Ushauri wenu: Baba anataka kuuza mali, hataki kunigawia mimi mwanae

Wewe

Siku nyengine huna ajira

Siku nyengine unayo umeunganishwa na mama

Mala maisha magumu hata pesa ya kula huna

Mala una pesa nyingi mpaka unanunua viwanja

mala unaulizia gari la kununua

Leo tena jana hukuwa na pesa ya kula
Ni stori tu, kwanza ukiangalia sababu ya kufukuzwa wala haina mantiki eti kujiunga na chama tu ndio iwe shida hivyo
 
Eti jasho lake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Vipi hao wadogo zako nao walipewa urthi? Kuna mahalo baba yako anasema atauza Mali na atawagawia wakajiendeleze huko waliko.
 
Ushauri wangu kwako mkuu baba yako hana kosa amekusomesha mpaka degree 1 sasa mkuu ingekuwa mimi nikusepa mbele kwa mbele pambana hizo ni mali za mzee akiamua akupe sawa,

Hii stori yako ilitaka ifanane na yangu mimi nami mzee wangu alipostaafu uhasibu alipata kiinua mgongo kama milioni 63, sasa mimi nilimwomba mzee wangu anipatie milioni 5 tu nianzie maisha kauli aliyonipa mzee kwamba hizi ni fedha zangu wewe nimekusomesha tumia taaluma yako katika maisha nilisikitika sana ila baada ya kukaa chini na kutafakari nimemuona mzee yupo sahihi.

Ndiyo kama wewe, wewe ni mtoto wa kiume miaka 39 unataka kurudi nyumbani kufanya nini pambana na maisha mkuu, halafu nazani huna mke wala mtoto umri unasogea mbele usipokuwa makini uzee unabisha hodi huna mtoto,

Mkuu pambana na degree kichwani, ningekuwa mimi ni wewe ningeandika mchanganuo wa kazi na kumpelekea mzee na kumwambia mzee utanisaidiaje hapo!! Na siyo kurudi nyumbani Kula na kulala!!!

Pole Mkuu!! Hii ndiyo dunia, wahenga walisema kuwa uyaone, na sasa unayaona!!
Nawasilisha maoni yangu, mzee yupo sahihi kabisa mkuu!!
 
mkuu uyu mzee sasaivi nahisi ametawaliwa na roho mbaya sana, nataka nipate na mimi maali siwezi kubali jasho langu lipotee mkuu.
We fala Sana una jasho gani kwenye Mali za mzee wako hembu elezea
 
Yaani umenyoa mavuzi kwa baba yako hadi umefikia umri huo bado hutaki kutoka kwake? Umemkosea heshima sana mzee wako.
Nakushauri tafuta mume wa kukulea waache wazazi wako wamechoka na kuzeeka sasa
Hapana mkuu mimi sina shida yeyote, pale ni kwetu mkuu na nina haki ya kupata mgao sawa sawa
 
Yaani usomeshwe mpaka chuo kikuu halafu bado unalazimisha uishi kwa dingi, pambana upate vyako!
 
Muombe mama yako laki mbili uanze kufuga kuku wa mayai. Anza na kuku 40 hiyo chenji utanunua chakula Chao na dawa. Mwakani mwezi wa sita you will be a very different man.

Mzee nae atakapokuona uko serious na kuku atajua umeacha ujuha. Atakuruhusu ukae hapo kwake kwa miezi hii kumi iliyobaki ya mwaka huu.

Baada ya miezi mitatu mkope mzee laki mbili Anza kuuza chips hapo hapo nje kwenu.
Lakini kwanza kabisa jiondoe CCM ili kuondoa akili za kisukule kichwani.
 
Miaka 39 upo nyumbani.. mwakani tu si unatoboa miaka 40... Unasubiri ajira hapo nyumbani... Utafute ajira uoe uwe na familia yako si miaka 70 imeahafika
 
Miaka 39 unalilia mali za baba yako? Umri wako huo ni wa kuitwa baba anayejitegemea. Kifupi hakuna mzazi anakataa mtoto wake. Ukiona amekukataa basi kuna mambo ambayo kwako ni mabaya mno. Na unavyojieleza tu wewe ni mzigo kabisa na mwekekeo wa maisha huna. Na kama hujaoa kwa umri ulio nao basi andika maumivu.

Baba yako katafuta mali zake na ana uhuru nazo. Taifa za kwako broo.

So sad for you.
 

Mkuu

Mzazi anapokataa kukupa Mali zake ujue anakusaidia.

Kaa Chini, tafakari, jipange utafute zako. Ukizipata mwenyewe atakutafuta!
 
Mkuu si utafute za kwako????
 
Mkuu kwanza nikupe pole. Ila tahadhari mali au urithi haulazimishwi mkuu labda mimi ndio sijui mambo ila mwenye mali ndio ana mamlaka ya kusema nani apewe nani asipewe. Zaidi navyo juwa ukiforce mali za urithi huwa hazina mwisho mzuri so kuwa makini mno hizo zina mwenyewe na amesha sema hataki uguse juwa kinyume na hapo hazita kupeleka pazuri jihadhari mapema
 
Picha nayopata mimi kama ndo hii hii aliyonayo mzee wako basi hata mimi ningekutimua;
1. Miaka 39
2. Degree 1
3. Akili kisoda
4. Una tamaa kali ya mali zisizo zako na unaweza kuua ili kupata mali.
Baba kastuka unaweza kumuua kwa sbb ya mali so anajidistance na ww.
Lkn kweli unagombania urithi tena kwa wazazi walio hai?
 
Si amekuleta hapa duniani, amekulea, amekusomesha na unataka nini kingine? Mali siyo zako hata kama amerithi kwa baba yake, katafute za kwako, Nyambafu ukweli wewe?
 
Ila kuna watu mnafurahisha na kuhuzunisha sana, mali za nani? Zako au za baba yako? Ulimsaidia kutafuta? Hajakusomesha? Una miaka 40 unalia lia? Nani kakuambia ukimpeleka Mahakamani utashinda? Angalia usijewekwa ndani wewe.

Acha kuwa taahira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…