RESOLVED HOJA Ushauri wangu: Mabasi ya abiria ya mikoani yaishie Mbezi Magufuli

RESOLVED HOJA Ushauri wangu: Mabasi ya abiria ya mikoani yaishie Mbezi Magufuli

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Stand tayari tunayo, hatuhitaji kila sehemu stand binafsi za watu. Order ndani ya nchi ni muhimu sana
Hakuna stendi binafsi za watu, Kuna Office binafsi za watu, halafu ni zuri sana zina hadi viyoyozi unapata baridi, unakunywa juice baridi wakati unasubiria bus bila kusumbuliwa na vibaka na wauza mayai.

Chukulia abiria aliyeshusiwa Shekilango kama vile aliyeshushiwa Kibamba.
 
Ktk historia ya DSM mnakumbuka kwamba mnazi mmoja ndio ilikuwa stand ya mabasi wakaja wakaisogeza ubungo mpk sasa ipo Mbezi , kilichokuwa kinasukuma yote hayo ni kuepuka msongamano wa mjini mnazi mmoja ilizidiwa wakaenda ubungo , ubungo ikazidiwa sasa wapi mbezi . Sasa tukiruhusu hayo mabasi yajijengee vituo kiholela working = to 0
Na mbezi wataitoa soon
Hatuna viongozi wenye mikakati,endelevu
Ni kama watu wanakuwa hawajuwi wanafanya nini!

Ova
 
2050 Hiyo stendi itageuzwa kituo cha SGR cha treni ya kuelekea Kaskazini ili tuendeleze vizuri legacy ya SGR ya JPM. 2050 itakuwa ni ushamba kusafiri kwa bus kwa zaidi ya Km 100.
Ndio maana wale vibosile kule migodini zaidi ya KM fulani hatumii gari ni chopa tuu 🔥
 
Tatizo ni maono finyu
Tatizo ni fikra mgandamizo

Mwanza ina stendi mbili Nyamhongolo na Nyegezi ambalo ni jiji la pili, likiwa na manispaa mbili tu.

Dar es salaam lenye manispaa Tano(05) lina stand Moja kama chupa ya chai, stand ipo zaidi ya kilomita 30, watu mnaona ni sawa, tuko makini kweli?

Dar es salaam inahitaji stand nne(04) za ziada.

Njia ya Nyerere road Stand iwekwe maeneo ya Chanika.

Njia ya Kilwa road iwepo stand maeneo ya Mbagala.

Njia ya Kigamboni kupitia Mwalimu Nyerere bridge Mandela road.

Njia ya Bagamoyo road.

Halafu Ring road kuizunguka Dar es salaam yote bila kuingia City Center.

Hii ndio way to go.
 
Kwa mara ya kwanza nimekutana na uzi unatoa mawazo na suggestions za kujenga na sio mihemko ya kichawachawa, ni ukweli mtupu thinking za jiwe aka malaika wa chattle zilikuwa sometimes za ukweli, malori yote ishia kwala, vibajaj boda zote mjini marufuku, imarisha mwendokasi ziwe nyingi kila kona na bei chee, maisha yatakuwa kama ya wanadamu
 
Sioni a ya kila kampuni ya mabasi iwe na kituo chake cha kushushia abiria, inatosha wakiishia kituo kikubwa cha mabasi Mbezi Magufuli itasaidia kupunguza msongamano ktk mji na pia stendi ya Magufuli haitopoteza mapato na wafanyabishara watanufaika.
Uliona Nani anashuka pale stand ya magufuli kutoka kwenye mabasi ya mkoani? Acha ushamba unataka kuumiza wasafiri wanaotoka kigoma uwashushe mbezi halafu uwaibie?
 
Tatizo ni maono finyu
Tatizo ni fikra mgandamizo

Mwanza ina stendi mbili Nyamhongolo na Nyegezi ambalo ni jiji la pili, likiwa na manispaa mbili tu.

Dar es salaam lenye manispaa Tano(05) lina stand Moja kama chupa ya chai, stand ipo zaidi ya kilomita 30, watu mnaona ni sawa, tuko makini kweli?

Dar es salaam inahitaji stand nne(04) za ziada.

Njia ya Nyerere road Stand iwekwe maeneo ya Chanika.

Njia ya Kilwa road iwepo stand maeneo ya Mbagala.

