PAZIA 3
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 1,102
- 1,919
Kuna Mambo yanaumiza Sana hasa unapoona kijana au mzee akipinga wazi wazi upinzani usishinde uchaguzi. Ni haki yao, lakini hebu fikiria, ukiondoa utawala wa awamu ya kwanza na wa pili, CCM imetuongoza kwa awamu tatu tangu kuanza kwa vyama vingi vya siasa, tumeona madhaifu yao, tumeona mazuri yao, basi tuwapeni na Wapinzani wafanye yao, tutalinganisha baada ya miaka 5 watakayoongoza.
Hatuwajaribishi maana hawaingii kubadili kila kitu, watakuta polisi ipo, mahakama, jeshi, Bunge, shule, vyuo, nk, maana yake wanaposema watafanya tofauti haimaanishi wataanza mwanzo Bali wataboresha baada ya miaka 5 tutawapima.
Kwakuwa CCM ina nguvu na pesa nyingi, baada ya miaka 5 mtatumia kila njia kurudi madarakani endapo upinzani utashindwa kutimiza yale waliyoyaahidi.
Ewe kijana, baba, Mama tuuchagueni upinzani. Kubaki na CCM au kuchagua upinzani haimaanishi tutagawana hela mifukoni, tutafanya kazi Kama siku zote.
Tuungane, tusiwadharau upinzani maana hatujawahi kuwapa nchi tukayaona mazuri na madhaifu yao.
#MakeTanzania great again