Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Ushauri wangu kwa vijana wa kidato cha 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya Chuo Kikuu

Ningependa kujua hio Engineering science inahusu nini mbona wameiweka kwa kila fani na hio technical drawing mkuu?

kinachohitajika kama graduate anaweza akitoka hapo kufanya fani husika, ndicho kinachohitajika,mengine mbwembwe...lol
Engineering scince ni physics lakini imeongezewa vitu kidogo

Technical drawing ni somo la michoro

Kwa kifupi haya masomo sio mbwembwe yana muandaa mtu awe fundi mzuri sana na ndio maana ukiwa na level 3 ya Veta utaitaji d mbili za masomo yoyote kasoro ya dini mfano civics na english kusomo uinjinia level ya diploma kwa sababu level za Veta 1,2,3 tayali zimebeba masomo ya scince ambayo unge itaji kuwa nayo cheti cha form 4 au form 6..
 
Engineering scince ni physics lakini imeongezewa vitu kidogo

Technical drawing ni somo la michoro

Kwa kifupi haya masomo sio mbwembwe yana muandaa mtu awe fundi mzuri sana na ndio maana ukiwa na level 3 ya Veta utaitaji d mbili za masomo yoyote kasoro ya dini mfano civics na english kusomo uinjinia level ya diploma kwa sababu level za Veta 1,2,3 tayali zimebeba masomo ya scince ambayo unge itaji kuwa nayo cheti cha form 4 au form 6..
Nimekuelewa mkuu, mimi naona watakaosoma uinjinia ama wanaotaka kuwa fundi ndio watakaofaidika na hio course ya Engineering science, kuiweka kwa kila fani ni uonevu,nimekubaliana na mengine yote,English,Computer,Maths kuwekwa kwa kila fani ila sio hio...😎
 
Ushauri wangu kwa vijana wa form 6 na wengine wote ambao bado hawajafikia elimu ya chuo kikuu.

Tanzania ya sasa haihitaji Degree, zimeshakuwa nyingi sana mtaani mpaka copy za vyeti zinafungiwa vitumbua. Yaani degree ni luxury sio hitaji muhimu.

Tanzania ama dunia ya sasa inahitaji stadi na ujuzi, ambao mfumo wa elimu yetu haujauweka kupatikana chuo kikuu. Yaani huwezi kwenda chuo kikuu ukapata degree ya kupaka rangi kwa mfano. Na kwa kiasi kikubwa ujuzi huu unapatikana VETA. Watu wengi huwa wanadharau kwa kuchukulia kama ni njia ya waliofeli shule.

Hata hivyo kutokana na maisha yanavyoenda, elimu ya chuo kikuu ni kipimo cha daraja la elimu tu kama ilivyo darasa la saba, form 4 na form 6 na unahitajika kuwa na kitu kingine nje ya hivyo ili uweze kufanya kitu. Hasa ikiwa umetoka moja kwa moja Form 6, ndo una hali mbaya zaidi.

Lakini kama utaamua kujitengea miaka miwili au mmoja kabla ya kwenda kujiunga na hiyo elimu ya ndoto yako. Ukaenda VETA na kusomea ujuzi tofautitofauti kama udereva, umeme wa magari, umeme wa majumbani, ujenzi na ufundi wa vitu vya aluminium nk.

Basi utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanikiwa kimaisha popote ulipo na hutolala njaa kwa kukosa ajira kwani utakuwa na vyeti zaidi ya vitano vya ujuzi vitakavyokuwezesha kupenya sehemu nyingi sana kuliko namna ambavyo cheti chako kimoja cha degree kinavyoweza. Na kwa ujuzi huo utaweza kujipatia pesa za kujisomesha hiyo degree muda wowote utakaotaka. Ni vigumu kulala njaa ukiwa na elimu ya VETA, ila uwe na uhakika kuwa utalala njaa ukiwa na cheti cha degree kabla hujapata ajira. Kitu ambacho ni kitendawili.

Ukweli ni kwamba, kama una uhakika wa ajira yaani kuna mahala umeandaliwa, au kuna mtu wako yuko ofisi fulani na atakuwepo mpaka muda utakapomaliza kusoma hiyo degree, basi kasome. Kama huna uhakika basi nenda kwanza VETA. Wengi wanaopata ajira huwekwa na watu wao, au kuhonga mishahara yao mmoja au miwili ya awali ili kuajiriwa.

