Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Ushauri wangu kwa ACT Wazalendo na Maalim Seif

Maalim hawezi kukubali huu ubumbavu wao, kaamua kujibu kistaarabu tu lkn najua kimya chake kuna kitu kikubwa anapanga na ccm watajuta kuharibu uchaguzi.
 
Toka kaapishwa hajawahi kanyaga Pemba na baadhi ya sehemu Unguja kama Kaskazini Magharibi
Muda bado hata mwezi haujaisha jamani? Baraza lenyewe limetangazwa juzi sasa atakuwa katembelea nchi yote? Daa punguza hasira kidogo mkuu!
 
Msiwafundishe cha kufanya sasa!

Sio kwamba tunawafundisha bali tunawakanya wasithubutu, labda kama ndio wameamua kustaafu siasa. Kauandamana watu wangepoteza maisha, je wao wasipoenda huko serekalini watu watapoteza maisha?
 
Mtawaonea tuu, binadamu hali misimamo, kugoma hakumfanyi ashibe, muombee kitu kimoja tuu, njaa yao isiingie kichwani, kwa sababu ikiingia basi tumbo ndio litakalo fikiri na kutoa majibu.

Uko sahihi sana, lakini kitendo cha kujiunga na serekali ya wamwaga damu, ndio ajue amepoteza mazima kwenye siasa za ushawishi.
 
Hata Magufuli toka ameapishwa hajawahi kukanyaga hayo maeneo, na haiwezekani rais aapishwe halafu ghafla awe amekanyaga maeneo yote,
Nyumbu hovyo kabisa.
Si ndiyo hapo hata mwezi bado, serikali yenyewe hajamaliza kuiunda ndiyo awe ametembelea nchi nzima? Hii mihemko jamani watu wanatafuta sababu duu!
 
Ndugu Maalim Seif,

Tumekusikia ukikiri kupokea barua toka Serikali ya Zanzibar( Rais wa Zanzibar) juu ya kushiriki kwenu ACT Wazalendo kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Ushauri wangu kwenu ACT Wazalendo na Maalim Seif

Kamwe msiingie kwenye huu mtego. Kwa sababu kwenye miaka yote ya mapambano ya ukombozi ni mwaka huu ndo tumeona tunaenda kupata suluhisho la uhakika juu ya udhalimu wa CCM na watu wake.

Ni mwaka huu ambapo Jumuiya ya kimataifa imepata ushahidi mzito na mzuri juu ya CCM na ubaya wao hivyo wamedhamiria kweli kuchukua hatua dhidi ya CCM na vibaraka wake.

Maridhiano yoyote watakayofanya ACT na CCM kwenye hatua hii yatawafanya hata Jumuiya ya kimataifa kutuona hatunazo na tunachojali ni matumbo yetu tu.

Imefika muda ni lazima waliofanya ufedhuli wawajibishwe kwa matendo yao na wanaotaka kuwawajibisha hawawezi kupata nguvu ya kuwawajibisha kama na sie tukionesha hatujielewi na tunajali matumbo yetu!!!

Kama ni kukubaliana na CCM sharti kuu ni kuwa wale wote waliohusika na mauaji ya watu pamoja na kuiba Uchaguzi wakashtakiwe tena ICC , sio hapa Tanzania na sharti na pili liwe Uchaguzi urudiwe chini ya Tume mpya ilivyo huru na haki.

Nawaonya ACT, lolote watakalokubaliana na CCM litarudisha mafanikio tuliyoyapata mara milioni moja nyuma na hakuna hapa duniani atakaewaelewa.

Kama wao wanaangalia ruzuku ya kuendesha Chama , hawatakiwi kuhofu kwa sababu hata kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la EU limejadili Jana juu ya kuvisaidia vyama vinavyotetea demokrasia na haki za binadamu kwa Tanzania. Hivyo kama ni hela watapata zaidi ya hiyo ruzuku.

Tumefika sehemu lazima tuchore mstari kuwa kuna vitendo havitakiwi kufanyika Tanzania na vikifanywa na yeyote lazima awajibishwe iwe ndani au nje ya Tanzania.

Watanzania tumeumia sana kwa yaliyofanywa na CCM kwenye uchaguzi huu, uzuri Mungu ametuona ameleta wakombozi watusaidie kweli. Na kweli wanatusaidia, kamwe tusiwaangushe watanzania na hawa watu waliojitolea kutusaidia.

