Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
.
Sasa mkisema haya maswala yanatokana na Zitto mwenyewe wakati ni player mzuri ktk team na hamna namba tatu mwingine au mshambuliaji kwa kiwango chake, well mtafungwa mengi sana na ndicho CCM wanakitaka.....Kumbuka tu huu ni ushauri wetu sote kwa sababu tunampenda sana..
Naelewa sana unachozungumza na ndio maana nimeiweka hii mada kwa Zitto kwa sababu team player haiwezi kuwa kiwanjani tu huanzia dressing room ambako mkuu wangu anavurunda sana wakati mwingi..But he is still a good player kama Tavez au Balotelli wa ManCity anahitaji support zaidi ya kashfa.Hilo la team-player limeongelewa mara nyingi sana Mkandara. and I still sense some difficulties ahead.
Zitto Anafanyiziwa na katibu mkuu wake....wabunge wa chadema wenye mlengo mmoja na mwenyekiti wameungana kutaka kuangusha ngome ya zitto hata kwa unafiki na uzandiki..lakini jamaa yupo strong ile mbaya
Mkandara,
Nakuunga mkono sana katika ushauri wako huu.Huku tunakoelekea i kuzuri.siasa za maridhiano kabla chama cha upinzani hakijaingia madarakani zinafifisha nguvu ya kuipinga na kuishinikiza serikali.
Ukifanya kazi ya maridhianao na serikali hiyo unataka irekebishe makosa halafu nafasi yako ya upinzani inakuwa irrelevant.mimi ni muumini wa falsafa ya mwanamapinuzi wa ufaransa na Ulaya napoleo bonaparte kwamba 'never interrupt your enemy when he's making mistakes'
Pia tujikite sana katika itikadi.kama kuna chama tunatakiwa kushirikiana nacho kama wapinzani ni vyama vingine vyenye sura ya radical reform katika focus yake na sio chama tawala.Simaanishi upinzani wa kupinga kila kitu but pia upinzani wa kuipongeza serikali katika mabo kadhaa lakini kimkakati.Siyo pongezi zinazokuondolea justification yako ya struggle na kuwashawishi wananchi waiondoe serikali hiyo madarakani.sifia kisera,walime kisera kwa akiba kubwa ya hoja ulizojiwekea kupambana na chama hasimu
Sasa hapa ndipo mnapokosea nanyi.. Chama ni team players hakuna cha Zitto na matatizo yake. Anapoumizwa Zitto ni lazima myasikie machungu yake hata kama yeye ndio njia ya mkato..
Mpirani maadui wakijua namba tatu ndio njia ya mkato inatakiwa formation ya ulinzi ubadilike, namba saba anashuka kusaidia na namba sita vile vile anacheza zaidi half ya kushoto mnaposhambuliwa..Hii inasaidia kutofungwa magoli maana ushindi wa Soccer/Football hutokana kwanza na kutofungwa.
Halafu pia mkiwa na mshambuliaji mzuri sana lazima yeye atapewa maadui wengi zaidi na pengine hata kukwatuliwa atolewe nje ili oppositon team ipate kufanya wao mashambulizi.. Kumbuka Mechi ya Italia na France alipoondolewa Zidane.. Ilikuwa imepangwa japokuwa ni makosa ya Zidane, Italia ilikosa Ushindi..
Sasa mkisema haya maswala yanatokana na Zitto mwenyewe wakati ni player mzuri ktk team na hamna namba tatu mwingine au mshambuliaji kwa kiwango chake, well mtafungwa mengi sana na ndicho CCM wanakitaka.....Kumbuka tu huu ni ushauri wetu sote kwa sababu tunampenda sana..
The only person who cannot learn anything is the one who already is convinced that he knows everything.
Kula kubwa
Hili ni tatizo la viongozi wetu Afrika na TZ nasikia hata mkuu wa kaya naye anajua kila kitu. Viongozi wetu hawana washauri kutokana na mahitaji, wanajiona wanajua kila kitu. Ninaamini hata CDM ingekuwa na washauri wazuri kwenye nyanja zote na wanaoweza ku-forecast future matatizo ya akina Zito yangekuwa historia. Hatu-vet viongozi wetu tunawapachika tu sio wote wanafaaa kuwa viongozi hata kama wanaongea kama vinanda.
