Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Atakae dharau VETA haijui vizuri.

Nilipomaliza kidato cha 4 na rafiki yangu me nilifauru vizuri tu yeye akapata 0 kabisa yani sio 4 ni SIFURI.

Me nikaenda alevel PCM yeye akaenda VETA kusomea mambo ya umeme.

kwasasa me nipo mtaani na degree yangu, ila yeye yupo TBL karume pale anakunja milioni na chenji na malupulupu kibao.

NAKAZIA: Ujuzi ndio unaitajika sio degree
 
Zero IQ
 
Ulienda kusomea degree ya nini?
 
Elimu ya chuo ina umuhimu wake tena sana at the managerial level. Watu wanachukulia poa diploma na degree sababu bado hatujaanza kuexpirience shida ya managerial workforce. Ulaya huko wanahitajika balaa.

Ukitaka kujua umuhimu wa degree anzisha biashara halafu ianze kukua halafu hauna elimu ya level ya degree especially eneo la biashara. Utajua haujui.
 
Wewe unakwenda kinyume na ahadi ya mwana TANU. Moja katika ahadi 10 za mwana TANU inasema, nitajielimisha kadri ya uwezo wangu kwa manufaa yangu na ya watu wote.
Wacha watoto wakale Boom!
 
sasa Ulisoma PCM, then chuo kikuu ukaenda kusomea nn?
 
Hapo cherehani toeni kwa kweli labda uwe fundi haswa ndo utapata wateja ila hawa wa kubana nguo wa bukubuku utapata hela ya mboga tu na mafundi cherehani wamejaa wa kutosha
 
Punguza ushauri kweny maisha ya watu
 
Mawazo mazuri hupotezwa na dira yenye fikra ndogo,, niamini boss umetoa mawazo ambayo mpingaji ni mjinga aliyeshiba kufanikiwa,, upo vzriiii huu Uzi utadumu!
Kiuhalisia jamii forum ilitakiwa iwe na vitu direct kama hivi,hali ni yeye mtaani biashara zimajaa kuliko wanunuzi ujuzi tuu ndo utatuokoa, jingine vijana wakimaliza degree wasave pesa baada ya mafunzo ya veta lakini wampeleke mmoja china ili tuanze kuund vitu vyetu vya moto
 
Degree ni muhimu sana ila ujuzi wa ziada una manufaa yake na hapo ndipo veta inapokuja kuwa na faida.
 
Kama ni hivo Mkuu wewe utakuwa miongoni mwa binadamu wachache wenye roho ngumu kama Adof Hitler πŸ˜‚πŸ˜‚... Japo si kwa ubaya lakini si kazi rahisi kwa zaidi ya 99% ya tulio wengi. Hongera sana kwa kuangalia na kuitikia ndoto na kurisk kiasi hicho mkuu.
 
Huu uzi upewe 5 🌟
 
Uzi makini mnoo. Mtoa mada Mungu akubariki sana kwa kututoa tongotongo maana ulichoandika hapa ni ukweli mchungu binafsi yamenitokea. Baada ya kumaliza chuo kikuu mwaka wa tatu sasa sijapata ajira ila naona madogo wenye ujuzi kitaa wanavyopiga bingo tena kwa gharama haswaa.. Assume mtu kushusha engine ya pikipiki tu anataka 50,000 hapo bado ya ufundi.
Watanzania tuamkee...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…