Uchaguzi 2020 Ushauri wangu kwa vijana na wazee wetu, tuchagueni upinzani tuone watafanya nini

Mtu anaweza kuwa na maendeleo bila vitu?

Hui ujinga wenu mmekaririshwa huko chadema
 
Tunahitaji Bunge litakaloisimamia Serikali vilivyo; tunahitaji Mahakama yenye kitendo haki sawa kwa kila raia na TUNAHITAJI RAIS KWENYE KUHESHIMU KATIBA NA SHERIA ZA NCHI.

LISSU NI JIBU
 
Huu ukweli huwa hawataki kuusikia
 
Tafuta nchi yako ya majaribio uwape hao waropokaji akina Tundu Lissu
 

Nyie dhamira yenu kuu ni RUZUKU.

Na safari hii inapungua JIPANGENI UPYAA na huyu mliomchagua ndo atawadhalilisha kabla jogoo hajawika.
 
Dah, safari bado Sana, huwezi amini hapa Kuna comments nyingi tu za wasomi ila wengine wanajifanya hamnazo, unaposema kuwapa upinzani Ni kujaribisha unamaanisha Nini? Magufuri aliwahi kuwa hata Katibu wa ccm wapi? Magufuri aliwahi kuwa Raisi wapi? Mwaka 2015 tulikuwa na wagombea wapya kabisa lakini tulifanya maamzi na matokeo yake ndiyo haya yaliyoleta kelele kwa watu wengi, Sina mashaka, ccm itashinda kwasababu ya ujinga wetu tuliojengewa na elimu ya kukalili, nimefurahishwa na michango isiyokuwa biased, kama upinzani una madhaifu ndani ya chama, waelekezwe watafanyia marekebisho, lakini tunaitaji sera mbadala, kwani ukiteseka kwa kuongozwa na upinzani ndo utaumia Sana kheri kuumizwa na ccm mpaka utakapokufa? Think beyond
 
Aisee ninyi mnaosema JPM kafanya mambo mengi sana hivi ni yapi hayo ya kutisha? Hivi atamshinda Kiwete aliyejenga shule za kata zaidi ya 1500 na akazipelekea walimu na maabara? Hakuna jambo jipya alilofanya JPM zaid ya stigaz goj! Haya mengine kama Flyover mbona zilikuwepo hata pale Manzese? Reli, madaraja na Ndege mbona zilikuwepo tangu awamu ya kwanza? Tofauti ni model na standard tu! Kwanza ukiungalia utawa wa JPM utaona wazi karibu 75% ya miradi iliyotekelezwa katika awamu hii ya miaka 5 ni ya wizara moja tu ya uchukuzi ambayo yeye alikuwa waziri wake kabla ya kuwa rais! Tuna wizara zaidi ya 10 alfu miradi ya maendeleo inabase kwenye wizara moja, Je hapo kweli tutafika! Iliishia wapi Tanzania ya viwanda iliyokuwa ikihubiriwa mwaka 2016? Vipi kuhusu miradi ya wizara kilimo, afya, Utalii,Elimu,Mifugo n.k ? JPM tulimpa nchi kwa kumjaribisha, lakini amefanya kazi zaidi kama waziri wa ujenzi na uchukuzi kuliko Rais na mwenyekiti wa baraza zima la mawaziri, Sasa ni wakati tumpumzishe tumuweke rais atakayetekeleza miradi kwa kufuata mizania!
 
