naunga mkono hoja......ya kukaa kimya lakini, hayo ya kwamba hakufanya chochote katika uraisi wake wa miaka kumi nayaacha nafsini mwa mtoa mada; aendelee kubishana nayo, yeye na Mungu wake anaemuamini. ila kwa upande wangu baadhi ya mambo ninayoyakumbuka kwa kikwete ni ujenzi wa mabarabara nchi nzima, ajira (ingawa siliangalii sana hili), ujenzi wa flyovers (nakumbuka kama sio 2010 basi 2011 nilishuhudia kwa macho yangu flyover ya tazara pale ikipimwa na kuwekwa tayari), hospitali nyingi tu km ile ya mloganzira, sijajua vizuri kuhusu chuo kikuu cha dodoma na shule za kata n.k
kwanini nami namtaka akae kimya?
jk anaandamwa, anachukiwa na kufuatiliwa mno na kundi lisilompenda lililoandaliwa vema kipindi kile (ingawa kwa wananchi wa kawaida jk wanamkubali sana.....ana nyota nao huku uswahilini tunasema). kuhusu hili nitaeleza kwa kirefu kidogo;
chuki na imani hii iliasisiwa wakati wa serikali ya awamu ya tano kwa nguvu kubwa; kilipondwa kila alichofanya, ulipigiwa kelele ya wizi kila mkataba wa mradi alioufanya wakati wake, lilisemwa dhaifu na tumepigwa katika kila jengo alilojenga.....tukawahi kuambiwa na kuonyeshwa ghorofa lililojengwa kwa mil.500 kama jitihada za kuhalalisha tuhuma hizo kwa kikwete ingawa nyumba ya kawaida tu std hujengwa mpaka mil.150. iweje ghorofa yenye floors kadhaa ijengwe kwa mil.500 hakuna aliyejua, na kwakuwa aliyesema alikuwa ni mwenye nguvu kuu akisaidiwa na uvivu wa kufikiri wa watanzania pamoja na uwekezaji wa kutosha wa kina musiba (aliyewahi kulipiwa mahali na jk), makonda, polepole, bashiru n.k, jina la kikwete likafanikiwa kuhusishwa moja kwa moja na ufisadi, wizi, unyang'anyi, kujuana, ulaghai n.k.
kina musiba waliandaliwa na kudhaminiwa vizuri tu waifanye kazi hiyokwa kurusha mamia ya clips kila leo yakimuhusisha jk na uovu na kila anayehusika na jk alikiona cha moto; ni wizi tu na uibaji. propaganda iliyopigwa kisawasawa kwa muda wa miaka mitano na ushee, huku mpigiwa propaganda akiwa hana pa kujitetea na usemaji (kwa vyombo vya habari n.k) ukiwa umezuiliwa vilivyo, matunda yalipatikana ya kutosha na jk akatambulika kama mwizi, laghai, asiye mzalendo n.k. haikuishia hapo tu, familia yake na waliokuwa wasaidizi wake walihusishwa pia na kila aina ya uovu.
baada ya raisi Magufuli kufariki (r.i.p), 'watesi' wake jk wameumia mno. kilichowaumiza kikubwa ni kutotimia kwa malengo yao ya muda mrefu waliyojiwekea (km vile kuandaa uhakika wa kula kwa muda mrefu (kupitia mpango wa kubadilisha katiba n.k)), kutompenda aliyeachiwa madaraka (kwa sababu ya ukanda, udini, jinsia n.k) na uwezekano wa kubumburuka kwa mamia ya uovu/madudu yao yaliyojificha chini ya kivuli cha kumkandia 'mharibifu' jk. kwa kutokuelewa au kuelewa msimamo wa raisi aliyopo madarakani sasa, wameamua kuja na kila aina tusi na shutuma mbaya kuwahi kutokea tangu pande hili la ardhi liumbwe ilimuradi tu kujaribu kuiambukiza jamii ya kitanzania hisia za kumchukia jk na familia yake na marafiki zake wote......yaani abaki pekee duniani hapa akisubiria kujifia na familia yake ipate tabu isiyo mithirika. katika kuhakikisha wanajaribu kumdhibiti jk na mama samia kwa ujumla (ili amuogope na kumuweka mbali jk kwa lolote lile na abaki tu akiwategemea kina polepole, bashiru n.k) yafuatayo yamezushwa:-
1. jk ndiye aliyemuua magufuli (ingawa haielezwi kivipi sababu marehemu alizungukwa vizuri na watu wake huku jk na wale walioitwa 'timu yake' walikuwa mbali kabisa na huo utawala)
2. jk ndiye anayeongoza nchi na mama ni 'remote' tu (lengo hapa ni kumshushia hadhi mama samia (sababu si wa kwao) mbele ya watanzania na kuendelea kumchonganisha jk kwa watanzania.
3. baada ya kuteuliwa makamba juzi kelele zimezidi kuwa ni yeye aliyesababisha hilo. wanasema hivyo huku wakisahau kuwa makamba (ambaye sasa anatangazwa mwizi kwa nguvu kubwa) aliteuliwa uwaziri na magufuli na kudumu nao kwa miaka 4........haieleweki kaiba nini (zaidi ya maneno tu ya musiba na timu yake walioandaliwa) na ni vipi aliteuliwa uwaziri na mtu anayesemwa kuwa ni 'muadilifu kuwahi kutokea dunia hii'. kuongeza chumvi katika jeraha, wanasema nape na ridhiwani hivi karibuni wataongezwa katika baraza la mawaziri (linasemwa hili basi tu katika jaribio la kumchanganya mama na kumkera jk) na mengine mengi yanayosemwa.
kivipi sasa unyamaze jk;
1. kwa sababu ya future ya kijana makamba. chuki na kila jina baya unalopewa wewe sasa yanapelekwa pia kwa makamba. anaitwa mwizi, anatukanwa n.k hayo yote wanayafanya kwa hisia kuwa ni kijana wako na sababu ya chuki waliyonayo kwako. kwa wewe kusema lolote kwa seriakli hii (hata kama utasema kile kile ulichokisema katika serikali zingine) basi kitapata muitikio wa hivyo. tulia brother na muachie Mungu mkuu....imetosha. simjui kwa undani makamba lakini kwa uchache namuona ni mtu stable sana anaweza kufanya kitu sahihi kumuaibisha shetani.
2. kumpunguzia matusi mama samia. anatukanwa mno na kundi fulani kwa kukutumia wewe (km nilivyosema hapo juu). kutia neno lolote, hata liwe la kawaida kiasi gani katika serikali hii, ni kuwapatia sababu maadui zako (walioandaliwa vizuri) ya kumshambulia na kumuaibisha mama pamoja na kukushambulia wewe. najua wewe ni mtoto wa mjini na unaweza tu kula nao sahani moja, lakini kausha brother kwani imetosha sasa acha karma tu ifanye kazi.
nakuuunga mkono mtoa mada, jk anyamaze!!