Hakuna mtu anamfanyizia Zito ndani ya CDM, matatizo yote kayaanzisha mwenyewe, ninsingependa kumnanga hapa wala wale. Ila kwa picha kubwa angalia kwanini Zito haivi na yeyote ndani ya chama ila inaiva na JK na watawala wa CCM, je kwanini usijiulize wakati wengine wako kwenye harakati yeye yuko na watawala.Zitto Anafanyiziwa na katibu mkuu wake....wabunge wa chadema wenye mlengo mmoja na mwenyekiti wameungana kutaka kuangusha ngome ya zitto hata kwa unafiki na uzandiki..lakini jamaa yupo strong ile mbaya
Sasa ktk swala la Zitto Kocha ni nani? maana najua yeye na Dr.Slaa hawana matatizo isipokuwa matatizo yako dressing room..Au ndio ya Azam kumuuza mchezaji kwa sababu alivaa jezi ya Yanga na kocha pia kwa kumpanga mchezaji wa Yanga!.Mkandara
Makocha wazuri hata uwe mchezaji mzuri kiasi gani ukishindwa kufuata formation ya mchezo anavyotaka yeye unawekwa bench. Hakuna mcheza mzuri kama hashirikiani na team kushinda. Siasa sio mtu mmoja na mafanikio ya siasa huletwa na kikundi kikubwa chenye mawzo na malengo yanayofanana, sidhani kama Zito anamalengo ya muda mrefu na CDM, na inawezekana amefanikiwa alichokuwa anakitaka sasa yuko kwenye mission nyingine.
Sasa ktk swala la Zitto Kocha ni nani? maana najua yeye na Dr.Slaa hawana matatizo isipokuwa matatizo yako dressing room..Au ndio ya Azam kumuuza mchezaji kwa sababu alivaa jezi ya Yanga na kocha pia kwa kumpanga mchezaji wa Yanga!.
Hapa umenena,
Sasa Kijana mwenzetu ameamua kufanya kazi na watala na anaamini kwa kupitia kwa JK ataingia ikulu sijui kwa tiketi ya CDM au CCM anajua yeye. matamko yake na mwenendo wake umekuwa wa kiccm na hawezi mpinga JK kisera hata mara moja siku zote hata JK akikosea anaona sawa fuatilia.
Duh sasa mwenzangu unachapia.. Chama leo ndio kimekuwa kocha tena? haya na Team itakuwa nini?, sema ukweli pengine Chadema haina kocha as a team?..tunapuyanga tu mpira wa vumbi kidongochekundu!.kocha ni chama, wanachama na katiba ya chama sio mtu kwani wote watapita ila chama kitakuwepo. Ieleweke kuwa pamoja na mitizamo na matendo ya Zito bado anao wengi wanamwamini na yeye anaamini hivyo, ila kwenye safari hii ndefu na ya kupokezana vijiti naona ameamua kucheza mpira anavyojua yeye na ndani ya viongozi wa chama wanamtazama kwa mshangao bila kuwa na la kusema. Tetesi za rushwa dhidi yake hazijaanza jana inawezzekana kwa sababu ya misimamo yake kuyumba na kubadili position kila mara ndio maana anashukiwa au kweli ana kula au vyote au hali ila ni mazingira tu. kuyumba kwa misimamo yake hasa kwenye mijadala ya kisera inatokana na yeyye ama chama kutoshikiana kwenye matatizo ya kisera nje ya chama na mapambano ya kwenda magogoni.