Mtoa post umetoa ushauri mzuri sana na katika wakati muafaka! Mimi binafs huwa nafika mahala nafikiria dawa kubadili katiba kuweka ukomo wa chama kutawala isiwe zaidi ya miaka 10 mfululizo! Nadhani tukifika huko tutakuwa pazuri ila shida ni jinsi ya kuimplement hiyo sheria! Wengi hawafahamu faida za kufanya mabadiliko ya utawala mkongwe kama huu wa CCM;
Mojawapo ni hizi zifuatazo:
1.Kukipa chama muda wa kujitazama na kujitathmini upya kiutendaji na hivyo kujisahihisha kikamilifu. Siku zote mchezaji aliye ndani ya uwanja hawezi kujitazama vema makosa yake kuliko aliyekaa nje ya uwanja.
2.Kuimarisha nidhamu na uwajibikaji kwa chama chochote kitakachoshika dola kwani kwa kutambua kuna siku kitaondoka madarakani hivyo kitatekeleza ahadi na ilani yake kwa unyenyekevu na ukamilifu mkubwa tofauti na sasa ambapo chama kama CCM kimejivika fikra za kutawala milele na hivyo kubaki kutengeneza tu mazingira ya kuhakikisha kinaendelea kuwepo madarakani badala ya kutumikia wananchi.
3.Kudumisha misingi ya amani mshikamano na umoja wa kweli. Kuondosha chama kimoja madarakani na kupitia uchaguzi huru na wa haki, kunaepusha chuki miongoni mwa washindani na kuepusha mazingira ya kuhasimiana na hata kukwamishana kisiasa, na hivyo kuwa na umoja wenye tija. Zaidi ya yote kunaepusha nchi kuingizwa katika machafuko ikiwa chama kimoja kitaendelea kung'ang'ania madaraka huku kikipewa ushindi isivyo halali.
4.Kunaweka mazingira mazuri ya kujikita katika kuimarisha ujenzi wa uchumi imara badala ya kuwekeza zaidi kwenye propaganda za kisiasa. Hebu vuta picha hivi ule muda ambao shirika letu la utangazaji TBC kwa miaka yote 5 linautumia kutangaza vipindi vingi vya kipropaganda ungekuwa unatumika kutangaza matangazo ya biashara za wafanyabiashara na makampuni binafsi, si tungepata fedha nyingi tu tukaweza kusaidia shule zisizo na madawati kuliko ilivyo hivi sasa?
 
Dah....bora tujaribu kwa Hashim Rungwe....tuanze kula wali kuku 🤣 🤣🤣
 
Kama mabeberu wamewahi kuziacha nchi za kiafrika kujitawala basi ccm itashinda tena kwa wiz wa kura lkn kama hawajawahi kuziacha hizo nchi za kiafrika basi ccm mwaka huu chali iwe Jua iwe mvua
 
Sasa kama.hajaprwa nafasi unataka ulione wapi alilofanya. Ndio maana Pazia kasema ili uone atafanya nini mpe nafasi.

Hongera Pazia kwa bandiko zuri
 
Aacha kulisha maneno mleta uzi,majaribio umesema wewe, walioanzisha mfumo wa vyama vingi si wajinga ila walafi na wezi ndio wanauchukia, mwanafunzi mjinga siku zote uchukia aliyebuni mtihani.
 
Sio Jambo baya kuchagua upinzani lakini kwa Sasa wakurupukagi ni wengi kuliko viongozi.
Tumewapa ccm wamekurupuka kwa miaka 60 hadi leo madawati mashuleni bado mo mtihani.
 
Naungo mkono hoja ccm wakagombe umiss siasa zimewashinda tumuachia Lissu tuone itakuaje
 
Wananunuliwa kama njugu.
Kwa sasa hapana labda 2030. Kura yangu kwa Mzee Magu
 
Acha utoto wewe nchi hii haiongozi kwa mazoea Kama unavofikiria wewe eboooo!😬😬, tunachagua kiongozi mwenye kutufikisha kwenye nchi ya ahadi na siyo kumuonea huruma mtu eti atuongoze kwa kujaribu damn!
 
Paskali wewe kwa uelewa wako huamini kuwa uzur I wa kitu huthibitka baada ya kuleta kitu kingne..kama umezoa kutumika desktop kumpyuta hivyo huweza kubali mpakato kwasabb desktop umeizoea? Paskali usiniangushee!!
Na kama ndvo huamini kwamba democrasia ni chachu ya mabadiliko na maendeleo?nakupa mfn. America ni nchi ilyokuja kuendelea baada ya kufanya mabadiliko ya uongozi kwa mara nyng . kuna Rais America alibadilisha nchi for 100 days!! Japo sikumbuki ni Lincoln or nani. Mifano iko mingi.
Hatuwez kuwa wasomi tusiotaka kubadilika na tukashindwa kukubali ukweli!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Ushuzi mtupu
 
Subiri kwanza Jiwe amalize miaka mingine mitano mkuu, then we'll see. Kwa sasa Magu all the way till '25.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…