahi kuwa na imani na tume ya uchaguzi, bali uchaguzi huu wangalau tulikuwa naye akiongea lugha ya kuweka wazi udhaifu wa tume, hata kwa wale waliokuwa na mashaka na hilo sasa wanajua bila shaka kuwa hakuna tume ya uchaguzi,bali kikundi cha wahuni wa ccm. Lisu amekimbia nje maana anaweza kuuwawa. Kama Magufuli anasifiwa ni jasiri na hachezewi, mwambie aende hapo kariakoo kila siku bila ulinzi, kisha uje uchukue mrejesho hapa.

Huyo Maalim Seif kachoka sana na wala sio kachoka kidogo, lakini ni kiafya na umri na sio kisiasa. Maalim Seif tunamsupport kisiasa, na sio kijeshi, ingekuwa ccm inapambana kisiasa ungejua support yetu. Ifahamike hata alipokuwa makamu wa rais hakuna mtu alikuwa anaenda kupakia naye VX ili kutoonyesha kuwa anaridhika na support yetu. Wakati wa maandamano utafika, cha muhimu ni yeye na wengine kuweka mazingira hayo, ila akikubali sasa ndio kapoteza uungwaji wetu mkono. Yeye ni mzee, ni kipi hajala anataka aje akile akiwa na miaka 80?
 
Back
Top Bottom