Zitto Anafanyiziwa na katibu mkuu wake....wabunge wa chadema wenye mlengo mmoja na mwenyekiti wameungana kutaka kuangusha ngome ya zitto hata kwa unafiki na uzandiki..lakini jamaa yupo strong ile mbaya
Zitto ni makini ila mapungufu machache kwa wanasiasa tunaweza kuyarekebisha.Ni role model wa wanasiasa vijana wengi
Mkuu wangu binafsi yangu sidhani kabisa kwamba Zitto anasukumwa na tamaa ya Pesa - Hapana.. sio kweli kwa sababu namjua Zitto japo sii kwa saana hivyo. Sii mla rushwa tena nadhani anapiga vita rushwa kuliko watu wengi sana hata ndani ya chama chake mwenyewe hupenda kuhoji matumizi ya chama..Ni mtu safi sana inabidi uwe naye karibu ndio utamjua..
...
Siasa anazozifanya mh.zitto ni vigumu kwa ww uliyenje na moyo wa chama kutathimini..zitto amezungukwa na simba kila kona.simba wanasaka mbuzi wote na watoto wake..zitto na mwenyekiti +katibu ni tofauti kisa zitto anaonekana amekuwa na nguvu za kisiasa ghafla ndania ya chama
Zitto ni makini ila mapungufu machache kwa wanasiasa tunaweza kuyarekebisha.Ni role model wa wanasiasa vijana wengi
Sasa hapa ndipo mnapokosea nanyi.. Chama ni team players hakuna cha Zitto na matatizo yake. Anapoumizwa Zitto ni lazima myasikie machungu yake hata kama yeye ndio njia ya mkato..
Mpirani maadui wakijua namba tatu ndio njia ya mkato inatakiwa formation ya ulinzi ubadilike, namba saba anashuka kusaidia na namba sita vile vile anacheza zaidi half ya kushoto mnaposhambuliwa..Hii inasaidia kutofungwa magoli maana ushindi wa Soccer/Football hutokana kwanza na kutofungwa.
Halafu pia mkiwa na mshambuliaji mzuri sana lazima yeye atapewa maadui wengi zaidi na pengine hata kukwatuliwa atolewe nje ili oppositon team ipate kufanya wao mashambulizi.. Kumbuka Mechi ya Italia na France alipoondolewa Zidane.. Ilikuwa imepangwa japokuwa ni makosa ya Zidane, Italia ilikosa Ushindi..
Sasa mkisema haya maswala yanatokana na Zitto mwenyewe wakati ni player mzuri ktk team na hamna namba tatu mwingine au mshambuliaji kwa kiwango chake, well mtafungwa mengi sana na ndicho CCM wanakitaka.....Kumbuka tu huu ni ushauri wetu sote kwa sababu tunampenda sana..
Mkuu wangu samahani sana kwa haya nitakayo changia kwa sababu nadhani umetoka nje ya mada yetu. Hapa nia yangu ilikuwa kumkanya Zitto kwa makosa anayoyafanya nyuma kisiasa, kwa fikra zake anafikiria ama kukidhania yeye kinasimamia maslahi ya wananchi basi atafuata mkondo wowote anaodhani una malengo mazuri..Mkuu Mtoa mada/wewe hajasema kuwa jamaa ni mla rushwa na wala rushwa si kigezo pekee cha kupima uadilfu wa mtu.Zitto hawezi kuwa mpinzani wa wapinzani na akabaki friend wa upinzani.He is an enemy of ccm enemy and that make him CCM`s friend than CDM compatriot.
Zitto amejidanganya kuwa alikuwa akiwaconfuse wana CDM ila hapa yeye ndio anonekana kujidanganya na kujichanganya zaidi.
Na sasa ni wazi kuwa ameshaenda mbali sana kiasi cha kuwapa CDM nafasi nzuri ya kumtema tena bila kumpa nafasi ya kugombea vipindi vijavyo.
Zitto si masikini tena kama watu wanavyofikiri, labda kama wanamaanisha kuwa umasikini wa fikra haujamtoka.Maisha yake yanajisema wazi kuwa si masikini wa hela tena.