Hata utakapomaliza maisha ya mtaani yatakulazimisha na yatakudai ujuzi au stadi fulani utakaopaswa kuwa nao nje ya hiyo degree yako ili ujiingizie kipato. Na ndicho ninachokisema hapa. Kwa bahati mbaya hutakuwa nao, na hutakuwa na uwezo wa kusoma VETA tena kwani hela ambayo ungeweza kuitumia kama mtaji wako wa kujipatia ujuzi huo utakuwa umeimaliza kwenye degree.

Elimu ya VETA ina uwezo wa kukusomesha degree, ila elimu ya degree ni vigumu mno kukusomesha kama bado hujapata ajira. Ni rahisi kujiajiri ukiwa na elimu ya VETA ila ni ngumu sana ukiwa na degree. Kwani utahitaji mtaji, na huo mtaji ndio utakuwa umeutumia kusomea degree. Kwa hivyo utakuwa mtaji huna na ujuzi huna, na itakuwia vigumu sana kujitafuta. Hapa wadada wengi waliohitimu ndio hudanga kusiko kawaida na wa kiume kupinduka na bodaboda kukimbilia abiria wapate hela nyingi ndani ya muda mfupi ili waache kazi hiyo.

Na uzuri wa kuya face maisha kwa ujuzi na stadi utakazopata VETA, ni kwamba utakuwa na uzoefu na namna ya kukabiliana na maisha ya mtaani na kikubwa zaidi utatambua wazi ni aina gani ya degree inayohitajika mtaani kwani vijana wengi huchagua degree kwa kutazama uzuri wake wa kutamkwa mdomoni. Ukitoka na cheti chako cha chuo kikuu hapa Tanzania ukaenda nchi za ughaibuni, kuna uwezekano mkubwa ukahitajika kusoma tena au kujiboresha kwa elimu watakayokupa wenyewe.

Yaani kwa kifupi, elimu yetu haiaminiki. Na ndio maana watoto wa viongozi na watu wenye pesa husoma nje ili kuepuka hili. Lakini ukitoka na Vyeti vyako vya VETA hata vikachanwachanwa, ujuzi wako utaongea. Na popote pale utapata nafasi, kisha utajisomesha hiyo degree.

Nimeandika kwa uzoefu wangu, na degree yangu niliyonayo ikiwa ni mwaka wa tatu tangu nihitimu na sijui hata interview inafananaje. 😀. Kabla sijaenda chuo niliambiwa karibia kama hivi nilivyoandika hapa, sikutilia maanani sana, na nikasoma degree kwa cash zaidi ya milioni 11, yaani ada pamoja na gharama za kuendesha maisha ya chuo baada ya kukosa mkopo. Mzazi asingenipa pesa hizi nikajiajiri, na sikuwa na lolote kuhusu kujiajiri. Mimi nimejitahidi hapa kuyanyoosha zaidi kwa vijana wenzangu.

Jitathmini kisha utajijibu. Ukiparamia degree, utakapomaliza hata hela za vocha utagongea kwa washkaji zako walioenda VETA na hao ndio watakusave vimeo vyako vyote. Hutaamini. Sikukatishi tamaa, ndio ukweli.

Kwa kifupi, degree imekuwa sio kitu cha kuanza nacho mtaani yaani ni lazima uwe na kitu kingine kwanza kisha ndio uongezee na elimu ya degree. Wanaonufaika moja kwa moja na elimu hiyo ni wale ambao tayari wako kazini, wanaenda vyuo kuongeza elimu kisha kurudi kazini kupandishwa vyeo. Sio mtoto wa form 6 au diploma.

Lakini kama umebahatika kupata mkopo, nenda kasome ila hakikisha unajinyima sana na hela zako una save ili utakapomaliza upate ada ya kwenda VETA kujiongezea kitu cha ziada au kufungua biashara yako binafsi lakini sio ajira. Na hata kama utatafuta ajira utahitaji nauli za kunguka mjini, hata ukipata sehemu ya kujitolea bado utahitaji kujigharamia kwa karibu miezi 6.

Mzazi hatokupa gharama hizo, kwani wazazi wetu wengi mkataba wao wa kukugharamia huishia siku una graduate. Baada ya hapo huanza kukutazama wewe sasa namna utakavyoweza kurudisha fadhila. Baada ya graduation hakutakiwa na pocket money wala boom la serikali.

Semester 6 au 8 ni muda mchache sana, lakini una mambo mengi na graduation halisi ni kurudi mtaani si ile ya kuvaa joho.
Niliwahi toa wazo kama lako kwa vijana flani ambao walirudi chuo wakaunda kundi la utanashati na kupenda mademu.. nazani watanikumbuka..
 
Umeongea mambo ya msingi sana bahati mbaya vijana wenyewe wapo busy kwenye porojo za bandari.
 
