Define city centre kwanza, kama ni huku Mjini kkoo, posta etc hayaruhusiwi kuingia Muda wa kawaida ni asubuhi Sana ama usiku, unless ni mabasi ya kimataifa.
Ukipanda Ratco Kariakoo mchana unakutana na Costa ambayo itakupeleka mbezi ukapande basi.
Mabasi ya kimataifa yanayokwenda Mombasa, Nairobi, Kampala etc yanatoka Direct Mjini bila kupitia mbezi, yakifika ubungo wanakata mawasiliano kutafuta Tegeta.
Foleni haitakomeshwa kamwe kwa kulimit magari ya public kama hayo. Basi kama Hilo linabeba watu 40-60 wakimwagika mtaani hao kila MTU akichukua Bolt, bajaji, boda etc wanasababisha foleni kubwa kuliko ukiwakusanya wote kwa pamoja.
Long story short usafiri binafsi ndio husababisha foleni, kila MTU akitumia kifaa chake binafsi foleni ni kubwa, Uchafuzi mazingira mkubwa etc. cha muhimu usafiri wa Umma uboreshwe, mabasi yaongezwe, mwendokasi ziwe nyingi, Daladala ndogo zitolewe ziwekwe kubwa Tu zenye Nafasi, waweke daladala premium if possible Ku encourage watu wasitumie usafiri binafsi.