Ndugu umejaribu ingia katika mtego wa ajabu.Normally huwa hatuguarantee binadamu kuwa ni mwadilifu muda wowote unaokuja na miaka mingi ijayo.Kama kubadilika kwa kwa imani, kupata pigo la kisaikologia kama kuachika na mpenzi etc kunaweza mbadili binadamu na kuwa kitu cha ajabu, sioni sababu ya kushupaa kutaka sadikisha watu kuwa Zitto ni mwadilifu hadi sasa na hadi kipindi CDM wanachagua mwakilishi wao.Kwanza Zitto anaweza asiwe na nguvu Kigoma yenyewe kama anavyodhani leo.Kura zake zilizompitisha kuwa mbunge zinajisema zenyewe kuwa si lazima umaarufu wake uwe unapanda.
Zitto tayari keshapanda mbegu kwa wana CDM walikuwa wakimwona katika kampeni.Hakuwa aki enjoy raia masikini walivyokuwa wakiruka na kucheza midundo na performance live za mr II.Alionekana wazi kuwaona raia masikini waliokuwa wakijipa matumaini kwa kushangilia nyimbo za sugu km vile wenda wazimu na wanapoteza muda huku akitabasamu kwa dharau.Nilimwangalia sana katika show za Arumeru.Hakuonekana kupenda kuwajali sana watu wachafu wala kufurahia attantion za wana CDM wengine ambao pengine anawaona ni junior kwake.Na wala hili halina na ubishi kwa wanaoujua saikologia na kufahamu gesture mbalimbali za mtu.
Tuache ushabiki Zitto kateleza na this time kateleza vibaya .Kama ni mbegu ya mashaka keshaipanda na kaiweka maji imeshaota na kukua.Na ajue akicheza itampasa aachane na siasa na kwenda fanya business nyingine,alizozisomea.Nani hajui alivyokuwa akishupaa wakati wenzie wakitoka katika bunge.Nani hajamwona anavyojipambanua kwa mambo yasiyoridhisha na kinyume na CDM.Miongozo yake wakati bunge likianza ilikuwa ikiboa, alikuwa kaisimama hovyo kama mtoto king`ang`anizi anayetaka onyesh akuwa kazoea bunge na pengine ni kama senior katika bunge.Lakini time zilivyoenda kaonekana si kitu ch atofauti sana katika cdm.Representation ya Sugu, Mnyika , na vijana wengine imekuwa nzuri sana kiasi na kama ni uzalendo hapiti yeyote hapo juu.Na asidhani kuwa ana chochote cha kisiasa ambacho anaweza mpita nacho JJ Mnyika.Labda fani za taaluma zao ambazo ni tofauti.Soon hata hao watu wa kigoma anaowatumia kulalamika nyuma yake ajue kuwa kura zao ni sehemu ndogo ya watanzania.Na sijui hata kama CDM watatikisika kwa hilo jimbo kwani NCCR wana option ya kuwazawadia CCM.
Pole Zitto ulipojiweka hakuna atakayekuamini tena hata ukijirudi na kutubu.Utabaki kama Malecela ndani ya CCM.
hata mimi nia ni kumkanyaMkuu wangu samahani sana kwa haya nitakayo changia kwa sababu nadhani umetoka nje ya mada yetu. Hapa nia yangu ilikuwa kumkanya Zitto kwa makosa anayoyafanya nyuma kisiasa, kwa fikra zake anafikiria ama kukidhania yeye kinasimamia maslahi ya wananchi basi atafuata mkondo wowote anaodhani una malengo mazuri..
