Upo mkoa gani?
Ukisha jibu hili swali ndipo itakua rahisi kukushauri kutokana na mkoa ama wilaya uliyopo.
Lakini pia kwaharaka nilicho kiona kwako wewe sio mfanya biashara kwasababu hadi hapo ulipo ungekua tayari umesha anza kupata walau wazo la biashara kadhaa (watu wa hivi wapo). Lakini pia hii haikufanyi usijifunze kufanya biashara sababu Mungu alimpa binadam maarifa ya kujifunza, lakini wasiwasi wangu ni kwamba kama hiyo pesa ndio akiba yako pekee... kwanini utake risk kujifunzia biashara?? (Ulipaswa ujifunze biashara wakati mshahara unaendelea kuingia).
Hivyo basi, kwanza nakushauri ujenge nyumba ndogo ya room moja, bebule, choo/bafu na jiko. Hii naamini ukiisimamia mwenyewe haitizidi 25 millions.
Baada ya hapo endelea kutafuta kazi huku ukiweka hata genge la matunda, nyanya, vitunguu, mboga hapo maeneo ya utakapo jenga nyumba yako.
Kaa kwenye kijiwe chako kipya ambacho walau utatumia sio zaidi ya 2 milions kukijenga kwa mabanzi pamoja na mtaji na kisha pesa iliyo baki fanya kuitunza bank.
Baada ya hapo endelea kutafuta kazi online wakati tayari unauhakika wa kipato kidogo cha kukuwezesha kujikimu kwa chakula na mambo madogo madogo.
Ukilifanya hili ninaamini utafanikiwa na kazi nyingine utaipata kwasababu hapo toka itakua nikama umepata experience