KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,187
Mkuu 'Lord', nimekusoma na kusikitika nawe pamoja kwa yaliyotokea.Tundu Antiphas Lissu
Umeona yaliyotokea, kura Watanzania tumepiga ila matokeo yake ndIo hayo. Matokeo yanayotangazwa sio matokeo ya kura zilizopigwa ni matokeo ambao tayari NEC na CCM walikuwa nayo kabla hata ya uchaguzi. Kilichofanyika Jana ni kujaribu kuionesha dunia kuwa kuna uchaguzi wakati hakuna uchaguzi ila washindi walishaandaliwa.
Napenda kukushauri, Watanzania wa Bara sio watu wa kuanza. Ni watu wa kumuona mtu ana anza na wao wanamfuata nyuma. Watanzania wengi wanapenda kuona mfano kwanza then wao ndo hufuata.
Kwa Tanzania ya leo huwezi ku achieve jambo bila kulianzisha mwenyewe. Usione hivi, Watanzania wengi wameumia na huu uhuni uliofanywa na CCM, hao wanaokusema vibaya ni watu wachache sana ambao ndo wana Ccm wenyewe , wengine Tupo na wewe.
Napenda kukushauri jambo moja, kama ni kuaga, ageni familia zenu na ndugu zenu, then wote mtangaze mahali pa kuonana katika maandamano yenu, ifanyike kwenye mikoa yote na muwe serious kwenye hili.
Tangazeni, tarehe ya kufanya haya na muanze kweli. Hata mkianza 2 nawaambia kadri ya muda utakavyokuwa unaenda mtaona watu wanazidi kuongezeka. Najua pia hakuna dunia itakaa kimya ikiona mkifanyiwa unyama
Lakini najua wewe sio msahaulifu kiasi hiki, mpaka usahau yaliyompata Mbowe na wenzake kule Kinondoni na kuishia Akwilina kupoteza maisha na Mbowe na wenzake kupata kifungo!
Ulisikia mTanzania aliyenyanyua kidole, pamoja na kwamba uonevu ule ulikuwa wazi kabisa?
Ndio, waTanzania walichanga kwa moyo safi kuwatoa gerezani wabunge wa CHADEMA, lakini sio kwenye harakati kama hizo unazomshauri Lissu azianzishe. Hutamwona mTanzania atakayejitokeza hapo.
Mange naye umemsahau na yale ya kwake nyakati zile?
Niseme tu, kwamba kuna kitu kinachowafanya waTanzania wasichemke damu hata kama wanaonewa waziwazi na kunyimwa haki zao.
Kitu hiki kinachowafanya waTanzania kuwa na hulka hii bado hakifahamiki, nadhani kuna kila sababu ya kulifanyia utafiti hili jambo.
Kwa hiyo, ushauri wako kwa Lissu, pamoja na kuwa wa nia njema, ni ushauri usiotekelezeka kabisa kwa waTanzania hawa tulionao sasa.
Lissu atateswa sana na hakuna atakayenyanyua mguu juu yake. Labda wamstahiki tu kwa kuogopa mahakama ya dunia, sio mahakama ya hapa nyumbani ya kuwategemea waTanzania waitoe.