Njia ya Kigamboni kupitia Mwalimu Nyerere bridge Mandela road.

Njia ya Bagamoyo road.

Halafu Ring road kuizunguka Dar es salaam yote bila kuingia City Center.

Hii ndio way to go.
Kuwa na stand za mabasi kila kona ya Dar es salaam sioni kama ni wazo zuri , kwa mtazamo wangu nashauri usafiri wa umma na barabara uzidi kuboreshwa ili mtu anayetoka sehemu yeyote ya mji aweze kufika stand main ya Magufuli terminal . Mtu akitoka mkoani anadandia usafiri wa mwendokasi unampeleka kwenye destination yake
 
Sioni haja ya kila kampuni ya mabasi iwe na kituo chake cha kushushia abiria, inatosha wakiishia kituo kikubwa cha mabasi Mbezi Magufuli itasaidia kupunguza msongamano ktk mji na pia stendi ya Magufuli haitopoteza mapato na wafanyabishara watanufaika.
Mimi na shauri utaratibu uwe kama inavyofantika sasa,ila usimamizi wa makusanyo ya tozo na kodi yaratibiwe kule gari inapo tumia kama maegesho yake ya kudumu tena isowe tozo holele,ziwe zenye kuhamasisha wamiliki kulipa bila usumbufu wala kero.
 
Uliona Nani anashuka pale stand ya magufuli kutoka kwenye mabasi ya mkoani? Acha ushamba unataka kuumiza wasafiri wanaotoka kigoma uwashushe mbezi halafu uwaibie?
Kaka punguza lugha kali toa hoja yako tu utaeleweka

Nakusahihisha , point yangu ni kwamba usafiri wa BRT uboreshwe kufika pale Magufuli terminal kwenda kona yeyote ya DSM , mabasi ya mikoani yaishie Magufuli
 
Kuwa na stand za mabasi kila kona ya Dar es salaam sioni kama ni wazo zuri , kwa mtazamo wangu nashauri usafiri wa umma na barabara uzidi kuboreshwa ili mtu anayetoka sehemu yeyote ya mji aweze kufika stand main ya Magufuli terminal . Mtu akitoka mkoani anadandia usafiri wa mwendokasi unampeleka kwenye destination yake
Wewe bila shaka ni mmojawapo wa Wafanyabiashara wa hapo Magufuli Stendi ndio maana umekomalia hivyo stendi 'kuu". Hatushuki hapo mkuu, tafuta tu sehemu nyingine ya kufanya biashara yako na kama kuna hirizi umefukia hapo muite tu mganga ahihamishie kwingine.
 
Mimi na shauri utaratibu uwe kama inavyofantika sasa,ila usimamizi wa makusanyo ya tozo na kodi yaratibiwe kule gari inapo tumia kama maegesho yake ya kudumu tena isowe tozo holele,ziwe zenye kuhamasisha wamiliki kulipa bila usumbufu wala kero.
Itakuwa ni hasara kwa mabilioni yaliyotumika kujenga stand ya Magufuli halafu isitumike na ma bus , uwekezaji uliofanyika pale ni mkubwa na una fursa kwa wafanyabiashara
 
Mimi na shauri utaratibu uwe kama inavyofantika sasa,ila usimamizi wa makusanyo ya tozo na kodi yaratibiwe kule gari inapo tumia kama maegesho yake ya kudumu tena isowe tozo holele,ziwe zenye kuhamasisha wamiliki kulipa bila usumbufu wala kero.
Tozo na kodi zote zikatwe kwenye tiketi na stendi gari inazoingia. Kodi nyingine za mapato wamiliki wa magari wanalipa bila kujali gari inalala wapi.
 
Wewe bila shaka ni mmojawapo wa Wafanyabiashara wa hapo Magufuli Stendi ndio maana umekomalia hivyo stendi 'kuu". Hatushuki hapo mkuu, tafuta tu sehemu nyingine ya kufanya biashara yako na kama kuna hirizi umefukia hapo muite tu mganga ahihamishie kwingine.
Naimani jamii forum ni jukwaa kubwa wenye mamlaka watasoma mawazo yangu .

Yani wewe siku ikitokea umepewa uongozi kwenye nchi hii utavuruga sana utaratibu Tanzania itakuwa kama jalala bila mpangilio , yani kabisa unaona sawa watu wajijengee stendi zao mji uwe zig zag
 
Back
Top Bottom