Issue hapa si kuwa nani si mchafu ama nani ni msafi zaidi na hivyo zitto hawezi ichukua kama claim ya kumtoa katika haya anayoonywa.Hiyo haitokuwa logic.Kama Zitto anataka blackmail CDM atakuwa ameanguka na atakuwa amethibitisha kuwa anahitaji kusoma logic,kabla ya kuutaka ujemedari mkuu.NAPATA KICHEKESHO KUWA NA PRESIDENT ANAYETAKIWA AWAJIBIKE KWA MATENDO YAKE HALAFU ANAPOTEZA MUDA KUNYOOSHEA MIKONO WATU KUWA NAO WAMEKOSA NA HIVYO AIULIZWE.nilitegemea pia nawe ungesema kama kuna wenye makosa basi angeyatibua kabla ya yeye kufanya hayo ayafanyayo huku akihifadhi ya wengine kama tool ya kublack mail.Hii inaonyesha hata katika rushwa anaweza kuwa keshazama kwa imani kuwa naye atalipuwa wengine.Na hapa huo uzalendo wa chama na Nchi hauna mshiko kwani hii dhana inautengua.Na hata ukimsikia ktk majibu yake mengi hutumia maneno haya ya kujiamini yeye pekee kwa kila anachokifanya ama maamuzi anayochukua, kumbe Kisiasa ni makosa makubwa sana, na hasa kwa nchi za Kiafrika unajimaliza kisiasa. Ni sawa na mwanamke/mwanamme alokuwa kwenye ndoa anaamua kufanya atakavyo kwa sababu he/she think of their personal rights of being independent..Unapokuwa katika ndoa kuna mambo lazima uyaache na kuna marafiki inabidi uwaache. Huchaguliwi marafiki lakini unashauriwa kuwa makini single friends wanaokuvuta kwenda Nyumbani Lounge bila mwenza..
Hii ndio logic behind, kumnasua Zitto ktk kiza lakini hakuna ukweli wowote kwamba Zitto ni mla rushwa. tena naweza sema kuwa na mashaka na watu wengine ndani ya Chadema kuliko Zitto japokuwa kwa Bongo yetu sidhani kama kuna mtu hata mmoja ni MSAFI niseme SAINT - Hakuna, alikuwa Nyerer naye kisha kutoka.. Jamani tusidanganyane, hali ya maisha na mfumo uliopo leo hii TZ huwezi kumpasa mtu msafi kabisa kabisaaa ambaye akaingia uongozi au Ubunge kwa usafi na anategemea atabakia mbunge kwa usafi wake wakati nchi nzima ipo ndani ya bomba la majitaka (sewerage system)... Inawezekana kweli?..mimi nina mashaka..sasa haya ya kumsingizia Zitoo mla rushwa wakati sii kweli na anajaribu kuwafahamisha hamtaki kujua yeye afanyeje? mnataka Zitto avue nguo zake kuwaonyesha ukichaa ndio muweke imani naye...Tena amini maneno yangu ningekuwa Zitto ningwambia ile Hotel Dodoma yangu, Nina majumba Dar Kigoma na kwingineko, leteni ushahidi zimetokana na rushwa..
Katika haya ya RUSHWA ni lazima mfahamu ya kwamba CCM wanataka WanaChadema muendelee kumchukia ZItto, utengano wetu utaanzia kwake na sijui kama umenielewa uliposoma Utangulizi wa kichwa cha mada..Kama Chadema itamfukuza Zitto ama kuendelea kumsodolea kidole, itafika mahala aidha yeye kujitoa ama Chadema kumfukuza na nakuhakikishia Kama Zitto ataondoka Chadema kama wanavyotaka CCM.. Amini maneno yangu 2015 uchaguzi mkuu usikieni ktk magazeni na Tv.. Chadema itaporomoka kama CUF 2010 kumbuka hawakudhania kwamba itatokea hivyo hadi uchaguzi waliendelea kuamini wao ni mbadala..Na Zitto hawezi kuifanya kazi nje ya CDM huo ndio utakuwa mwisho wake kisiasa.. aamini maneno yangu atakuwa Mbatia au Jussa wa Chadema, kuingia Ubunge kwa hisani ya rais au baraza la wawakilishi..
CCM wanataka Chadema kisambaratike kupitia Zitto na inaonekana mnaumeza mtego wake nyote sii Zitto au wanaChadema... Mkae chini muulizane nini matatizo yetu, na kwa nini hatuishi kugombanishwa ukweli ni upi..Chadema njooni na mafaili yenu mlopewa kuhusu Zitto na Zitto aje na mafaili yake alopewa kuhusu Viongozi wengine wa Chadema halafu mtayatazame mlinganishe ukwlei ndio mtajua kwamba nyote mlikuwa mkilishwa uongo..