Huu uzi mods wauwekee pin ili vizazi viusome jamaa kamaoiza kila kitu japokua kuna paka wana roho ngumu humu hawawezi kukuelewa

Labda nifupishe uzi wako kwa maneno haya machache.....

Elimu itolewayo VETA/SIDO kwa nchi za ulimwengu wa kwanza ndizo haswaa elimu za vyuo vikuu NA elimu zitolewazo vyuo vikuu huku kwetu mostly ndio elimu za sekondari msingi na nasari huko laya
 
😂 😂 😂 Mkuu usitutanie bhana
Najua huwezi amini kwasababu hunijui,ila huo ndy ukweli wangu sipo hapa kupotosha au kudanganya wengine.

Niliacha chuo mwaka wa tatu semista ya pili and then life is good.

Bado naamini pesa ndiyo elimu yenyewe kunasiku jamaa mmoja ana masterdegree neurosurgery pale muhus nilimsimulia huu mkasa akasikitika sana lakini sometimes nampiga tafu kwenye mambo ya fweza.

Akisoma hapa atanijua.
 
Kuna watu wanasoma combination ya Physics, mathematics na Computer science form 6 pale, mi nawashauri Hawa waliosoma hii kombi, miezi hii mitatu minne wajibrush YouTube kwa content za Computer science kiundani then, afanye kazi Upwork na freelancer.

Atasahau habari za chuo kabisa.

Yaani aliyeanzisha combination ya Physics, mathematics na Computer science abarikiwe. Hii ndo ya kujiajiri Sasa.
Mkuu, hii kombi ipo shule gani
I wish ingekuwa enzi zangu ningeipiga hii
 
Nimekuelewa mkuu, mimi naona watakaosoma uinjinia ama wanaotaka kuwa fundi ndio watakaofaidika na hio course ya Engineering science, kuiweka kwa kila fani ni uonevu,nimekubaliana na mengine yote,English,Computer,Maths kuwekwa kwa kila fani ila sio hio...😎
Hilo somo ni muhimu sana kwa sababu fani asa za umeme bomba magari chelehani uchomereaji ujenzi lina kuwa na umuhimu wake ila uzuri ukifika level 3 lina kuwa halipo
 
Nadhani hapa umezingatia zaidi upande wa familia zinazojiweza.

Ni mzazi gani maskini mwenye uwezo wa kumsomesha mtoto chuo (kama amekosa mkopo) kisha tena ampeleke VETA?kama umesoma vizuri jamaa amesema option iwe kwanza VETA then baadae huyu muhitimu arudi mtaani achunguze cha kwenda kuchukulia degree chuo ili aende akiwa tayari ana uwezo wa kujisomesha
Nilichogundua humu ni kuwa baadhi wanasoma kumaliza tu na siyo kusoma kuelewa, maana mada imenyooka sana hii.
 
Daaaaaaaaaah,! Hi inaitwa "KULA CHUMA HICHO".

Mwenye akili mtambuka,hatahoji Mara mbilimbili.
 
Nitakuwa wa mwisho katika watu zaidi ya bilioni 7 waliopo duniani kukubaliana na hii hoja ya mleta uzi. Kusema vijana waache kwenda kusoma degree ili waende VETA kwanza ni ufinyu wa fikra na kukata tamaa. Ni sawa na wale wanaosema hela sio kila kitu huku hawajawahi zishika za kutosha. DEGREE NI MUHIMU KULIKO CHETI CHA VETA. Degree itakusaidia kufika ambako mtu wa VETA hawezi fika.

Tusipotoshane kwamba degree haina maana. Kama kwa nchi maskini kama yetu degree haitakuwa na maana basi huko Ulaya na kwingine kulikoendelea inabidi wafunge tu vyuo. Bado kwa nchi yetu tunahitaji wasomi wengi. Haya mabadiliko tunayoyataka yatapatikana haraka kukiwa na wasomi wengi. Kijana mwenye ndoto za kuwa daktari bingwa aache kwenda MUHAS ajiunge VETA? Aisee acheni kukata tamaa. Kama wewe bado maisha hayajakaa vizuri usitake kupotosha vijana. Zamu yako ikifika hata wewe utafanikiwa.

NINAWASIHI VIJANA WAUPUUZE HUU UZI NA KUCHANGAMKIA DEGREE HUKO UDSM, MUHAS, SOKOINE, SAUT na vyuo vingine vinavyotoa degree. Ila pia wasiridhike na degree peke yake. Wajiongeze na maarifa mengine.
Kama wanataka pesa za chapuchapu angewashauri wawe bodaboda maana unajifunza Leo kesho uko road unakula vichwa
 
Back
Top Bottom