Cc.@Zitto kabwe , Ado Shaibu,@ Juma Duni Haji,@ Nassoro Mazrui, ismail Jussa
Maalimu ukikubali upuuzi huu,damu za wanzanzibar waliouawa wallah zitawalilia sana,acheni Wakae kwenye madaraka walioyatafuta kwa kuuwa watu
 
Mambo yashaanza kuchechuka sasa wanatafuta pa kushikilia washaona harufu ya ICC vikwazo nk sasa wanatafuta pa kuhemea.

Wallah Maalim ukikubali utakua umehalalisha yote utakuwa umekubali udhalimu ulotokea bara na visiwani.

Utakuwa umeleta divide and rule, maana tushaanza vizuri kama upinzani sasa ukilegeza nati moja ya mapambana utauharibu muqawama (mshikamano wa mapambano) ambao tumeuanza.

Utakuwa umeyakanusha yalotokea yote kwamba zilikua ni hadithi tu, sio hivyo tu utafanya miaka mitano ijayo udhalimu uendelee. Nakuasa usiangalie hii miaka mitano, angalia future ya wazanzibari na vijana wa tangangika ambao ninyi viongozi mmekua kama taa ya kuwaongoza katika mapambana.

Ukikubali sasa hivi miaka ijayo itakua michungu zaidi, utarudi nyuma hatua 1000.

Nimeiona na hii pia mdau kashauri[emoji1313]

Maalimu akiingia kwenye serikali hiyo ya dhulma siyo tu kwamba atakuwa amewasaliti Wazanzibari bali atakuwa amesurrender kwa wanyang'anyi.

Atawasaidia kuwapa CCM legitimacy wasiyoistahili, na atakwamisha jitihada ya kufanyika kwa reforms za msingi nchini za kikatiba za upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi na hata katiba mpya

Atawasafisha wauaji waliovamia Zanzibar kuteka na kupora maamuzi ya Wazanzibar dhidi ya dhambi yao ya kuua, kupiga na kutesa wananchi wa Zanzibar wasio na hatia.

Na kibaya zaidi ACT-Wazalendo ikiingia katika serikali hii itaipa serikali ya muungano life Support ya kidiplomasia ambayo inaihitaji sana baada ya dunia kuinyooshea kidole kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.

Nawaomba wana za ACT Wazalendo, kikubwa na cha msingi siyo kugawana vyeo bali ni reforms za msingi. Tupambane tupate katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, Kama mkijiunga kwenye serikali haranu ya Zanzibar, mtakosa moral authority ya kudai haya mambo kwa nguvu zote kwa sababu na nyie mtakuwa sehemu ya serikali.

Kumpa Maalim umakamu ni kumpoza yeye lakini hakuna manufaa ya maana kwa wananchi wa Zanzibar.

Maalimu kumbuka, hawa wanaotaka kukupa cheo ndiyo haohao waliokufanyia hila kukutoa kwenye CUF. Sasa leo hii uzuri wako kwao umetokea wapi?

ACT Wazalendo, Achaneni na hizi nafasi mlizorushiwa chambo! Mkihalalisha haya mtakuwa mmeubga mkono udhslimu na nyie mtakuwa sehemu ya udhalimu. Sisi Wananchi tutawadharau na kuwapuuza!

Hivi leo eti maalimu apate kura 19% si ushenzi huo?

Maalim akikubali kukalia hiyo nafasi wakati wamemfanyia hiyana nzito na kumdhalilisha, Wqzanzibar waramuondolea heshima kubwa sana wwliyompa. Ni bora akastaafu kwa heshima akaacha legacy ya kutukuka ya kupigania maslahi ya Wazanzibar badala ya kustaafu huku wakiwa wamemtukana kwa kumpa cheo ambacho wao CCM wwnajua ukweli kuwa alistahili kuwa zaidi ya hapo!


Tatizo linalowakumba Viongozi wa upinzani ni Ukata unaotokana na wao wenyewe kushindwa kutumia Rasilimali watu kuendesha vyama vyao na kuwaenzi viongozi wao wakuu .
Chama Kama ACT Wazalendo kina Wanachama wengi Zaidi ya Laki saba , bara na vizwani.
Viongozi wangekua wamevijenga vyama vyao kuanzia Chini mpaka Juu wangeweza kuanzisha mchakato wa kuvijenga vyama vyao na kuwaenzi vingozi wao kwa kuwachangia fedha kwa ajili ya Mafao yao wanapostaafu.
Wanachama Laki 7 wakichanga kila moja 2000 ni takribani bil.1.4 . Kama wanatokea watu waaminifu kabisa ,fedha kama hizo angekabidhiwa Maalim Seif kama Kiinua mgongo chake ndani ya Chama na upinzani alitumika kupigania Demokrasia. Hiyo ingejenga moyo zaidi kwa viongozi wa Upinzania kuepuka mikataba ya kupoozwa na vyeo baada ya kuumizwa na CCM ambao wao wanatumia nguvu ya Chama na Serikali kufanya wanalotaka na fimbo yao kuu ni madaraka.


Lakini pia wapinzani wasiishie hapo kwa viongozi bali waende mbali zaidi kwa wanachama wao waliopoteza ndugu kwenye harakati halali za kupigania Demokrasia.
Mfano: Familia ya Ben saanane na Alfonsi Mawazo na wengine wengi waliangamizwa kwa sababu ya kusema kile wanachokiamini kuwa ni kweli kama haki ya kisiasa na kutoa maoni.
Hawa kwa Upande wa Chadema yenye wanachama Takribani Mil. 6 wapishindwa kuchanga rambirambi kwa hamasa kubwa nchi nzima kwa ajili ya kuwahudumia familia hizo kwa muda mrefu ili zisiteseke.Mfano kila Familia ingeweza kupewa mil.100 kwa ajili ya kusomesha watoto wao au wazazi wao au wajane waliobaki.
Nilishangaa Mgombea mmoja wa upinzani akiambiwa kuwa Mgonjwa ambaye ni mpenzi wa chama chake alikua anadaiwa Pesa za matibabu elfu 35 badala ya kuzichangisha pale pale na kumpatia hata laki tano ,yeye alompa Bendera ya Chama . Kosa kubwa kwenye siasa za Afrika zinazogharimu maisha ya watu wengi hasa wapinzani.

ACT waepuke sana mitego ya CCM lakini pia waangalie Kesho njema ya Maalum Seif baada ya kustaafu kwenye siasa na uongozi.
 
Una umri gani?

Unachokijua ni next to nothing!

Post-election violence za 2010 zilichinja watu 3000+ Ivory Coast kisa Gbagbo kung'ang'ania madaraka.

Na kwa taarifa yako mpaka sasa Gbagbo keshafutiwa mashitaka yote toka November 2019 anakula bata akisubiri rufaa yao,sasa sijui Gbagbo yupi kafungwa ICC.

Kama mambo yangekuwa rahisi hivyo basi ICC ingeshajaa wafungwa.

Mnapoteza muda wenu tu.
Kwanza kujibizana na Lord dening kuhusu ICC ni kupoteza muda.

Jamaa ni mweupe kabisa kuhusu hiyo mahakama.

Mimi kila siku huwa nampa mfano wa hapo Kenya tu kwamba Kenyata na Odinga walisababisha watu zaidi ya 1500 kupoteza maisha lakini kesi yao kule icc haikumaliza hata mwaka na Kenyaga na Odinga ndio wale pale ikulh wanakula mema ya nchi.
 
Hata wakati wa ukoloni, kulikuwa na waafrika wanasema wazungu wasisumbuliwe maana wamewapa waafrika wenzetu vyeo. Ni hivi, huyo maalim Seif akikubali kuingia kwa hiyo serikali ya wamwaga damu na wezi wa kura ajue ndio mwisho wetu wananchi kuwaamini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sasa wewe unawaamini hao jamaa kwa lipi?

Mfano uliweka imani yako kwa Lisu mpaka ukafikia hatua ya kusema mbele ya Lisu hata tume huru haina haja kwa lipi?

Seif keshajichokea kiumri hana la kupoteza, atakubali hiyo nafasi ili ajimalizie uzee wake vizuri.

Kajitahidi sana wakati wake, kapigana sana, lakini nyie wafuasi wake mnaishia kumsapoti mitandaoni.

Na Lisu alientegemea kumpa backup ndio huyo kala kona.

Bora ajikalie kimya ale maisha.
 
Hilo ni hitaji la katiba ,ACT nashauri wakubali chama chao kinahitaji kukua.
 
Kwanza kujibizana na Lord dening kuhusu ICC ni kupoteza muda.

Jamaa ni mweupe kabisa kuhusu hiyo mahakama.

Mimi kila siku huwa nampa mfano wa hapo Kenya tu kwamba Kenyata na Odinga walisababisha watu zaidi ya 1500 kupoteza maisha lakini kesi yao kule icc haikumaliza hata mwaka na Kenyaga na Odinga ndio wale pale ikulh wanakula mema ya nchi.
Na Bagbo yuko wapi?
 
Nimeona kuna dalili kuwa atakubali. Lakini nitashangazwa sana akifanya hivyo.
On a serious note....
Maalim hana muda mwingine tena wa kugombea kiti cha urais Zenji....
umri na nguvu vimeshamtupa mkono....
it's better aseto now...
 
Back
Top Bottom